Tafuta hela ikusaidie uzeeni

Tafuta hela ikusaidie uzeeni

Killa Cam

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2022
Posts
2,264
Reaction score
6,679
Tafuta hela iwe mlizi wako usitafute hela kwa kupata wanawake wazuri. Ukiwa na hela ina kupatia heshima kwenye familia na jamii. Ukiwa na hela ukiumwa inakuwa rahisi kwako kupata matibabu mazuri. Tafuta hela ikupe mke mwema sio mke mzuri, unaweza kuwa na mke mzuri wa sura na umbo lakini akawa hana tabia njema. Hela inasaidia kujua thamani ya maisha yako, ukiwa na hela huna hesabu ya muajiri wako atakupa mafao yako wakati wa kustaafu kwako. Bali unawekeza hela yako ilete hela nyengine(pesa inafanya kazi sio wewe unafanya kazi). Tafuta hela ili uwe na amani kwenye mizunguko yako, hujuwi nani utamkwaza kwenye mihangaiko yako. Masikini akionewa humuachia Mungu lakini tajiri mna pelekana mahakamani. Huna hela huwezi kuwa na mtetezi(mwanasheria), huwezi kumfanya polisi akawa upande wako. Ukiwa na Hela na Wadhifa serikali(cheo)heshima lazima ije wenyewe(utapewa). Ukipata cheo serikali watakuja watu hata huwajui na kukutukuza kwa nafasi iliopo tu, lakini siku ukija ondoka nao huwaoni. Cheo ni Sawa na hela anaweza tokea jamaa Mjomba/Shangazi au ndugu tokea udogoni hujawahi kumuona. Lakini sasa unazo anakwambia nae jamaa yako. Kama unatafuta hela ili uwachape, ikimaliza hio hela yako utachapiwa wewe, lakini ukitafuta hela ili kuleta mafanikio utayapata na utabakia nayo mwenyewe. Tumia nguvu zako zikunufaishe mwenyewe
 
Angalizo: wakati wa kutafuta hiyo hela, tunza sana afya yako, usije baadaye ukaingia gharama ya kutumia fedha zako hizohizo za akiba (na zaidi) kutibu afya uliyoijeruhi in the process.

By the way, hakuna akiba bora kabisa ya uzeeni kuliko kujenga na kudumisha afya bora itakayokuhakikishia uzee mwema. If you know, you know!

NB: AFYA means sound and healthy mind, soul and body.
 
Nashangaa 90% ya watanzania wanatafuta hela kwasababu ya wanawake pathetic generation.
 
Back
Top Bottom