Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

kung'amua dhima ya fanani kwa hadhira yake!
Ulichong'amua wewe ni kipi?mbona unaishi kwa kukariri majina? hiyo haikuwa hoja yangu ni aliyeelewa Sizonje aweke alichokielewa kwa faida na manufaa kwa wengine.Kuishia kutaja majina km William Shakespeare, Socrates,Plato,Aristotle, Macbeth,Romeo & Juliet na Julius Caesar tunakuwa hatumtendei haki mtunzi wa Sizonje. Kama ulivosema hoja hujibiwa kwa hoja ungeweka hoja mezani, lakini kusema mwanakijiji ooh sijui nani unafeli siyo sawa na mbwembwe ulizokuja nazo.

Lete mezani ulichokielewa kuhusu Sizonje that is it.
 
Jamani nimekuwa nikipata wakati mgumu wa kujua maana hasa iliyofichika katika wimbo ulio imbwa na MRISHO MPoTo, ni ujumbe gani uliopo katika mashairi yake hasa anaposema

"...kuna picha mbili ya kwanza ni picha na ile picha ya pili ni mchoro wa picha ya kwanza......"

pia anposema...

"Nyumba ina milango lakini watu wanapita madirishani "

ila hasa huyo "SIZONJE" ni nani......

Ila hata kama kuna mstari ulio uelewa unaruhusiwa kutoa tafsiri yake kwa sababu najua wengi hatukuweza kuelewa ujumbe uliomo katika wimbo huu....

Kutoka enzi za mjomba hadi sizonje
 
mi mwenyewe sijauelewa na nimeshindwa kuuhusianisha na kinachoendelea Tanzania hivi sasa chini ya uongozi mpya.

nilocho penda tu ni huyo babu mpiga zomari yupo kihisia zaidi nimemkubali.
 
Sizonje... ni neno alilo libuni yeye mwenye na kuamua kulipa maana ya ...
Mkombozi... au nuru...
 
Aliutunga mwaka jana... yeye kama kawaida yake hasemi ukweli amemuimbia nani ila ni kama anamwambia Magufuli karibu kwenye nyumba yetu ambayo inamatatizo kibao...

Kama ana mjuliaha mapema...

Kuna vyoo hawavitumii wala hawatupi taka... (nchi inasomesha watu wengi lakini haiwatumii)

Usikilize tena vizur utauelewa zaidi..
 
Picha halisi ni nyerere na mchoro wa picha ni kikwete (tafsiri isiyo sahihi)
 
Picha halisi ni nyerere na mchoro wa picha ni kikwete (tafsiri isiyo rasmi)
 
if I were Mr presdaa, ningetuma vijana wangu wamkamate huyu kijana mguu kwa mguu mpaka mabwe ya pande aongee yooote aliyomaanisha.haiwezekani acheze na akili zetu eti "hata mimi sielewi nlichoandika".anatuvuruga sana huyu kijana sasa imetosha ,ebo...gademitih
 
Twende hivi..

Vyumba Vinne.. Ni awamu nne za marais waliopit.

•Vitatu havifunguki.. Ni awamu tatu, ya hayati Jk1, Mzee wa Ruksa, na Anko benja, hivi vilikuwa havisemeki sana, either kutokana na mazuri waliyofanya au kunyima Uhuru wa vyombo vya habari hivo mabaya yao yanafichwa na hayasemeki.

•K1 hakina mlango- ni awamu ya misho kabla ya sizonje, ni awamu ambayo ilikuwa na mapungufu mengi hivyo kuwaacha watu wajifanyie mambo bila sheria (kuingia bila hodi, kisa hakuna mlango)

Picha Mbili.. Viongozi wawili katika nchi yetu (hii ndio nyumba yetu)

Ya kwanza ni picha, huyu ndiye kiongozi mtimilifu kuliko wa kwanza, mwenye sifa nyingi kuliko wa kwanza... Huyu ni Jk1.

Ya pili ni mchoro wa picha ya kwanza... Huyu ni kiongozi ambaye ana sadifu sifa za kiongozi wa kwanza, hakumfikia wa kwanza (na ndio maana yy ni mchoro wa picha ya kwanza, siku zote mchoro hauwezi kuwa kama picha halisi kwa 100%) huyu ni Edward Moringe Sokoine.

Tutaendelea...
 
Pale kwenye bahasha

Anamaanisha vijana wamepewa elim inayotegemea kuajiriwa na sio kujiajil.

Ko wako bize na bahasha wakisaka ajira maana waliambiwa zipo . na nyumba waliambiwa ni yao

Waliambiwa nchi n yao na ajira ni zao, lkn huko ndan wamejaa kina kanjibah
 
Utunzi mahiri wa mashairi na ughani uliotukuka wa Mrisho Mpoto, umeligusa sikio la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameeleza kuwa shabiki mkubwa wa kazi za msanii huyo hususan wimbo wake ‘Sizonje’.

