SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 65
Sijapata mtu anayeleta hoja zake zenye mashiko kuelezea jinsi watu wanavyonufaika na hizi biashara hasa fx, kutokana na majadiliano yanayoendelea nabaini kwamba kuna baadhi wanafanya vizuri ila hawako wazi kuthibitisha hatua nzuri waliyoifikia kuelekea mafanikio na hivyo mimi naona hizi biashara zina makandokando mengi kwa wanaozifanya.
 
Naupenda usemi huu wa kimombo 'If you do not know where you are going any road will take you there'
Neno zuri jingine ni hili :'Any decision you make in life, you are responsible for it' (uamuzi wowote utakaoufanya maishani mwako utawajibika mwenyewe)
 
Nilibahatika kupata elimu ya ujasiriamali zaidi ya miaka 30 iliyopita, kwasasa namalizia kuandika kitabu cha ujasiriamali,nimekiandika kwa kimombo kama kitabu mama, vingine vitafuata kwaajili ya kulisha aina tofauti za uelewa , naendesha maisha yangu kupitia ujasiriamali kimesheheni vitu vingi pamoja na njia ya kugundua mwenendo wa sera,siasa na yanayomzungua mfanya biashara vinavyoweza kuathiri biashara kwa kutumia IPYANA analysis niliyoibuni mimi 'IPYANA Analysis by Ipyana Benny Haraba 'IPYANA analysis, that will help to detect internal and external critical determinants of uncertainty in business or in an organization
 
Nilibahatika kupata elimu ya ujasiriamali zaidi ya mia 30 iliyopita, kwasasa namalizia kuandika kitabu cha ujasiriamali,nimekiandika kwa kimombo kama kitabu mama vingine vitafuata kwaajili ya kulisha aina tofauti za uelewa , naendesha maisha yangu kupitia ujasiriamali kimesheni vitu vingi pamoja na njia ya kugundua mwnendo wa sera,siasa na yanayomzungua mfanya biashara vinavyoweza kuathiri biashara kwa kutumia IPYANA analysis niliyoibuni mimi 'IPYANA Analysis by Ipyana Benny Haraba 'IPYANA analysis that will help to detect internal and external critical determinants of uncertainty in business
Una mawazo chanya sana, na mimi nitakitafuta kitabu chako lakin vya fx havijawa na tija kwangu.
 
forex inabidi ujifunze sana na uwe na nidhamu ya kumanage hasara
Na hicho kitu ndio kigumu, mtu anaweza kujitahidi lakini mwishowe atakuta tayari kachoma akaunti yake kuwa na hiyo nidhamu ndio ngumu kabisa.
 
Tatizo ni nguvu ya ushawishi, kiufupi mtu anavyoanza biashara ya fx anaweza kwanza kujitathimini kwa demo akaunti, demo a kaunti ni indicator nzuri kwa mru anayeanza biashara hiyo, tatizo mfumo ulivyo wa fx unakutamanisha kuwa na zaidi na zaidi, na hapo trader atatamani kuweka lot size kubwa ili avune parefu na kadri anavyozidi kutamani ndio anazidi kukaribia kuunguza akaunti yake, na hapo ndio ugumu unapoanzia wa yeye kunufaika na biashara hiyo.
 
Aisee hii ni kweli kabisa,watu wengi hususan vijana wanapenda mafanikio ya haraka.Juzi tu nimetoka kujifunza somo la maisha kwamba utajiri hauji kirahisi kama wengi wetu tunavyodhani.
 
Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia kubwaa mkamaria mwenzangu....hata mimi kati ya kuBet na Foreksi nilichagua,nachagua na NitachG
Aua kubet maishaaa FX amna pesa nshawai kujaribu kusoma na mavideo ya course za udemy ninazo ila roho ikakataa kabsaa mwaisa roho inasema "kama unataka kuona dunia chungu anza kutrade Foreksi" kuna mdau kasema hapo juu kubet ukiweka pesa ikaenda ndo imeenda....hapana haiko ivo ckuiz tumia System bet mfano ukiweka mechi 3 ikalost 1 unarudishiwa stake yako kiasi ila uko kwenye kudownload mapesa hapana aisee
Kampuni gani mkuu unatumia?
 
