TAHADHARI: Benki Kuu, Kuna Uhalifu Kwa Wakopeshaji Mtandaoni

TAHADHARI: Benki Kuu, Kuna Uhalifu Kwa Wakopeshaji Mtandaoni

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Uryevyedi mdau Mtanganyika!.

Basi ndugu yangu ikiwa nchi imefunguka na pesa zimejaa kwenye mifuko na account za watu huko walipo hali ipo hivi.

Watu/Taasisi binafsi kwa sasa zinatafuta watu wa kuwakopesha kwa nguvu na hali kubwa sana, wanaunda App na kuilipia kama Ads kwenye mitandao ya kijamii ili kushawishi wananchi kukopo.

Binafsi sijawahi na kwa sasa sitarajii kukopa huko ila kinachoendelea ndicho tatizo na kero kubwa sana.

Inaonekana wengi wanaojisajili kwa nia ya kukopa (wenye akili na D2) wanaangalia kile tunaita Vigezo na Mashariti, baada ya hapo wanaandaa kila documents muhimu.

Hapo ndipo wanajaza namba fakes za simu za watu wasiofahamiana nao, anaweza kubuni namba za uongo ili mradi ameangalia majina yaliyopo kwenye namba husika.

Benki Kuu nyie kwa sababu ndiyo mnaotoa vibali kwa hawa wakopeshaji nikiwa muhathirika mmojawapo kwa kutumiwa sms na kupigiwa simu kwamba namba yangu iliandikwa kama mdhamini wa mkopaji haipaswi kuachwa lipite hivihivi.

Serikali kupitia kwa wasimamizi wa sekta ya mikopo wauteni hawa wakopeshaji muwape darasa, dunia ni kijiji kikubwa ambacho kila unachoanzisha kuna wanaobuni ulaghai haraka iwezekanavyo ili kuhadaa wengine.
 
Back
Top Bottom