SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 65
[emoji867][emoji867][emoji867][emoji867]
Latvia mimi nakubaliana na hoja zako lakini hazina mashiko yoyote, mimi nategemea kwamba wewe unayeijua utaweka hoja zako ukiionesha jamii jinsi unavyoifahamu hiyo biashara, jinsi ambavyo umefaniwa na umeendeleza vipi mafanikio yako siyo habari zako za kuonesha kwamba hatujui bila kuonesha wewe umeifahamu vipi na unafaidika vipi au ndo unaugulia kimyakimya tu[emoji2][emoji2] leta hoja zako hapa sio maneno tu.
 
Stress zitakuua
Biashara ya FX ni sawa na vipofu wanaoanza safari kwa kuendesha mtumbwi kutoka Dar kwenda Zanzibar bila ya kuwa na mtu sahihi wa kuwaelekeza, hivyo wao wataamini zanzibar ni karibu sana na huenda watatumia muda mfupi kufika tatizo hawataona kilichopo mbele yao wala mawimbi na ukubwa wake na yanakotokea mawimbi hayo hivyo wasipopinduka mapema wataokotwa mbali tena wakiwa wamepotea sana na hari zao zikiwa mbaya mno kama si kufariki kabisa.
 
Inaumiza kichwa sana. Huo muda ukiamua usome blogging, adobe, content writing na vitu kibao unajikuta unajua madude na unapata angalau hela ya kuishi kwa siku. Sasa unasoma Forex msuli wake hata daktari ni kama chekechea alafu hupati faida. Huwezi kuwa na nuru, unajaa hasira na fake expectations, unapoteza muda, unakula hasara kibao
FX ni biashara za watu wanaopoteza malengo yao.
 
Pole sana, ila ninachoweza kusema kwa uzoefu wangu ni kwamba kila biashara inahitaji uzoefu na akili ili kutoboa.

Ukiwa na akili ya short-cut kwamba nitatoboa fasta ndani mwezi mmoja hapo ndo ni rahisi kukata tamaa na kuwa frustrated.

Mfano kati ya Forex na Kubeti bora kubeti. Hizo biashara mbili zote ni kamari, ila forex ni kamari ambayo haichezwi kwa uwazi kama mechi za soka. Na kwa Tanzania Forex haina ulinzi kwa kuwa haiko regulated. Mchezeshaji anaweza akatokomea na pesa zenu msijue hata pa kuanzia. Maana ile ni kama benki tu, mnaweka hela zenu kwa mtu awatunzie.

Na pili hapo ulipoongelea Jackpot ndo nimeona unjuka wako. Jackpot achana nazo kabisaaaaa. Zile ni mtego wa kuvuna hela. Na mikeka pia achana nayo chagua mechi moja ya uhakika kila siku.

Siri ya kubeti ni akili. Akili ikishachoka kuchambua mechi kwa sbb unatengeneza mkeka mreeefu ndo hapo unapoliwa. Ila ukiwa unatafuta mechi moja moja kila siku na kuongezea ulipoishia jana yake ni rahisi kupata milioni 80 ndani ya mwezi mmoja tu.

Mengine ni nenda mdogo mdogo. Kubeti kunahitaji angalau mwaka mmoja wa uzoefu (yaani upate uzoefu wa ligi mbalimali) ndo utaanza kupiga hela. Kwa hiyo sio umeanza tu unaweka madau ya elfu kumikumi au ada ya shule kama madenti wanavyofanya. Anza na madau ya jerojero. Utaliwaliwa kama mwaka mzima hivi ndo unajifunza. Laki mbili inatosha kwa kujifunzia mwaka wa kwanza. Baada ya mwaka utakuwa unajua mambo mengi sana kama vile mechi za uhakika za kubetia ni zipi, na ubeti nini ktk mechi hizo; kampuni gani zina odds nzuri, na muhimu zaidi ni uzoefu wa kuchambua mechi na mitandao ya kutumia ili kupata data.
Yaani ndugu yangu kubeti ndio balaa tupu yaani hapo unaweza ukabahatisha mkeka wa odd 5,6,10 hadi 100 na ukapata hata TSH 3,000, 000/= Kitakachofuata utakuwa ukiweka mkeka wa timu 3 unakosea 1, ukiweka timu 9 unakosa mbili yaani hapo unapata imani kubwa ya kumliza Mhindi na kusahau kwamba ile pesa uliyoipata ndio unazidi kuiteketeza na kuingia mfukoni Da! nayo hii haifai kabisa.
 
