Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Sizonje = Magufuli

Nyumba yetu = Nchi ya Tz

Wanapita madirishani = Rushwa

Makaburi yaliyofukiwa lazima yazikwe upya = Mambo ya zamani kwa nini uyafukue? (Wala rushwa kama akina Tiagi masamaki na HSC).

Chumba hiki usiingie = Usilijadili swala la HSC

Wenyeji wanalala sebuleni = Watanzania walalahoi hawana kazi na ofis nyeti wameshika wageni.

Kule tulikotoka wanaita jikoni = Hii ni awamu ya JK, full kujiachia na siri za nchi nje nje.

Chumba hakina mlango na waliomo hawazungumzi Kiswahili = Wageni wanaingia nchini bila vibali na kufanya kazi.

Usiyemtaka kaja = Wengi walikuwa hawamtaki Magufuli awe Rais sasa kawa.
Nadhani chumba hiki usiingie itasadifu sana mgogoro wa zanzibar!
 
Sizonje = Magufuli

Nyumba yetu = Nchi ya Tz

Wanapita madirishani = Rushwa

Makaburi yaliyofukiwa lazima yazikwe upya = Mambo ya zamani kwa nini uyafukue? (Wala rushwa kama akina Tiagi masamaki na HSC).

Chumba hiki usiingie = Usilijadili swala la HSC

Wenyeji wanalala sebuleni = Watanzania walalahoi hawana kazi na ofis nyeti wameshika wageni.

Kule tulikotoka wanaita jikoni = Hii ni awamu ya JK, full kujiachia na siri za nchi nje nje.

Chumba hakina mlango na waliomo hawazungumzi Kiswahili = Wageni wanaingia nchini bila vibali na kufanya kazi.

Usiyemtaka kaja = Wengi walikuwa hawamtaki Magufuli awe Rais sasa kawa.
Kwa mbali ni kama umeutendea haki ng'amua zaidi na vilaza waelewe....
 
VYUMBA VINNE NI AWAMU ZA MARAISI WALIOPITA HAPA TANZANIA SASA MAGHUFULI(sizonje) NDO ANAKARIBISHWA AWAMU YA 5 AJIONEE UPUUZI ULIOKO
 
[Chorus – Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

[Bridge – Banana Zorro]
Tulikaa barazani, tukasikia kelele
Kelele toka ndani, mtu anaruka dirishani
Sizonje, karibu nyumbani kwetu
Uone maajabu ya nyumba yetu

[Verse 1 – Mrisho Mpoto]
Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu
Tulipoficha mundu za kupondea wezi
Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne
Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango
Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni
Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
Sizonje chumba hiki naomba usiingie
Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa
“USIYEMTAKA KAJA”
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia

[Chorus – Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

[Verse 2 – Mrisho Mpoto]
Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto
Na kamwe mtoto hawezi kuungua
Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
Njoo huku uone Sizonje
Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?
Sawa, Sizonje, huu hapa ni ua
Lile pale ni shimo la taka
Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi
Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka
Wala kwenda chooni
Kama ukiwa makini
Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu
Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi
“KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?”
Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje
Kuna watoto, wazee na kina mama
Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele
Ninavyosikia, ila sina uhakika
Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao
Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki
Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni
Uone maajabu mengine ya nyumba hii
Sizonje, ukiona tembo anaringa
Ujue mvua zinakaribia

[Chorus – Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

Nadhani:- ni Nchi yetu, watu wapitao dirishani ni akinani? Sauti za kelele je? wasiotupa taka na kwenda chooni,

Malenga mwagikeni nipate ujumbe hapa
 
dah mi mwnyewe huyu mtu simuelew maana huwa namsikia anaozungumza tu na sio kuimba.....ila nahis sizonje ni jpm na nymba ni tz
 
Sizonje ni State house ! Dedication kwa ankal magu! Soma vizuri na digest hizo lyrics kisha changanya na zako!
 
mi huwa naskilizaga beat na chorous kweny nyimbo zake
 
Nimeweza kung'amua machache

Sizonje- uncle Magu...rejea "usiye mtaka kaja"

Shimo la taka na Choo- ni sheria na taratibu ambazo viongozi hawazifuati, wanafanya watakavyo
 
Ikiwa Sizonje ni presidaaa sawa lakini hawa wanapita madirishani ni akina nani?,Milango ipo wanapita madirishani, hawa wasiotupa taka wala kwenda chooni je?
Jinsi ajira za bongo zinavyopatikana (mlango wa nyuma type) hao wengine ni vijana wanaotafuta kazi/ajira......personal opinion
 
Nilivyouelewaa mm ni kuwa;;;
Anaposema
Sizonje hii ndo nyumba ytu.
Rais magufuli hii ndo nchi yetu tz.
Mlango upo wnpta madirishan.
Watu hawafuati sheria na taratibu zilizowekwa Bali wanapita njia za mikato kukamilisha mambo yao binafsi.
Njia za panya.
Ingia uone maajabu ya yumba yetu..
Yaan karibu katikaa urais uone jinsi nchi hii ilivyokuwa na mambo mabaya yanayofanyika.

