Tahadhari: Adaiwa kutaka kujichinja baada ya kukamatwa ndani ya Kiwanda Bubu cha kutengeneza Pombe Feki Kigamboni

Tahadhari: Adaiwa kutaka kujichinja baada ya kukamatwa ndani ya Kiwanda Bubu cha kutengeneza Pombe Feki Kigamboni

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Inadaiwa kuwa huyu Jamaa alikua amepanga nyumba maeneo ya Kigamboni, barabara ya kuingia Baracuda Beach. Ndani ya nyumba alikua na kiwanda cha kutengeneza pombe feki aina ya K-vant, Konyagi, Henessy na brand nyingine. Inadaiwa alimuua mmoja wa wafanyakazi wake na akamtupa kisimani.

Sasa ile harufu ikawa inafika mpaka kwenye Petrol station ya jirani. Wahudumu wakatoa taarifa Polisi. Askari walipokuja jamaa akataka kulipua nyumba na kujiteketeza yeye pamoja na vyote vilivyopo. Aliposhindwa akaamua kujichinja shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali. Polisi wakavunja mlango na kuingia ndani ambapo walimchukua na kumuwahisha hospitali. Hata hivyo inadaiwa alifariki muda mfupi baadae.!


Pia Soma

- DOKEZO - Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk
 
One side of the story, wazungu hakuna Cha kuaminiana polisi lazima uvae body cameras ukiwa kazini
 
Mods unganisheni huu uzi na ule wa mshana jr
 
Back
Top Bottom