The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Tanzania inaendelea kuona ongezeko la shule binafsi jambo ambalo ni zuri na sina shida nalo hata kidogo. Tuliosoma enzi za ujima waliosoma shule hizi tuliwaona mafogo kinoma. Kwanza kwa sisi tuliokuwa nje ya Dar hatukuwahi kusikia school bus, ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa eti kuna chalii anafuatwa nyumbani na gari la shule kisha jioni kurudishwa nalo. Ilikuwa ni ajabu sana.
Leo hii, kila mahali tunapishana na mabasi ya njano. Njano iliyokolea, njano iliyofifia – yaani all shades of njano. Na yapo katika maumbo mbalimbali – madogo, size ya kati na makubwa. Yote yapo kazini. Nimewahi kukutana na Noah imegongwa rangi fulani inayokaribiana na njano ikiwa imebeba wanafunzi kibao, na imeandikwa school van
Katika baadhi ya mataifa, kwa mfano Marekani na Canada, utakuta kila basi la shule limepakwa rangi ileile kabisa - rangi ambayo rasmi inajulikana kama "National School Bus Glossy Yellow". Ni rangi ya taifa ya kutambulisha magari hayo. Hii inasaidia magari haya kuonekana kwa urahisi na waendeshaji wa magari mengine.
Moja ya sababu kuu za kufanya mabasi ya shule kupewa rangi ya njano ni kuwa imebainika kwamba rangi hiyo inavuta macho haraka zaidi kuliko rangi nyingine yoyote. Hata kama ukitazama moja kwa moja mbele, unaweza kuona kitu cha njano ambacho hakipo moja kwa moja mbele yako. Wanasayansi wamegundua kwamba watu wanaweza kuona vitu vya njano katika pembe za macho mara 1.24 zaidi kuliko rangi nyekundu, kwa mfano. Tofauti na rangi nyekundu, njano pia inaonekana kwa urahisi zaidi katika mazingira ya giza.
Lakini pia, kuna suala la usalama. Si kila gari limetengenezwa kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Hapa kwetu ukiwa na ki-Hiace twende, ukiwa na Coaster sawa, ukiwa na Heicher pia fresh tu. Kwa wenzetu wenye mifumo inayoeleweka magari ya kubebea wanafunzi yanatengenezwa mahususi kwa kazi hiyo. Si kila gari linaweza kutumika kubeba wanafunzi. Hii ni kwa sababu za kiusalama zaidi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, magari ya shule hutumia teknolojia inayoitwa 'compartmentalization' – ambao ni mfumo unaohusisha viti vyenye muundo maalum unaolenga kulinda abiria, hasa watoto, wakati wa ajali. Hata hivyo, mfumo huu unapunguza tu uwezekano wa kupata madhara makubwa, ila hauzuii kabisa madhara kwa 100%. Sasa, unadhani nini kinaweza kutokea kwenye magari yanayobeba wanafunzi ambayo hayana usalama wa aina hiyo na hayana mikanda? Nadhani sote tunaelewa udereva wetu tuwapo barabarani. Ni vurugu tupu!
Niliwahi kukutana na hili basi (picha hapo juu) Arusha. Ndani halina hata mikanda ya usalama. Linabeba wanafunzi kibabe tu kwakuwa eti lina rangi ya njano. Niliwaza dereva akishika breki ya ghafla watoto si watapaa.
Nadhani ifike wakati mamlaka zinazohusika zitengeneze au ziweke wazi standards ambazo wenye shule wanapaswa kuzifuata likija suala la magari ya kubeba wanafunzi. Siyo gari halina emergency exit, halina fire extinguisher, limezidisha idadi ya wanafunzi hadi wanabebana, halina mikanda ya usalama n.k. Nadhani tusibaki tu kwenye rangi, ni muhimu tuwe na tafsiri ya basi la kubeba wanafunzi. Kuwe na vigezo maalum ili hata wazazi wawe na taarifa kuwa watoto wao wanasafirishwa kwa usalama au la.