Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Sinzonje ni magufuri nyumba ni tz, tulikaa balazani tukasikia kelele hichi ni kipindi cha lowassa kutangaza nia akiwa ccm makada wa ccm walipiga kelele walioaminishwa kuwa lowassa fisadi yaani kelele zilitoka ndani ya ccm, namtu aliyeruka dirishani ni huyohyo magufuri maana kwawaliotangaza nia ya urais magufuri hakuwemo akaja kuchomekwa tu ndo aliruka dirishani, na ndo anakalibishwa kuyaona matatizo ya nchi yetu, hii ndo myumba yetu tuliyoficha mundu za kupondea wezi yaani tz serekali yetu imeficha makucha dhidi ya mafisadi kwenye vyumba vitatu havifunguki sielewa ila kwenye kimoja hakina mlango japo kuwa kinawatu ndani hawaongei kiswahili hapo kaongelea wachina wamejazana na wanapata ajira ila wenyeji wanaolala sebuleni ni sisi watz hatuna ajira lakini wachina wanapata ajira na tunawaona ndo maana chumba chao kipo wazi, na wapishi hapo wametajwa ni akina kikwete mkapa na kundi lao ndo wanaopikia mpango mzima wa nchi, nawanasubilia tu dakika hizi za kwanza ziishe waanze kumwongoza njia zao zote za wizi apitie ndo wanamsubilia ale alale akiamka tu waanze kumwongoza,anaambiwa akiwa makini kwa nje atasikia kelele ni za vijana wa ukawa wamevalia gwanda za khaki✌✌✌, na ukiona tembo analinga hapo ujue mvua zimekalibia ni lowassaaa hashituki hatishwi anajiamini ukombozi umekalibia 2020 pipooooozzzzzzzz ✌✌✌✌✌ lowassaaa tena 2020 uelewa wangu umekomea hapo!!!
 
If you take time and listen... I think there are really wonderful jewel build inside this poetic song "sizonge"
 
Duh!wacha nami nitoe nilichoelewa vyumba vinne ni awamu zilizopita vitatu vinafunguka ina maana awamu ya kwanza mpaka ya tatu ya nne haina mlango ndo anasema usiingie mwisho nitakwambia kwa nini!kuhusu makaburi ni uozo wa uongozi uliopita so anasema yakifukuliwa kuna haja ya kuzika tena?
 
Fasihi huwa inamaana pana sana ila mi nilivyoelewa Sizonje ni kiongozi tulienae sasa na nyumba yetu ndo taifa letu milango ipo ila wanapitia madirishani yaani watu hawafuati utaratibu mfano kutoa mizigo bandarini kwa kutolipia kodi na kupitia dirishani nyumba ina vyumba 4 vitatu havifunguki na kimoja hakina mlango na watu wamo na hawaongei kiswahili hii ni kwamba awamu tatu za mwanzo zilikua zimefunga mianya ya unyonyaji na ufisadi ila awamu ya nne imekua wazi na kuwaacha wageni wafanye watakavyo na mengine mengi kama wimbo unaofaa humbembelezea mtoto na harufu ya uzazi haishi mpaka mtoto akue ni kuwa sera za Sizonje ni nzuri lakini taifa hili bado linanuka rushwa wizi na ufisadi wa hali ya juu na hali hiyo itakua sawa mpaka taifa litakapo kua
 
At least nimepata mwanga.
 
Mpoto mwenyewe kahojiwa kasema ye mwenyewe haelewi..Anaendelea kuusikiliza zaidi ili apate maana..
Mh mh kweli?? Ila ile nyimbo nzuri Sana kwa kweli
 
Shukran kwa uchambuzi wako mkuu
 
Milango ipo wanapita madirishani.. = Sheria, taratibu na kanuni za kazi zipo lakini watu wanapindisha sheria na kufanya yao (wanapiga dili)
Hii je imekaaje ukiona tembo anaringa jua mvua zinakaribia
 