Timu tatu au tisa kwa dau la milioni 3 unatafuta nini?

Kila siku chambua mechi hata 50, halafu cheza moja tu. Kama umekwiva vzr, dani ya mwezi unaingiza milioni 80.

Halafu inatakiwa uwe na laptop na internet kwa ajili ya kuchambua data. Sio unabeti kwa kuotea tu, au kwa uzoefu wa kuangalia mechi za kwenye TV. Kuna ligi zina mechi nzuri sana kwa kubetia ila hazioneshwi kwenye TV, ni mpaka uzigugo.

Ila kama ni ngumu kuelewa basi fungua genge, duka au mgahawa. Hizi pesa za kuokota burebure achana nazo.
 
Mwanafalsafa umenifurahisha na mstari wako wa mwisho hizi pesa za kuokota bure ni heri kuachana nazo, kiufupi nilimaanisha kwamba mtu anaweza kuwa alishawahi kubashiri na kushinda labda hata laki tano lakini ataanza kuweka dau kidogokidogo kwenye mikeka yake na mwisho atajikuta anamaliza na ile aliyo ishinda na mwisho anaingia na mfukoni kwake.
 
Hizi kauli hutolewa milele na milele, kila mtu akifeli Forex hupewa sababu nyingi sana. Huwezi nionesha mtu aliyefanikiwa kwa Forex Tanzania hii, ina maana wote ni vilaza
Forex ni international trade kwanini unafocus Tanzania tu, kama kuna aliyefanikiwa akiwa Ujerumani au Singapore basi mahali popote unaweza kufanikiwa.

Kwa kuwa hakuna aliyewahi kusema hadharani au kuonyesha faida aliyoipata, haimaanishi kwamba hakuna aliyewahi kufanikiwa. Na hata mtu akifanikiwa hawezi kujitangaza watu wamjue (ili iwe nini?) kwa kuwa hii ni biashara ya mtu mmoja against market.

Isitoshe forex kwa bongo bado haijawa kama biashara rasmi inayotambulika na serikali, kwa hiyo ni wewe, PC na bundle lako tu.
 
Hii biashara siyo rasmi Tanzania ila inafanyika na wanayoifanya hatuwaoni wakifanikiwa lakini pia kupoteza fedha kwenye biashara hii na rahisi sana kuliko biashara zingine mimi nimefuatilia hata sehemu nyingine duniani mafanikio yao kwenye biashara hii hayako wazi sana ebu fikiria juu ya matajiri wakubwa duniani ni rahisi kukuta kwenye profile zao wanaonesha biashara wanazozifanya zinazoeleweka ila kwao fx ni nadra kuikuta, sasa hiyo biashara au sehemu ya kufilisi watu wenye uchu mkubwa wa utajiri[emoji779]
 
sio sehemu ya kufilisi watu wenye uchu wa utajiri bali ni sehemu watu wenye uchu wa utajiri wanafilisika,
there is no get rich quick in Forex
na mafanikio ni process ya siku baada ya siku kadri unavyotrade, hasara unazopata ndizo zitakufanya utafute mbinu mbadala ambazo mwisho wa siku zikikupa faida hiyo ndiyo inakuwa uzoefu wako.

Hata author wengi wa vitabu vya forex wanaweka bayana kwamba wamekuwa successful trader baada ya kipindi kirefu almost 4 mpaka 6 years, hivyo kwa mwenye uchu wa utajiri wa chap aliyefundishwa forex mwezi mmoja akafanya demo mwezi mmoja na kuanza kutrade live atakapo poteza hela aliyoweka hawezi kuwa na moyo wa kuendelea.
Hivyo tatizo sio Forex ni mtu mwenyewe kakosa msingi na taarifa za biashara husika. Forex trading ni professional kama zilivyo professional nyingine sio kamari, kama betting.
 
