SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 65
Sikia ishu Iko Ivi wengi wanakimbilia kufundisha,kuuza kozi,kuuza signals,kuwakamata newbies,
Kufanya akaunti management Ila kiukweli hao wamechezea za uso mkuu.

Hii ishu ni legitimate Ila ni ngumu.
Is not easy but it's simple.
Sijafanikiwa so Sina shuhuda.
Ila ni ngumu mkuu sio suala la kitoto mpaka kufikia kileleni
Kabisa kiongozi hapo nakuunga mkono, labda hatujafahamu kilichopo nyuma ya mfumo, kwa mfano nina rafiki yangu yeye alikuwa anafanya biashara hii kupitia binary kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa na USD 1200 kwenye account yake baada ya wiki mbili ilipanda hadi USD3400 nilitamani sana anielekeze, kweli alijitahidi kunitafutia vitabu pamoja na audio za training ambazo na yeye aliniaminisha ndizo zimemsaidia, nami nilianza kufanya biashara hiyo kupitia demo akaunti wiki iliyofuata nilienda kwake kufuatilia alupofikia nikiamini angalau kwa speed aliyokuwa nayo ningemkuta na USD zaidi ya 5000 lakini nilikuta tayari ameunguza akaunti yake na hapo ndipo nilianza kuiona biashara hiyo kama sehemu ya kupoteza fedha zako. Hivyo ni kweli kabisa wengi wanachezea za uso.
 
Forex ni biashara kama biashara nyingine ila inahitaji maarifa nidhamu na uzoefu ili kufanikiwa.

Ukiingia kichwa kichwa lazima ulie, ila kama una malengo ya muda mrefu hasara na faida njiani zitakupa uzoefu, utakaokuwezesha.

Kibongo bongo ni wachache sana wanaofundisha uhalisia wa hii biashara wengi wanakusanya watu kwa ushawishi wa utajiri wa chap, wanawalia ada zao ila wanapoenda kujaribu kutrade wanachoma akaunti.
Waliofanikiwa kwenye hii biashara hawana muda wakutafuta watu wawafundishe wako busy kuingiza hela.

Wale wenzangu na mimi ujue wanatafuta mtaji tu kwa kutumia maarifa waliyonayo bila uzoefu na nidhamu.
 
Inawezekana ukawa sahihi lakini kujifunza biashara mpya wewe mwenyewe ni ngumu na inawezekana kati ya watu 100 wakatokea watu watatu wenye uwezo huo, shida sio elimu ya biashara watu wametumia hizi biashara kama njia mkato ya kufikia kilele cha mafanikio, na wengi wao wakishasimuliana hutumbukia moja kwa moja na hao ndio wengi tuliao ila wanaofanikiwa ni wachache tena shuhuda zao hazipo wazi, labda wewe kama ulishafanikiwa weka ushuhuda wako tukujue kwamba haupo level yetu.
Pia unahitaji uwe umejitoa kiukweli kweli sio suala la kitoto. Ile una plan B kuwa nikifeli nitafanya ivi. Kubali uwe masikini Mana ulikuwa unapigania ndoto yako na haikutiki.
Hii ni career Kama career zingine. Sio unamuona surgeon anamchana mtu kichwa unaona ni easy unaamua kuchukua weekend kozi,ama kusoma kitabu Kama wiki ivi afu na wewe unataka kujipima kupasua mtu kichwa.

You've to dedicate much of your time. It's more than a job. I can call it Vocation ndugu.

Burn all bridges no point of return.

Kuna captain mmoja alichukua jeshi lake wakatumia boti wakavuka kwenda vitani,Ile wamefika ng'ambo Ile akazichoma moto.jeshi lake lilikuwa dogo compared na la adui zake.
So akawaambia mnaona huo Moshi Ina Mana hapa hakuna kurudi Kama tukishindwa.
We've one option survive or perish.
Unaambiwa jamaa walipigana kufa kupona mpaka wakashinda wakarudi home kwa boti za maadui.