At least nimepata mwanga.
Shukran mtunzi kaficha tafsiri ili hadhira ishiriki kutafakari kwa namna mbalimbali.Nyumba yetu ni ikulu ndipo tulipoficha silaha zetu yaani nguvu ya kupambana na adui na jikoni ni wizara ya fedha shimo la taka ni ajira kwa vijana wetu wanawaambia zipo lakini hazipo au kwa mchongo ndo zinatoka.nawe unaweza kuleta uelewa wako.
 
sizonje ni raisi mpya as msanii anavyomwita kama mkombozi na kama watanzania wanavyoamini.

wimbo umejaa kwenye nyumba ambayo kwa mara ya kwanza binafsi nilidhani ni tanzania lakini vijana walioshika bahasha za khaki(wasaka ajira) wanaouliza KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI? wanaonyezsha wazi kuwa nyumba ni serikali ya tanzania na wanachouliza ni KAMA HAMTUPI AJIRA MLITUSOMESHA KWA NINI?.
IDADI YA VYUMBA:kama ilivyosemwa kuwa nyumba ni serikali na kawaida ina mihili mi3 ila hii ya kina msanii ina vyumba vinne(mihimili mi4) mahakama,bunge,serikali ndio vile vyumba vi3 ambavyo havifunguki(havisikilizi wananchi) na cha nne ni watu toka ng'ambo ama mataifa makubwa ndio maana hakia mlango(hakihusiani na vyumba vingine wala wananchi) na hawaongei kiswahili kuonyesha ugeni wao

JIKO:jiko ni idara mbalimbali kama BANDARI,BENKI,TANESCO N.K...huko ndo kuna wizi sasa na wanahusiana sana na watu kama sizonje(raisi) ndo maana wanaulza anapenda vya aina gani????

CHUMBA KISOFUNGULIWA:sizonje mkkmbozi...chumba hiki kina picha(baba) na mchoro wa picha(huyu anaweza kuwa mwana wa baba) kwakuwa kulikuwa na picha na kisha ukaja mchooro.kulikuwa na baba na kisha mwana.pengine sizonje hatakiwi kufungua humu ndani maana kuna mabalaa yakutosha na yatazua makubwa.na maneno ya USOMTAKA KAJA kwani mwenye chumba alimtaka sizonje(baba)?

SHIMO NA CHOO:wachafu kutoka serikalini hatuwaoni mahakamani wala gerezani....

NB...MUONO HUU UNAWEZA KUWA TOFAUTI NA LENGO LA MSANII
 
kwenye kiitikio inaonyeshwa wazi kabisa pale msanii anapomkaribisha sizonje(raisi) kwenye nyumba(serikali)

kwenye kelele nadhani ni maswala ya chaguzi za vyama.kwani kuna mtu aliruka toka chama cha nyumbani kwa njia ya mazonge? ndo huyo wa dirishani labda AU kama mhakiki anatakiwa ayajue maswala yanayomtukia msanii na kumzunguka kilichotokea dirishani ni makonteni yaleeee...ya kule baharini na kulikuwa na kelele kweeeli...

maiti ilofukuliwa yaweza kuwa mafisadi wanaosafishwa sasa hivi.tushawafukua na kuuona uozo wao tunawazika ili iweje tunaficha nini?
 
Sawasawa.
 
Mpoto mwenyewe kahojiwa kasema ye mwenyewe haelewi..Anaendelea kuusikiliza zaidi ili apate maana..
Duh hii kali; lakini inawezekana maana jamaa nyimbo zake nyingi anatungiwa.
 
NIMEMUELEWA ALIPOSEMA VIJANA WENYE BAHASHA ZA KAKI WANAOLALAMIKA KUTOTUMIWA KWA VYOO NA MASHIMO YA TAKA,KAMAANISHA VYAMA PINZANI HASA CHADEMA(GWANDA ZA KAKI)
 
Mpoto mwenyewe kahojiwa kasema ye mwenyewe haelewi..Anaendelea kuusikiliza zaidi ili apate maana..

Hahahahaahhhh....
Mkuu embu kuaa serious😀:lol:
 
Wachangiaji mmenisaidia sana at least nimeanza kuuelewa huu wimbo. Ama kweli penye wengi kuna mengi. Ngoja niendelee kuusikiliza tena.
Ila neno "sizonje" ni la kilugha ama ni kiswahili fasaha??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…