Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Sizonje = Magufuli

Nyumba yetu = Nchi ya Tz

Wanapita madirishani = Rushwa

Makaburi yaliyofukiwa lazima yazikwe upya = Mambo ya zamani kwa nini uyafukue? (Wala rushwa kama akina Tiagi masamaki na HSC).

Chumba hiki usiingie = Usilijadili swala la HSC

Wenyeji wanalala sebuleni = Watanzania walalahoi hawana kazi na ofis nyeti wameshika wageni.

Kule tulikotoka wanaita jikoni = Hii ni awamu ya JK, full kujiachia na siri za nchi nje nje.

Chumba hakina mlango na waliomo hawazungumzi Kiswahili = Wageni wanaingia nchini bila vibali na kufanya kazi.

Usiyemtaka kaja = Wengi walikuwa hawamtaki Magufuli awe Rais sasa kawa.
 
Wenyeji hawatupi taka jalalani.....soko la ajira wenyeji hawapati ajira na ajira ni za kujuana
 
Mpaka sasa hakuna MTU aliyeelekea kuelezea vizuri huu wimbo
Huyu mpoto sio mtanzania wallah mnajaribu ila mmeshindwa ngoja nisubiri wengine
 
Pwilo ipe akili yako nafasi ing'amue..... Mfano hapo Banana anaposema tumekaa barazani mara tunaona wanaruka madirishani.... Huwezi kuona hapo hao ni ile kamata kamata kule TRA na Bandarini? Maana walikurupushwa toka sebuleni..!!
 
Ukimuona tembo anaringa ujue mvua imekaribia kunyesha
 
Harufu ya mama mzazi haiishi mpaka mtoto akue = Huwezi kumaliza swala la rushwa kwa mwezi mmoja wakati watu walishajenga kuwa maisha yao yatajikita kwenye rushwa...

Mtoto hauungui kiazi kilichoko kwenye kiganja cha mama yake = Mfano wewe ni mfanyakazi wa TRA na Waziri Mkuu Majaliwa anataka kupitisha mzigo wake bila kulipa kodi, wewe uliyeko huko TRA huwezi kutiwa hatiani maana issue ni ya mkubwa na wewe umeagizwa kutekeleza maagizo.
 
Vyumba vitatu havifunguki = Hii ni ile mikataba iliyofanywa siri na serikali n,a wananchi hawajui yaliyomo. Mfano ni ile mikataba 17, JK aliyosaini na Xi Jinping.

Kile kimoja kilicho wazi na waliomo hawazungumzi Kiswahili = Hii ni mipaka ya nchi, wageni wanaingia kiholela na kupata vibali vya kuishi kinyume na utaratibu..
 
Wapishi = Wachonga madili kama yule Mhindi wa IPTL..
 
Milango ipo wanapita madirishani.. = Sheria, taratibu na kanuni za kazi zipo lakini watu wanapindisha sheria na kufanya yao (wanapiga dili)
 
Siku za hivi karibuni Msanii Mrisho mpoto katoa Wimbo wake ambao unaitwa SIZONJE na kasema Yakuwa Sizonje maana ake ni Ukombozi! Sasa mistari yake nimeona Niilete hapa tuijadiri nakuijua Vizuri nini Anamaanisha na nani Anazungumziwa hapa!

Najua ya kuwa wanasiasa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa humu wapo wengi na watu wenye uelewa Mkubwa

Natambua ya kuwa mambo aliyo yazungumzia Mrisho mpoto ni yale current katika Nchi yetu! Tafadhari toa maana ya mstari utakao kuwa unajua maana yake,kama huwezi tuwe wavumilivu wengine watakuw wanatusaidia! Ila navyo jua kaimba mambo mengi na ya muhimu kujadiriwa hapa!

Anaanza kwa kusema
-Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
-Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
-Tulikaa barazani, tukasikia kelele,Kelele toka ndani, mtu anaruka dirishani,Sizonje, karibu nyumbani kwetu,Uone maajabu ya nyumbani kwetu

Mrisho anaendelea kwa kusema
-Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu,Tulipoficha mundu za kupondea wezi
-Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?
-Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne,Vitatu havifunguki, kimoja hakina,mlango Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili
-Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea
-Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika
-Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako Wanashangaa mbona ghafla
-Samahani sana mgeni Wapishi wameniomba kwamba Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
-Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
-Sizonje chumba hiki naomba usiingie Ukimaliza nitakwambia kwanini
-Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
-Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa! Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
-Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa “USIYEMTAKA KAJA”
-Hatukuwahi kuelewa maana yake Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia
-Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto Na kamwe mtoto hawezi kuungua
Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
-Njoo huku uone Sizonje Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?
-Sawa, Sizonje, huu hapa ni ua Lile pale ni shimo la taka Na kile pale ni choo Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka Wala kwenda chooni
-Kama ukiwa makini Kwa nje utasikia sauti za makundi ya
watu
-Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi
-“KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?”
-Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje Kuna watoto, wazee na kina mama Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele
-Ninavyosikia, ila sina uhakika Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao Na wana haki ya kutupa taka na kutumia
choo hiki
-Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni Uone maajabu mengine ya nyumba hii
-Sizonje, ukiona tembo anaringa Ujue mvua zinakaribia!
Hapo kamaliza!
 
Karibu sana sizonje hii ndio nyumba.....
Sasa hivi wanakupikia ule ulale.......
Kwani makaburi yalifukuliwa ni lazima yazikwe upya.....

Tafakari utanielewa
 
Back
Top Bottom