Binafsi Nina amini kuwa binadamu tuna uwezo mkubwa mno kuliko tunavyowaza wa kufanya endless or unimaginable things.

Sema ishu we don't stick or dedicate the whole energy in one thing and only one thing jamani.

Some people are proud to be multi-purpose or kumaliza job nyingi kwa wakati mmoja.
Ila wasichojua ni kuwa wanamaliza partially tofauti na aliyejikita kwa eneo moja pekee.

Pia unapokuwa una plan B hiyo B inachukua energy za plan A mkuu.

Ukifanya A if you encounter any difficulty unaiwaza B kumbe ungepata solution ya A.

Ukifanya kazi Kama umeshikiwa bunduki nyuma Nina Imani unafanikisha usichokiweza mkuu.

Ni hayo tu mpaka nimechoka.
Ila it aspiration mind or soul
 
Kabisa kiongozi hapo nakuunga mkono, labda hatujafahamu kilichopo nyuma ya mfumo, kwa mfano nina rafiki yangu yeye alikuwa anafanya biashara hii kupitia binary kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa na USD 1200 kwenye account yake baada ya wiki mbili ilipanda hadi USD3400 nilitamani sana anielekeze, kweli alijitahidi kunitafutia vitabu pamoja na audio za training ambazo na yeye aliniaminisha ndizo zimemsaidia, nami nilianza kufanya biashara hiyo kupitia demo akaunti wiki iliyofuata nilienda kwake kufuatilia alupofikia nikiamini angalau kwa speed aliyokuwa nayo ningemkuta na USD zaidi ya 5000 lakini nilikuta tayari ameunguza akaunti yake na hapo ndipo nilianza kuiona biashara hiyo kama sehemu ya kupoteza fedha zako. Hivyo ni kweli kabisa wengi wanachezea za uso.
Hapo aliingiwa na overconfidence , dopamine ikajaa mwilini afu euphoria ikachukua nafasi yake.
Ukielewa hapa utakuwa umekaribia
 
Forex ni biashara kama biashara nyingine ila inahitaji maarifa nidhamu na uzoefu ili kufanikiwa.

Ukiingia kichwa kichwa lazima ulie, ila kama una malengo ya muda mrefu hasara na faida njiani zitakupa uzoefu, utakaokuwezesha.

Kibongo bongo ni wachache sana wanaofundisha uhalisia wa hii biashara wengi wanakusanya watu kwa ushawishi wa utajiri wa chap, wanawalia ada zao ila wanapoenda kujaribu kutrade wanachoma akaunti.
Waliofanikiwa kwenye hii biashara hawana muda wakutafuta watu wawafundishe wako busy kuingiza hela.

Wale wenzangu na mimi ujue wanatafuta mtaji tu kwa kutumia maarifa waliyonayo bila uzoefu na nidhamu.
Fungakazi nimekuelewa, kwenye hii biashara waliofanikiwa hawana muda wa kuwaelekeza wasiojua ila wasiojua ndio wako busy kuwaelekeza wenzao wasiojua kinachofuata ni kuunguza akaunti na wengi ndio hao wasio jua[emoji122][emoji122]
 
Hapo aliingiwa na overconfidence , dopamine ikajaa mwilini afu euphoria ikachukua nafasi yake.
Ukielewa hapa utakuwa umekaribia
[emoji3][emoji3][emoji3] Hapa unaonesha unwamba wako kwenye field ya FX ila sasa sijui kama unaziishi hizo terms [emoji2][emoji2]
 
Forex ni biashara kama biashara nyingine ila inahitaji maarifa nidhamu na uzoefu ili kufanikiwa.

Ukiingia kichwa kichwa lazima ulie, ila kama una malengo ya muda mrefu hasara na faida njiani zitakupa uzoefu, utakaokuwezesha.

Kibongo bongo ni wachache sana wanaofundisha uhalisia wa hii biashara wengi wanakusanya watu kwa ushawishi wa utajiri wa chap, wanawalia ada zao ila wanapoenda kujaribu kutrade wanachoma akaunti.
Waliofanikiwa kwenye hii biashara hawana muda wakutafuta watu wawafundishe wako busy kuingiza hela.

