SIZONJE ndio jina la wimbo wake mpya Mrisho Mpoto alieyeshirikiana na Banana Zoro. Nimeusikiliza kwa makini lakini bado sijajua maana halisi ya huu wimbo.
Maana Ya "Sizonje", Wimbo-Shairi Kutoka kwa Mrisho Mpoto
Sizonje hii ndio nyumba yetu =Sizonje, hii ni Tanzania nchi yetu. Hapa, sizonje ni wewe mtanzania wa kawaida. Wewe sizonje uko nje. Umetengwa.Mrisho Mpoto anakuimbia wewe.
Milango ipo wanapita madirishani = Njia mwafaka zipo lakini [viongozi] wanapenda za mkato
Sizonje ndio nyumba yetu = Sizonje, hii ni Tanzania nchi yetu
Milango ipo wanapita madirishani = Njia mwafaka zipo lakini wanapenda za mkato
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu = Hayo ndio maajabu ya nchi yetu, fungua macho.
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu = Hayo ndio maajabu ya nchi yetu, fungua macho
Tulikaa barazani tukasikia kelele: Sisi kama watu wa kawaida, kupitia kwa vyo vya habari, tunasikia yanayofanyika serikalini.
Kelele toka ndani mtu anaruka dirishani: Ya kwamba baadhi ya watu wanapitia njia za mkato (corruption)
Sizonje karibu nyumbani kwetu: Sizonje, njoo na hebu tuicheke Tanzania yetu.
Uone maajabu ya nyumba yetu : Njoo uone jinsi tulivyokosa maadili.
Karibu sana Sizonje hii ndo nyumba yetu: Karibu Sizonje, hii ndio nchi yetu
Tulipoficha mundu za kupondea wezi: Tulipotupilia mbali uwezo wetu wa kupiga kura inavyostahiki
Kwani makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya: Mbona shida za zamani lazima ziwe za kila siku
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne: Nchi hii ya Tanzania ina vigao vinne.
Vitatu havifunguki: Vigao vitatu — legislature, executive and judiciary — ni vigumu kuingia (ndiposa [viongozi] wanapitia dirishani).
kimoja hakina mlango: hiki kigao cha nne ni kile cha wale wageni kutoka nchi za nje, wale watu kutoka ugenini wenye wana uwezo wa kuinfluence uongozi wa Tanzania.
Japo kuwa kina watu ndani na hawaongei Kiswahili: Hiki kikundi kina watu wasio watanzania halisi.
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea: Watanzania wameshawekwa kando na imekuwa kawaida sasa.
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni: Sizonje tulitoka huko kwa uchaguzi, kwa kupiga kura.
Huna haja ya kwenda kule kumejaa mafundi wa kupika: Hakuna haja ya kufikiria kura; zina waongo, watapeli wa kukudanganya na siasa.
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale: Sasa hivi wanapiga tu siasa hawa viongozi. Watakuhadaa tu.
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako: ukijashajanjaruka watajaribu kuuliza shida iko wapi.
Wanashangaa mbona ghafla: [Wanasiasa] Wanashangaa kwa nini huwezi kuwa watu wenye subira.
Samahani sana mgeni: ukiwakaza sana, wanakuwa watu wa kuomba msamaha wa uongo
Wapishi wameniomba kwamba: Halafu, kwa kejeli, wanasema Eti serikali kuu[wanasiasa wakuu] wetu wameomba ...
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba: Tuwaulize manataka nini, yaani wanjifanya hawajui matakwa ya wananchi.
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi: Haya ni maneno mazuri wanasiasa wanawaambia wananchi ili kuwahadaa wanyamaze.
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje: Wanaonyesha ya kwamba hao ni viongozi kamili watakaoshughulia matakwa yao.
Sizonje chumba hiki naomba usiingie: Sizonje, hii njia ya siasa za ungo usifwate.
Ukimaliza nitakwambia kwanini: Ukishadanganywa na wanasiasa ndiposa utajua.
