SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 65
Biashara nyingizi zinakufa kutokana na kutojikubali ulivyo unataka uwe kama fulani 'status quo'
 
Vipi kuhusu frelancer? Ukinijibu hili nakupigia kura
Frelancer ni nzuri, kwa sababu wao wanatangaza kazi fulani na wewe ukiona hiyo kazi unaimudu ndio unaiomba ukikidhi vigezo mnafanya na mhusika makubaliano changamoto yake inabakia kwenye uaminifu wa namna ya kutekeleza makubaliano yenu. Na huo mfumo pia upo katika GURU. Kwa maelezo hayo mafupi utakuwa umepata kitu japo si sana. Asante.
 
Malengo gani we famba? Hamna kitu hapo.
Taja mtu mmoja tu anaefaidika na forex hapa TZ.

Mtabaki kujituliza na maneno ya busara na faraja but ndani ya mioyo yenu mna maumivu makali sana.
Poleni sana kwa kulisha kuku choma wazungu kwa hela zenu mnazozitafuta kwa jasho na damu.

forex will never make you rich, never ever. Utapoteza na kupoteza daily.

Em niambie ni kina nani hao wanaonunua hizo hela mtandaoni?

Kumbuka hela ya mtandaoni ni just digital money haiitaji kuwa converted to any local currency et ndio ufanye manunuzi.

Shtuka mtaalam unapigwa.
 
hakuna mtu aliyemshawishi mtu mzee baba, sasa mtu akushawishi ufanye forex ili iweje faida ukipata ni wewe hasara ukipata ni yako mimi sio wakala wa forex kwamba nikishawishi watu wajiunge nalipwa hapana tunapeana maarifa tu ambayo waliyoyakosa wanaita utapeli.

Hapa tunajaribu kuwekana sawa kimawazo tu sehemu ambazo hazijaeleweka kuhusu forex, hii sio biashara ya kujipatia pesa za ubwerere ni biashara ya wale waliodhamiria tu kuifanya iwe wanaliwa pesa au vipi as long as wanajua baada ya kuliwa pesa ni uzoefu baada ya uzoefu ni kurudisha hela uliyoliwa baada ya hapo ndio mafanikio utayaona, it take years, its not an overnight process
 
Mkuu kubeti nayo ni taaluma aisee usitusilibe wazee wa mikeka.

Mikeka yenyewe uzuri wake kujifunza ni mwaka mmoja tu unatosha, na ni kamari ya wazi tofauti na forex. Forex nayo ni kamari mkuu, ila yenyewe haiko wazi.
Tofauti ya Forex na kubet ni hii hapa;

Betting ni gambling ambayo unaweka pesa halafu unabashiri win or loss, ukipata unakula hela ukikosa unaliwa,
Forex ni financial market speculation kutokana na kupanda na kushuka kwa demand ya currency fulani against currency nyingine ambapo unanunua/kuuza currency fulani kutokana na speculation yako kama sokoni inapanda/inashuka.

Kununua na kuuza kunaifanya Forex kuwa trade na sio gamble, ila Betting ni tofauti hakuna bidhaa unayonunua halafu ukauza, ndio maana katika forex professional traders wanasisitiza technical analysis kufanya trade zako kitaalamu, nje na hapo ndio inakuwa saw a na kufanya gambling.
 
braza inaelekea ushalizwa ndio maana umepanic, ila kwa hizo sentensi bolded hapo juu zimeonyesha uelewa wako wa forex ni wa mashaka
 
braza inaelekea ushalizwa ndio maana umepanic, ila kwa hizo sentensi bolded hapo juu zimeonyesha uelewa wako wa forex ni wa mashaka
kwanza Hujitambui, af sjaiii shkiwa akili na mnambe kama wewe nijiunge na huo upuuzi.

Njoo maeneo ya Kivukoni light house leo 1:30 PM tuonane and see kama nipo hivyo unavyowaza. Watu nitakao kuwa nao are from the highest place In the government so make sure unavaa smart tukapate na lunch.

Tuma namba yako PM. I'm very serious.
 
sio kwa mwandiko huo
 
Kuwa profitable trader inahitaji muda sasa nyie mnafanya forex kama kubet au tatu mzuka lazima mle za uso
 
Hizi kauli hutolewa milele na milele, kila mtu akifeli Forex hupewa sababu nyingi sana. Huwezi nionesha mtu aliyefanikiwa kwa Forex Tanzania hii, ina maana wote ni vilaza
Kufanikiwaje? Coz kama mtu anaendesha maisha yake kwa forex dola 20,30 kwa siku hakosi si ndo mafanikio ayo. Au unataka wenye mijumba na magari makali ndo useme mafanikio??
 
Tatizo mnaingia kwa kuambiwa zinaela, hamtaki kukaa na wenye maarifa. Biashara ya mtandao nimeianza tokea 2017 , lakini nimekuja kuziona hela 2021. - kutokana niliingia bila ya kuwa na mtu mwenye kunielimisha. Na wanaojua hawataki ujue kutoka waliji- sacrifice mpaka wakayaona mafanikio. Na usije kujaribu kuingia kwenye biashara ya mtandao bila maarifa YA KWELI , kutokana utafeli kimaisha, utapoteza muda na hela yako
 
Mwenye maarifa ni nani, yuko wapi, anapatikana wapi, maana kila anayetrade ni mtaalamu zaidi ya yote atakurundikia vitabu, video hapo ndo anakufundisha, hata hivyo mafanikio yenyewe ni kusimuliana tu uhalisia hauonekani.
 
Mwenye maarifa ni nani, yuko wapi, anapatikana wapi, maana kila anayetrade ni mtaalamu zaidi ya yote atakurundikia vitabu, video hapo ndo anakufundisha, hata hivyo mafanikio yenyewe ni kusimuliana tu uhalisia hauonekani.
Hey, sio kila biashara iliyopo ni ya kufanya, vivyo hivyo online sio kila idea unayoambiwa inafanya kazi. Na ukiona Biashara inatangazwa uifanye hiyo haina hela, wenye siri tupo wachache
 
Hey, sio kila biashara iliyopo ni ya kufanya, vivyo hivyo online sio kila idea unayoambiwa inafanya kazi. Na ukiona Biashara inatangazwa uifanye hiyo haina hela, wenye siri tupo wachache
Ukweli unabaki palepale kwamba wanaofanikiwa kupitia biashara hizi za mtandao kama fx ni wachache sana ukilinganisha na wanaopata hasara, wengi wanateketeza fedha zao kwa namna wanavyoshawishika na kuingia kufanya biashara hiyo lakini pia wengi wamepotezewa malengo yao. Cha msingi watu wachukue tahadhari biashara za mtandaoni si za kukurupukia.
 
Biashara hizi zina matapeli wengi kuanzia anayekushawishi tapeli, anayekufundisha kuifanya tapeli, anayekuelekeza naye tapeli, mwenye biashara hiyo naye tapeli, wewe mwenyewe ukianza tu kuifanya unakuwa tapeli.
 
Biashara hizi zina matapeli wengi kuanzia anayekushawishi tapeli, anayekufundisha kuifanya tapeli, anayekuelekeza naye tapeli, mwenye biashara hiyo naye tapeli, wewe mwenyewe ukianza tu kuifanya unakuwa tapeli.
Kwa upande wangu mimi sijihusishi na forex, bitcoin wala mitandao kama Q-net. Mtaji nao tumia 20000 na faida ni Laki 1 ndani ya siku tatu. Inahitaji ujue JAVA , HTML na CSS. Kwenye Coding ndo wengi hufeli
 
Kwa upande wangu mimi sijihusishi na forex, bitcoin wala mitandao kama Q-net. Mtaji nao tumia 20000 na faida ni Laki 1 ndani ya siku tatu. Inahitaji ujue JAVA , HTML na CSS. Kwenye Coding ndo wengi hufeli
Tuelekeze jinsi unavyofanya ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…