Wale wenzangu na mimi ujue wanatafuta mtaji tu kwa kutumia maarifa waliyonayo bila uzoefu na nidhamu.
Mkuu Kuna Vita nimepigana mpaka naona ni sawa watu wafeli kweli.
Yaani sio kawaida Kama unavyowaza. Napigana akaunti ikisoma £10M+ nitawapa vijana motto wa kutosha pia na withdraw kadhaa.

Huwa nawacheki watu wanavyoiponda nanyamaza.

Ishu hii ni ngumu hata msuli wa MD ukasome ni naseri kwa hii mambo.

Kiukweli a real trader kwanza hawezi onyesha trades zake hata siku moja huyo bado hajaiva.
Sema ataweza kukuonyesha anavyo trade basi Mana hakulazimishi umuamini.

Yaani mie mtu akiongea najua huyu ni trader ama educator or journalists unawajua.
Mpaka vitabu vyao unavijua.

Vitabu vya trading unajaza semi Ila vya ukweli unabeba mkononi vya real traders achana na vya hao waliokata tamaa
 
Fungakazi nimekuelewa, kwenye hii biashara waliofanikiwa hawana muda wa kuwaelekeza wasiojua ila wasiojua ndio wako busy kuwaelekeza wenzao wasiojua kinachofuata ni kuunguza akaunti na wengi ndio hao wasio jua[emoji122][emoji122]
Sawia kabisa,

Wanaotoa kozi wenyewe bado hawajayaona mafanikio, ndo wanatafuta wasio na uelewa wa hii biashara wanawashawishi wanapiga pesa wajazie akaunti zao wapate dola za kufanyia majaribio kitu ambacho hawajakimudu.

Forex inahitaji muda na kujitoa unless mtu amefanikiwa kumake 4 to 6 figure consistently usikubali akufundishe bora ujifunze youtube bure.
 
Mkuu Kuna Vita nimepigana mpaka naona ni sawa watu wafeli kweli.
Yaani sio kawaida Kama unavyowaza. Napigana akaunti ikisoma £10M+ nitawapa vijana motto wa kutosha pia na withdraw kadhaa.

Huwa nawacheki watu wanavyoiponda nanyamaza.

Ishu hii ni ngumu hata msuli wa MD ukasome ni naseri kwa hii mambo.

Kiukweli a real trader kwanza hawezi onyesha trades zake hata siku moja huyo bado hajaiva.
Sema ataweza kukuonyesha anavyo trade basi Mana hakulazimishi umuamini.

Yaani mie mtu akiongea najua huyu ni trader ama educator or journalists unawajua.
Mpaka vitabu vyao unavijua.

Vitabu vya trading unajaza semi Ila vya ukweli unabeba mkononi vya real traders achana na vya hao waliokata tamaa
Kiongozi kuna jamaa yangu mwingine alinieleza amefikia sehemu ya kutoa ushuhuda ila nilivyomfuatilia zaidi nikagundua amepata kweli mafanikio kwenye demo account ila real haitembei kiongozi kiufupi biashara hii ni ngumu mno
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Hapa unaonesha unwamba wako kwenye field ya FX ila sasa sijui kama unaziishi hizo terms [emoji2][emoji2]
I don't need to prove anything to you. Mie bado newbie mkuu.
Hata Ontario hakuwa anaijua hii kitu kiundani Kama alikuwa anajua aliamua kuwaliza wana kwa spreads kubwa.
Pia broker ukiingia tu kwake anakucheki unavyo trade mwanzoni anaa accommodate kulingana unavyotrade anajua in long run you'll loose so ukinunua anakuuzia ukiuza ananunua Ila ukianza kumeki mane anakuweka kwa group la winners.
So trades zako anazipeleka direct kwenye interbank electronically anakuunga na liquid providers.