Akizungumza na Mpoto jana, muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli alimueleza msanii huyo kuwa anazifahamu vizuri kazi zake na kwamba anaupenda sana wimbo wake wa ‘Sizonje’ huku akichambua baadhi ya mistari iliyomo kwenye beti za wimbo huo.

Mpoto alikuwa msanii pekee aliyeongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Wakuu wote wa Wilaya za Dar es Saalam pamoja na viongozi wengine waliofika katika uwanja huo wa ndege kumpokea Mkuu huyo wa nchi.

“Nasikiliza nyimbo zako sana, ila huu wimbo wako wa Sizonje nimeuelewa sana na nausikiliza kila siku, kwangu umekuwa kama wimbo wa taifa, mwanzoni nilipata tabu kuuelewa lakini sasa hivi… aaaah, nimeuelewa vizuri sana. Halafu Sizonje namjua, nimtaje?,” yalisikika baadhi ya maneno ya Rais Magufuli kwa Mrisho Mpoto.

Akielezea tukio hilo lililoleta msisimko wa aina yake uwanjani hapo, Mpoto alisema kuwa baada ya kumsikia Rais ameanza kuusifia wimbo wake alishtuka na kujawa na furaha ya aina yake kwani kwa msanii ni jambo la thamani kubwa kusifiwa kazi yake na Mkuu wa Nchi.

Alisema kuwa pamoja na kuusifia wimbo huo, Rais alionesha kuufahamu vizuri zaidi baada ya kuanza kuipitia baadhi ya mistari na kuahidi kumfumbulia fumbo lililofichwa kwenye wimbo huo watakapokutana tena.

“Unapopata thamani kutoka kwa Mkuu wa Nchi inaleta faraja sana," amesema Mpoto. "Kwahiyo, mheshimiwa Rais leo kuniambia kwamba yeye ni shabiki wa kazi zangu na kwamba anapenda sana wimbo wa Sizonje, na akafunguka kwa mistari ‘minane’ ya Sizonje ikiwa ni pamoja na ile inayosema ‘huyu mgeni anayepitia madirishani wakati milango ipo!’ Na akaniambia siku tukikutana ataniambia vile vyumba vitatu kwanini havifunguki,” ameongeza.

Msanii huyo amemshukuru Rais Magufuli kwa kuthamini mchango wake katika sanaa kwakuwa anaamini kuthaminiwa ni hitaji kubwa la kila msanii.

“Kwakweli leo ni siku yenye furaha sana. Najisikia furaha sana. Asante sana mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. Umenifanya nimekuwa na siku nzuri sana,” Mpoto amefunguka kwa furaha.

Mwaka huu mwanzoni, Mrisho Mpoto aliachia audio na video ya ‘Sizonje’ aliomshirikisha Banana Zorro ambapo kwa muda mfupi tu, wimbo huo uligeuka kuwa mkubwa na kufanya vizuri. Kutokana na ufanisi wa kazi zake, Mpoto ameendelea kukubalika akipata mikataba ya ubalozi wa mashirika na taasisi kubwa nchini ikiwa ni pamoja na mfuko wa pensheni wa PSPF.

Mpoto ambaye mwaka jana alipewa tuzo ya heshima ya WASTA ya nchini Kenya kutokana na mchango wake katika lugha ya Kiswahili, amejipatia heshima kubwa kutokana na utunzi mahiri wa nyimbo za awali, zikiwemo Nikipata Nauli, Adela, Chocheeni Kuni, Samahani Wanangu, Waite, Njoo Uichukue na zingine.
 

Attachments

  • Rais John Magufuli akisalimiana na Mrisho Mpoto.jpg
    Rais John Magufuli akisalimiana na Mrisho Mpoto.jpg
    122.9 KB · Views: 144
Hata mimi nimefurahi maana wimbo wa Sizonje ni dira ya tulipotoka na kinachofuata.
 
Mpoto anastahili sifa. Ni anatumia akili katika kutunga nyimbo sio hawa waongeaji ambao ni wengi hata lugha za mafumbo hawajui
 
Msanii ktk usanii. Anatembea peku huku anavaa mavazi ya malaki na nyumba anaishi ya kisasa, angekuwa ana uchungu na utamaduni angeishi kwenye nyumba za kitamaduni hasa, msonge ulioezekwa makuti. Asijisumbue kutu manipulate kwa kutembea peku kujipatia funza bure, avae tu viatu.
 
Mpoto cheka cheka tu. Magufuli hachelewi kukuchenjia na kukuuliza risiti za mauzo ya CD aangalie kama umelipa kodi huyo.

Unafikiri anafurahi kuona umenenepa zaidi yake?
 
Mpoto cheka cheka tu. Magufuli hachelewi kuku henjia na kukuuliza risiti za mauzo ya CD aangalie kama umelipa kodi huyo.

Unafikiri anafurahi kuona umenenepa zaidi yake?
😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom