Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Mpoto....Akijitahidi kwa nyimbo zenye ujumbe kama huu...Na akiweza kutunga Vitabu...May be anaweza kumfikia Almaruhum Shabani ROBERT....Lakini afanye kazi....!...Kwani Shabani Robert ni Gwiji wa KISWAHILI...
 
Jamani Mrisho Mpoto amenishinda...
Huu wimbo wake mpya wa Sizonje naupenda japo nimejitahidi kuuelewa ila hadi sasa sijafanikiwa kuelewa hata mstari mmoja wa shairi lake.
Naomba tusaidiane hapa.
Hiki ndo kiitikio
.....,............................
Sizonje hii ndio nyumba yetu,
milango ipo wanapita madirishani,
ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu.
 
Jamani Mrisho Mpoto amenishinda...
Huu wimbo wake mpya wa Sizonje naupenda japo nimejitahidi kuuelewa ila hadi sasa sijafanikiwa kuelewa hata mstari mmoja wa shairi lake.
Naomba tusaidiane hapa.
Hiki ndo kiitikio
.....,............................
Sizonje hii ndio nyumba yetu,
milango ipo wanapita madirishani,
ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu.
Sizonje hii ndiyo Tanzania yetu,Mipaka ipo ila wanapita kinyemela.........niendleeee???
 
Sizonje hii ndiyo Tanzania yetu,Mipaka ipo ila wanapita kinyemela.........niendleeee???
endelea ndugu...
anasema...
Hii ndio nyumba yetu tuliyofichia mundu za kupondea wezi.
Kwani makaburi yaliyofukuliwa ni lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje inavyumba vinne, vitatu havifunguki na kimoja hakina mlango japokuwa kunawatu ndani na hawaongei kiswahili.
Wenyeji wanalala sebuleni na walishazoea.

Twende kazi...
 
endelea ndugu...
anasema...
Hii ndio nyumba yetu tuliyofichia mundu za kupondea wezi.
Kwani makaburi yaliyofukuliwa ni lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje inavyumba vinne, vitatu havifunguki na kimoja hakina mlango japokuwa kunawatu ndani na hawaongei kiswahili.
Wenyeji wanalala sebuleni na walishazoea.

Twende kazi...
sizonje wageni wanalala chumbani wenyji sebulen means that Wageni ndio wanaoshika nyafifa nzuri serikalini au katka makampuni ila wazawa lol.......niendleeee
 
Hapo ni mstari gani mkuu au yote maana naona humu kaongelea mambo mengi hadi ukosefu wa ajira kama sijakosea kwenye ule mstari wa bahasha ya kaki
hahahaaaAAAA bahasha ya kaki!!!
 
Kutafsiri shairi sio kaz rahs n bora hata upewe riwaya utaelewa kinachoendelea but all in all wimbo unahusu maisha ya mtanzania
 
Habari Zenu Wakuu, Juzi Kati Katika Pitapita Kwenye Social Network Nikabaatika Kusikiliza Nyimbo Mpya Ya Mzee Wa Asili Na Mfalme Wa Kughani Mashairi Mrisho Mpoto Ngoma Inaitwa Sizonje, Baada Ya Kusikiliza NaKuitafakari Kwa Kina Wimbo Huo Nikabaini Kuwa Mtajwa Na Mlegwa Mkuu Wa Ujumbe Huo (Sizonje) Ni Raisi Magufuli na Nyumba Yetu Ni Tanzania,
 
-Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto Na kamwe mtoto hawezi kuungua
Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
-Njoo huku uone Sizonje Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?

ninachokihisi hapa ni kumsema. Magufuli. kuwa yeye ni kama mtoto anavyojifunza mambo mengi ya kimaisha kuna wakati hukosea mathalan wakati wa kujifunza kutembea huweza kuanguka na sheria ya maumbile haina huruma anapoanguka huumia hapo hapo na mama humuonea huruma. mtoto wake kwa kumfariji kwa kumpa matumaini

na kiazi kilichoko kwa mama ...ni uongozi wa nchi ...bado mwenyekiti wa ccm ni kikwete na magufuli yupo madarakani kwa nguvu ya chama. na afanye ayafanyayo katika madaraka yake ya urais ni ccm ndio itakayopata misukosuko itakayosababishwa na utendaji na maamuzi yake ya Urais

Njoo huku Magufuli harufu ya uzazi haishi. mpaka mtoto akue....wewe Magufuli bado mtoto kisiasa subiri uive kisiasa ndipo uachiwe uongozi wote wa Nchi
ni kumuasa Magufuli kuwa yeye ni bado mtoto kisiasa asiache kuongozwa na mama yake ccm na kujitakia misifa ya ovyo ovyo kuwa amekuwa mkubwa mama ni ccm na kiongozi wa ccm ni Kikwete. kwa maana hiyo Magufuli hawezi kuhimili misuko suko ya kisiasa. pekee bila ya kuongozwa na mama yake ccm
 
Back
Top Bottom