Hakuna broker anayekuibia ni wewe tu.
Inagwa wahuni wapo ambao sio regulated like with FSA Asic etc
 
Mkuu Kuna Vita nimepigana mpaka naona ni sawa watu wafeli kweli.
Yaani sio kawaida Kama unavyowaza. Napigana akaunti ikisoma £10M+ nitawapa vijana motto wa kutosha pia na withdraw kadhaa.

Huwa nawacheki watu wanavyoiponda nanyamaza.

Ishu hii ni ngumu hata msuli wa MD ukasome ni naseri kwa hii mambo.

Kiukweli a real trader kwanza hawezi onyesha trades zake hata siku moja huyo bado hajaiva.
Sema ataweza kukuonyesha anavyo trade basi Mana hakulazimishi umuamini.

Yaani mie mtu akiongea najua huyu ni trader ama educator or journalists unawajua.
Mpaka vitabu vyao unavijua.

Vitabu vya trading unajaza semi Ila vya ukweli unabeba mkononi vya real traders achana na vya hao waliokata tamaa
Asee ni zaidi ya msuli inahitaji vitu vingi sana kuelewa, pia uzoefu ni muhimu,
 
Kiongozi kuna jamaa yangu mwingine alinieleza amefikia sehemu ya kutoa ushuhuda ila nilivyomfuatilia zaidi nikagundua amepata kweli mafanikio kwenye demo account ila real haitembei kiongozi kiufupi biashara hii ni ngumu mno
Wale 95% hela zao zinachukuliwa na 5%
 
Asee ni zaidi ya msuli inahitaji vitu vingi sana kuelewa, pia uzoefu ni muhimu,
Shida ni kuupata huo uzoefu, yaani hadi umepata huo uzoefu umepoteza kiasi gani! Na bahati mbaya demo account haina morali.
 
Shida ni kuupata huo uzoefu, yaani hadi umepata huo uzoefu umepoteza kiasi gani! Na bahati mbaya demo account haina morali.
Hapo ndipo kuna suala la kujitoa, kama umejitoa na una nia na forex ;

Utakusanya maarifa na kuijua biashara namna inavyoenda, faida, hasara, risk management, profit management

Utafanyia mazoezi ulichokijua, hii inaifanya demo akaunti kuwa ya lazima na muhimu kwa sababu huwezi kufanyia majaribio hela

Utafanya trade kwa kuzingatia principle zote ulizojifunza, na kuendelea kutafuta maarifa mengine zaidi maana haina kugraduate, always be a stuudent
 
Pia unahitaji uwe na capital ya Mana ya ku execute standard lot Kama vile unavyobofya micro lot mkuu.
Tatizo waliowengi wakiwa na capital kubwa lot size wanazotembea nazo unakuta ni kubwa ndio maana si ajabu mtu kuunguza hata demo account ya usd 100,000[emoji2]
 
Tatizo waliowengi wakiwa na capital kubwa lot size wanazotembea nazo unakuta ni kubwa ndio maana si ajabu mtu kuunguza hata demo account ya usd 100,000[emoji2]
Ila na wewe bana mbona mie naunguza Hadi za milioni 5$ sembuse hao walaji moja,😂😀
 
Na pia katika kipato chako inatakiwa utenge kiasi ambacho ni mahsusi kwa ajili ya forex hii itakuongezea kujiamini sio unatrade na hela ambayo unamahesabu nayo kwenye matumizi yako ya mwezi

hii itakupunguzia kujiamini na kujikuta unaingiwa na wasiwasi ambao utapunguza ufanisi wakuexcute trade yako mwisho wa siku unapoteza
 
Ila na wewe bana mbona mie naunguza Hadi za milioni 5$ sembuse hao walaji moja,[emoji23][emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23] Pole sana mkuu, umenikumbusha jamaa yangu aliniambia kwamba amemaliza TSH 5,000,000/= Ila alivyopata ajira akanieleza kwamba anaenda kutafuta mtaji wa FX akiwin ajira ndio basi ila namuona huu ni mwaka wa tano na anayobidii ya kazi[emoji2] sijui kama kweli bado mawazo anayo ya kuiacha kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom