SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 65
Kwanini mimi nikuoeneshe wewe mtu wa mtandaoni ushuhuda wa ninachofanya ikiwa hicho kitu nafanya kwa ajili yangu binafsi.Naomba nieleze ni vipi mtu anapoteza usd 200 ndani ya dk 20 , asante
Mimi sizungumzii $200 ya yule jamaa nazungumzia Forex kwa ujumla. Huyo aliyepoteza $200 ndani ya dakika 20 hujui ana capital gani na strategy zipi, huwezi sema amekosea. Huyo mtu hana tofauti na trader yeyote mwingine hapa Bongo maana wote wanajumlishwa kwenye ile "97% customers using this broker lost their capital, trade with caution"
 
Leo kuna mwingine ameibuka na P2P kwa wiki faida laki uwe na safal com laini na bongo voda com!
Sio wa leo huyo ni wa jana. Laini ya Safaricom ninayo ila siwezi risk 250,000 kununua kwa ninayejua alafu kuuza kwa ambaye sijui atatokea lini. Hiyo 250k nikiitoa nakwama ingekuwepo iddle ningejilipua
 
Sawa ,trader wa hapo Bongo unaowazungumzia umejuaje umahiri wao ,je umefanya utafiti kutoka kwa mabroker wote ambao unadhani hao wabongo wanatrade kwao na wakakupa majibu au unafanya guessing,

.Unadhani kila trader anataka kujionesha kupitia telegram au instagram au platform yoyote au kila trader ajitangaze kuwa amaefanikiwa kuwa profitable na akupe ushahidi, ili iwaje.

Kama imekushinda kwa binafsi yako unatafuta shughuli nyingine kimya kimya,,si kila mtu atakuwa trader na si kila mtua atakuwa mkulima nk
 
Forex ni legal ila haitambuliwi na mamlaka za Tz. Ila sasa kuna illegal business zinafanyika, hawatangazi maana watakamatwa ila wanapata hela na wanajulikana. Nani hajui kwamba madawa ya kulevya na ujangili vina hela, mbona wanaojihusisha wanahisiwa na kutajwa, na hela hizo unaziona. Kwani wao hujitangaza

Sasa kwanini wanaofanikiwa Fx wasijulikane kisa wanakuwa wenyewe na market. Hawa kina Sirjef wanaotukana watu na kushinda wanataja mafanikio hewa wangekuwa na hela ndio wajifiche kisa walikuwa wenyewe na PC. Nakataa

Waliofanikiwa kimataifa ni wale established, ambao kuwaiga ni vigumu mno. Ni kama HIV inaambukizwa kwa ngono ila scientifically kuna watu hawaambukizwi HIV sasa hatuwezi tumia hao in generalization kudai HIV haitoambukizwa.

Nani unaweza mshawishi atumie dawa ambayo 97% ya watumiaji hufa, asome kozi ambayo 97% wanaosoma hufeli, anunie gari ambalo uwezekano wa kulitumia ni 3%?
Sasa how comes nimshawishi mtu awekeze ambako 97% wanaowekeza hufeli
 
Mbona Kama uko arrogant na ego inakutawala mkuu.
Unajipamabanua Sana hata sijui umefanya Nini dunia tukufahamu. Sasa kusomea Latvia umevumbua Nini ama kisa kuruka na ndege na kula nyeupe huko club unajiona Kama unatembea hewani haukanyagi ardhini Kama sie mkuu.

Kwani mchaga umefanya invention gani basi ndugu. Yaani uko na ego Ile mbaya unajiona uko smart Sana kuliko binadamu wote.
Una ukwasi gani ndugu.
Uko Forbes ama uko jf?
Nina Imani hauna hata kitu kinaitwa Dola Billioni ili angalau uweke kwenye list ya matajiri.
Mbona dangote akatulia mkuu.
Yaani debe huvuma Sana ili lisikike Ila lililojaa limetulia.
NB mie Sina hela,Mana utaanza kuwa mie Nina hela gani.

Ila am sure you don't own $bilioni even a half.
Watanzania Wana nguvu za kuwekeza kwa juice Ila sio kwa gesi. In prof Muhongo voice.
Una hela unafanya Nini huku mkuu.
Remember money can't lenghten your tongue, so be humble kijana Kama umezipata unajiona kuwa unaweza kumtawala kila mtu Kama mkeo ama mwanao sio ivyo.
Usiwe limbukeni wa kushika hela.remember gives you freedom and make you rich.

