Tahadhari: Bei ya mafuta yapanda ghafla kataka soko la dunia baada ya uzalishaji kupungua

Tahadhari: Bei ya mafuta yapanda ghafla kataka soko la dunia baada ya uzalishaji kupungua

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Bei ya mafuta imepanda baada ya wauzaji kadhaa wakubwa wa mafuta duniani kutangaza kupunguza uzalishaji kwa ghafla.

MAFUTA.JPG

Bei ya mafuta yasiyosafishwa ya Brent ilipanda kwa zaidi ya $5 kwa pipa, au 7%, hadi zaidi ya $85 biashara ilipoanza.

Ongezeko hilo limekuja baada ya Saudi Arabia, Iraq na mataifa mengine ya Ghuba kusema siku ya Jumapili kuwa yanapunguza uzalishaji kwa zaidi ya mapipa milioni moja kwa siku.

Bei ya mafuta ilipanda wakati Urusi ilipovamia Ukraine, lakini sasa imerejea katika viwango vilivyoonekana kabla ya mzozo kuanza.

Hata hivyo, Marekani imekuwa ikitoa wito kwa wazalishaji kuongeza uzalishaji ili kupunguza bei ya nishati.

Bei ya juu ya nishati na mafuta mwaka jana ilisaidia kuongeza mfumuko wa bei - kiwango ambacho bei hupanda - kuweka shinikizo kwa fedha za kaya nyingi.

Akijibu taarifa za kupunguzwa kwa uzalishaji kwa hivi karibuni, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani alisema: "Hatufikirii kupunguza tunapendekeza kwa wakati huu kutokana na kutokuwa na uhakika wa soko - na tumeliweka hilo wazi." Kupungua kwa pato kunafanywa na wanachama wa wazalishaji wa mafuta wa Opec+.

Kundi hilo linachukua takriban 40% ya pato lote la mafuta ghafi duniani.

Saudi Arabia inapunguza uzalishaji kwa mapipa 500,000 kwa siku na Iraq kwa mapipa 211,000. UAE, Kuwait, Algeria na Oman pia zinapunguza.

Afisa wa wizara ya nishati ya Saudia alisema hatua hiyo ni "hatua ya tahadhari inayolenga kusaidia utulivu wa soko la mafuta", Shirika rasmi la Habari la Saudi lilisema.
 
Jambo la msingi la kufanya sisi kama nchi ni kuhakikisha GESI yetu aliyo tubariki Mungu kutoka msimbati kuwa tunaitumia kikamilifu kama matumizi mbadala.wa mafuta.

Lakini pia utafiti wa mafuta kwenye maeneo yaliyo bainika kama vile znz waongeze Kasi ya uchunguzi na hatimaye kuzalisha mafuta.yetu sisi wenyewe.

Tumeona Uganda iliwekeza kikamilifu katika utafiti na hatimaye sasa inaanza kuzalisha mafuta.
 
Jambo la msingi la kufanya sisi kama nchi ni kuhakikisha GESI yetu aliyo tubariki Mungu kutoka msimbati kuwa tunaitumia kikamilifu kama matumizi mbadala.wa mafuta...
Mafuta bado yana umuhimu wake sana, na twayahitaji sana
 
Njia pekee ya kuachana na huu utaahira ni kununua gari ya umeme tu.

Elon musk katuletea suluhisho la kudumu Duniani kuachana na wahuni wa opec kujisikia tu wanapunguza uzalishaji wanapiga hela.
 
Wacha nikuongezee na janga jingine !! Nchi haina dollar [emoji385] za kilipia mafuta kwa sasa !! Meli zote ziko on financial hold !! Mwingulu na Govenor wa BOT wanahaha!! Balaa zito!! NO FOREX !!! Balaaa !!
 
Back
Top Bottom