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara: Hao hupiga siasa kila mara.
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa: Na katika siaza zao kuna Chama tawala na chama pinzani.
Moja picha nyingine mchoro wa picha wa kwanza: Nyama vyote na viongozi wa pande zote wanafanana tu kitabia.
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa ‘Usiyemtaka Kaja’: Ya kwamba Kuna uhuru wa kupiga kura na uchangua kiongozi umtakaye
Hatukuwahi kuelewa maana yake :Ila huu uhuru wa kupiga kura huenda haupo
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia :Labda ufikiri zaidi indio ujue maana ya siasa hizi bandia.
"Sizonje hii ndio nyumba yetu" =Sizonje, hii ni Tanzania nchi yetu
Milango ipo wanapita madirishani = Njia mwafaka zipo lakini wanapenda za mkato
Sizonje ndio nyumba yetu = Sizonje, hii ni Tanzania nchi yetu
Milango ipo wanapita madirishani = Njia mwafaka zipo lakini wanapenda za mkato
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu = Hayo ndio maajabu ya nchi yetu, Tanzania
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu = Hayo ndio maajabu ya nchi yetu, Tanzania
Najua wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto: najua nazungumza ukweli ambao wananchi, ambao wanadanganya kama watoto,hawatopenda kusikiza.
Na kamwe mtoto hawezi kuungua Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi: Wengi wanaamini kwamba mwananchi hawezi kuumia akiwa Tanzania (Nchi ndio mama hapa).
Njoo huku uone Sizonje: Lakini sasa fungua macho wewe.
Si unajua harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue: Lazima kuwe na mabadiliko, enyi watanzania.
Sawa Sizonje huu hapa ni ua, Lile pale ni shimo la taka Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi, Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka
Wala kwenda chooni = Hawa viongozi wamejenga vitu vya kifahari ambavyo hata hawavitumii.
Kama ukiwa makini Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu: Wananchi wanalalama.
Wengi ni vijana wana bahasha za khaki mikononi: Vijana wanaotafuta kazi.
Kama hamtupi taka shimo hili mlichimba la nini: Wanauliza mbona viongozi wanaharibu mali ya umma kwa vitu visvyofaa?
Lakini pia kwenye sauti zao Sizonje Kuna watoto wazee na kina mama: Hawa ni wananchi wa kawaida wakiwemo wamama na watoto, hata wazee na vijana.
Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele: Wote, kwa ujumla, wanalalamikia uongozi mbaya.
Ninavyosikia ila sina uhakika Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao: Waliambiwa Tanzania ni ya watanzania, lakini kumbe ni ya wachache.
Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki: na kwamba wana uhuru wa kufanya kile watakacho
Sasa njoo nikuonyeshe huku uchochoroni: Sasa tena kuna shida yningine ya ungozi
Uone maajabu mengine ya nyumba hii: wewe kama sizonje, mwananchi wa kawaida uliyetengwa, fungua macho.
Sizonje ukiona tembo anaringa :ukiwaona wanasiasa wanapiga siasa zao tena
Ujue mvua zinakaribia: ujue msimu wa uchaguzi mkuu umekaribia tena, na watafanya hivyo jinsi wanfanyavyo, waipitie dirishani, warudi bungeni.
"Sizonje hii ndio nyumba yetu" =Sizonje, hii ni Tanzania nchi yetu
Milango ipo wanapita madirishani = Njia mwafaka zipo lakini wanapenda za mkato
Sizonje ndio nyumba yetu = Sizonje, hii ni Tanzania nchi yetu
Milango ipo wanapita madirishani = Njia mwafaka zipo lakini wanapenda za mkato
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu = Hayo ndio maajabu ya nchi yetu, Tanzania
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu = Hayo ndio maajabu ya nchi yetu, Tanzania
Interpretation by Ezekiel Micah Mukhwana Mukwambo Sitati
Nairobi, Kenya.