Hata kama ikitokea ukaupata utajiri kiurahisi kuna uwezekano mkubwa ukapotea kiurahisi kwa sababu ya haujauwekea msingi mzuri wa kusimamia huo utajiri wako, mafanikio mazuri ni yale ambayo umeyatengenezea njia au Channel ya kusapot utajiri wako, ukiona bahari, ziwa halikauki maji ni kwa sababu kuna vyanzo vikubwa na vidogo vinavyo ingiza maji ndani yake wakati wote, lakini vyanzo vyote vikikauka hapo inaweza kupelekea kupungua kwa kina cha maji ndani ya ziwa hilo na wakati mwingine hata kupelekea kukauka. Mfano mzuri kuna jamaa huku kwetu yeye alikuwa hana chochote, na mimi nimekuja kumfahamu baada ya yeye kufanikiwa kupitia kubashiri sio mimi tu niliyemfahamu bali watu wengi walimfahamu kwani hakufanikiwa kidogo bali alifanikiwa zaidi na tena kwa mara moja, yeye huyo alibashiri Jackpot ya MBET "Perfect" mechi 12 na zote alizipatia akawa mshindi wa milioni mia mbili themanini na ushee (TSH280, 000,000/=) na ilikuwa mwaka 2018. Baada ya ushindi huo kwanza alifahamika na wilaya nzima pamoja na uongozi wake, jina lake lilizubgumzwa mara kwa mara midomoni mwa watu, Pamoja na hayo yeye mwenyewe alianza kutafuta vitu ambavyo siku zote alitamani awe navyo alianza kununua nyumba mbalimbali kwa bei kubwa yaani nyumba ya kawaida yeye anainunua kwa milioni 60,70,80,nk akanunua gari la kutembelea la zaidi ya TSH MILIONI 30, akafungua Hardware yake, akanza kusoma chuo na bahati mbaya alikuwa akitoka mkoa mmoja kwenda mwingine kusoma na hiyo ni kwa sababu alikuwa na usafiri wake, akaanza kujishughulisha na shughuli za vyama vya kisiasa na huko nako alikuwa hajulikani ila akaanza kuheshimika ndani ya chama kiufupi alifanya mambo makubwa na kwa kawaida mtu angesema tayari huyu yupo level nyingine kabisa, pamoja na hayo yote mpaka sasa ameshauza nyumba alizozinua kwa bei kubwa na yeye huuza kwa bei ndogo, hardware yake imeshafungwa, na kwa mara ya mwisho gari lake nalo lilikuwa halitembei tena na sijui kama anaendelea na masomo tena, simanishi kwamba tayari ameshamaliza pesa zake hizo ila nakuonesha jinsi pesa zisizo na msingi mzuri zinavyopotea. Hivyo utajiri unaokuja kwa haraka unapotea pia kwa haraka, ni vema mtu akaweka msingi mzuri ili akishaupata huo utajiri basi upate sehemu imara ya kusimamia.
 
kuna jamaa wangu wa karibu aliniomba sh. 5000 ya kula
aisee nilistuka, imekuaje, kaibiwa kila kitu au

baadae sana ndiyo nikapata ukweli, alishiriki hii kitu, foreksi
Watu wanaoifanya hiyo biashara ni rahisi kuwasikia wakiipamba mara utawasikia wakisema aliyeteketeza hizo fedha alikurupuka, hakuwa na elimu sahihi ya trading, mara hakuelekezwa, wengine hakujidhatiti kwenye biashara hiyo ila ukweli wahanga ni wengi wameshalizwa na wanaendelea kulizwa, kinachowatesa wengi ni msisimko wa biashara zinazoonekana kuwa na utajiri wa haraka hizo huwaliza wengi.
 
Biashara ni ile ya kubadilishana huduma au bidhaa kwa fedha au kukopesha fedha au bidhaa kwa bidhaa.

Biashara ambayo ni ya pesa tu, tunaweka pesa na ili mm nipate lazima wewe upoteze haiitwi biashara.
 
Back
Top Bottom