Tulkaa brzan tukskia kelel
Kelel tok ndan MTU anaruk dirshn

Yaan ss wananchi tunashuhudia watu wankmatwa na kes kubwa za kuhujum taifa .
Vyombo vya hbar vitapiga kelel kutangaza Lkn watapindish kes kupitia njia za panya itaishia hukohuko juu.

Tukipofcha mundu za kupondea wez

Nchi inawanasheria na wanadiplomasia weng tyu wanaoweza kutetea haki

Vyumba vitatu havifnguk
Ni ile mikataba iliyosainiwa na serikal iliyopita MF ile 17 ya rais wa China.
Haiwez kuvunjwa na ni siri ambayo wananchi hawaijui.

Kimoja hkina mlango japo kuna watu ndan hawaongei kiswhil
Yaan nchi imefungwa mipaka yakee lkn bado wazunguu wengi wanaingia na wanafnya wanachotaka.
 
kama unashindwa kuelewa maana hata ya ushairi wa sizonje utaweza kung'amua chochote kweli kwenye poetry za elton john kama nikita,daniel kweli?!
 
kama unashindwa kuelewa maana hata ya ushairi wa sizonje utaweza kung'amua chochote kweli kwenye poetry za elton john kama nikita,daniel kweli?!

Poor contribution ever, umesoma fasihi kweli wewe? unahisi fasihi ina jibu moja kama ilivo 1x1=1? majibu ya uchambuzi wa fasihi andishi yanaweza kuwa zaidi ya million katika mstari mmoja tu wa ushairi. Na ndo maana ktk yoyote ile utakutana na swali likikutaka ueleze nini dhima ya mwandishi ktk tungo husika, wakati mwingine ukitakiwa kuelezea mafanikio ya mtunzi ktk tungo husika.

HABARI za Elton John was not my concern, nimemwongelea Mrisho Mpoto ktk Sizonje. Na kutumia hiyo heading haina maana sijamwelewa bali kukusanya mawazo ya watu mbalimbali kabla ya kujeneralize.
 
Lile pale ni shimo la taka
Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi
Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka
Wala kwenda chooni
Shimo la taka na choo mie nilidhani ni kuwatimua na kuwafunga wasiofanya kazi au wabadhilifu. Lakini hayo mashimo hayatumiki.
 
Asante hauko mbali na mtizamo wangu, shimo la taka au choo hakika ni Magereza ambayo watawala wamejikuta wakishindwa kuyatumia kutupa takataka ndani yake, Takataka ni mafisadi, wala rushwa, nk
 
Poor contribution ever, umesoma fasihi kweli wewe? unahisi fasihi ina jibu moja kama ilivo 1x1=1? majibu ya uchambuzi wa fasihi andishi yanaweza kuwa zaidi ya million katika mstari mmoja tu wa ushairi. Na ndo maana ktk yoyote ile utakutana na swali likikutaka ueleze nini dhima ya mwandishi ktk tungo husika, wakati mwingine ukitakiwa kuelezea mafanikio ya mtunzi ktk tungo husika.

HABARI za Elton John was not my concern, nimemwongelea Mrisho Mpoto ktk Sizonje. Na kutumia hiyo heading haina maana sijamwelewa bali kukusanya mawazo ya watu mbalimbali kabla ya kujeneralize.
OKWOKWO KILLS IKEMEFUNA!...THINGS FALL APART, IS IT POSSIBLE!, naijua vizuri fasihi ama literature zaidi hata ya the late chinua achebe na sakayonsa ama ngugi wa thion'go!,ama mzee mwanakijiji humu jukwaani! hoja hujibiwa kwa hoja! hakuna mahala nimesema kuwa fasihi ina maana moja, ktk poetry kama sizonje inaufanya ubongo ufikiri beyond! kung'amua dhima ya fanani kwa hadhira yake!
 
Back
Top Bottom