Haya boss hata huwa unadhamini Nini hapo kijijini kwenu
 
Margin call alert

Margin level of your account 10000 has fallen below the minimum maintenance requirement of 80%. Kindly take urgent actions to avoid stop out. TemplerFX

Ukiona hio sms ujue mambo sio mambo mjomba
Overtrade akazidisha lot size pia hajaweka sl
 

Mkuu kubeti nayo ni taaluma aisee usitusilibe wazee wa mikeka.

Mikeka yenyewe uzuri wake kujifunza ni mwaka mmoja tu unatosha, na ni kamari ya wazi tofauti na forex. Forex nayo ni kamari mkuu, ila yenyewe haiko wazi.
 
Mat@ko yako tena na tena.
Haya ndiyo hayo uliyojifunza huko kwa wenzko? Ama ndo kwenu mnafundishwa ivyo mkuu.
Ila unaonekana kweli umesoma na pia wazazi wamekulea kwenye maadili mazuri. Wanastahili kupewa Nobel as good parents waliolea kijana wao akawa na maadili na lugha nzuri kwa wenzake.

Binafsi Nina Imani hujafanya invention yoyote new hata Kama ni matusi unatukana uliyokariri.

Nina Imani hauna tusi jipya.
Kama hili nilishasikia kabla na zaidi ya Mara alfu alfu bilioni.
So kuja na id ya nchi ya wanaume wengine Tena inawakilisha nchi Yao so utaonekana Kama keki fulani ama.
Ila akili za blacks kafanyiwa Brainwashed Sana mpaka huruma.
Majina ya kwao ya asili hayataki
 
Yap, tengeneza STRATEGIES ZAKO mwenyewe...karibu binary
 
Mbali na kushiriki mimi naamini mada zinazotolewa si za kupuuza kwani ukizisoma utapata lolote la kukusaidia ndugu yangu hatushiriki ili kushinda tu bali hata kuelimishana.
Target ya maskini ni kuvuna papo hapo, wenzetu wanawekeza kwa 5 good years ndipo anaanza kula matunda.

Forex nimeanza 2017, nimepoteza sana but now ni gwiji wa fx na binary natumia uzoefu utokanao na fx.
Elimu
Elimu
Elimu
 
Target ya maskini ni kuvuna papo hapo, wenzetu wanawekeza kwa 5 good years ndipo anaanza kula matunda.

Forex nimeanza 2017, nimepoteza sana but now ni gwiji wa fx na binary natumia uzoefu utokanao na fx.
Elimu
Elimu
Elimu
Hongera kwa kuwa gwiji ila huenda ikawa ni maneno tu na kwa sababu ni siri yako hongera.
 
Forex will never make you rich. Go find a job. Toka hapo kwa shemeji yako acha dada yako akazwe kwa uhuru.

Find a job dude. Huu ndio ukweli mchungu kwako na washamba wenzako.

Tena wewe utakuwa umesoma education maana mnakuwaga wajinga sana.

Find a job man. Forex Is scam.
 
Napata hasira sana nikiona vijana mnatapeliwa kirahisi namna hii.
Fuga hata bata achana na mambo ya forex.

We endelea kulipia bills za wanaume wenzako huko Bahamas.
 
Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia kubwaa mkamaria mwenzangu....hata mimi kati ya kuBet na Foreksi nilichagua,nachagua na NitachG
Aua kubet maishaaa FX amna pesa nshawai kujaribu kusoma na mavideo ya course za udemy ninazo ila roho ikakataa kabsaa mwaisa roho inasema "kama unataka kuona dunia chungu anza kutrade Foreksi" kuna mdau kasema hapo juu kubet ukiweka pesa ikaenda ndo imeenda....hapana haiko ivo ckuiz tumia System bet mfano ukiweka mechi 3 ikalost 1 unarudishiwa stake yako kiasi ila uko kwenye kudownload mapesa hapana aisee
 
Kubet nako kuna changamoto, ni wachache sana wanaowin kwenye mikeka yao asilimia kubwa ni losers kwa hiyo sio rahisi betting kuwa kitega uchumi cha mtu fulani na hata anaye weka mkeka hana uhakika wa ku win mkeka huo. Asilimia kubwa ya wanaobashiri hawana furaha wanakuwa na stress hasa wale wa live betting.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…