Mimi najiuliza BabaaJq mtu aliyeielewa biashara hii vizuri na akafanikiwa hadi kufikia level ya kuandika kitabu lakini bado mtu mwingine anakisoma kitabu chake na kuzielewa mbinu alizozielekeza lakini anapozitumia mbinu zilezile ambazo mwandishi anaziamini ndio ziko sahihi lakini bado anapata hasara sasa mtaalamu wa hii biashara ni yupi?.
 
Latvia mimi nakubaliana na hoja zako lakini hazina mashiko yoyote, mimi nategemea kwamba wewe unayeijua utaweka hoja zako ukiionesha jamii jinsi unavyoifahamu hiyo biashara, jinsi ambavyo umefaniwa na umeendeleza vipi mafanikio yako siyo habari zako za kuonesha kwamba hatujui bila kuonesha wewe umeifahamu vipi na unafaidika vipi au ndo unaugulia kimyakimya tu[emoji2][emoji2] leta hoja zako hapa sio maneno tu.
Mzee sjaiii shikiwa akili na wajinga jinga kama kina lunatoc Singo & keisangora hadi kujiunga na huo upatu.
Kwanza nina elimu saafi toka Riga nchini Latvia.

Naona vijana wanavyoteseka sana mitaani na misemo yao ya kujipa moyo eti.. Cash Inayo flow kwa Forex per day ni zaidi ya uchumi USA.. So what?

Wananishawishi sana nijiunge na huo utapeli kisa wanaona ukwasi wangu daily but mChagga mimi mweye elimu kindaki ndaki toka Riga nchini Latvia nawajibu kwa upole.. Fanikiwa kwanza then nitapita njia ulizopita wewe.

Anyway.. Mtajeni hata mtu mmoja tu aliyefanikiwa kwa Forex hapa TZ.. Wanapoteana.

Kuna watu wapo huko Bahamas wanakula bata Ile mbaya kwa cash za wajinga jinga wa forex all over the World.

Mtu smart hawezi jiunga na huo utapeli wa wazi wazi.

Ni ujinga kiasi gani unaweka cash then Inaliwa unaweka tena na tena na tena.. khaaa!

Maaaanina zenu.
 
Sasa umekosea hicho kichwa cha habari. Ungeandika kampuni zinazotumia mtandao kujipatia pesa.

Biashara mtandaoni ni kitu cha tofauti , maana kuna biashara za bidhaa kama nguo, electronics, viatu, stationaries, huduma kama usafi, ufundi, mapambo, etc.

Halafu wewe unasema utapeli wa biashara za mtandaoni.....
 
Nilikuwa nadharau Sana betting lakini siku moja nikasema ngoja nijifunze nikadownload some applications....nikajifunza vitu vichache usiwe tempeted Sana na kupata millions kwa bet moja plus hizo jackpots, sio kila siku au kila mechi lazima uingie kucheza, fanya uchambuzi vizuri siku moja kabla ya mechi , live bet wakati mechi inachezwa it's better mfano mechi ziko dk 80 mtu kashamzidi mwenzie goli 2 bila au 3:1 halafu unakuta odds ndogo Sanaaaa ukiweka hapo elfu 10 and above huwezi kosa pesa na hizo Mimi sijawahi poteza pesa Cha msingi uwe na muda na kuwa sharp online zinapotokea hizo opportunity...nisehemu ambayo huwezi kosa pesa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sasa umekosea hicho kichwa cha habari. Ungeandika kampuni zinazotumia mtandao kujipatia pesa.

Biashara mtandaoni ni kitu cha tofauti , maana kuna biashara za bidhaa kama nguo, electronics, viatu, stationaries, huduma kama usafi, ufundi, mapambo, etc.

Halafu wewe unasema utapeli wa biashara za mtandaoni.....
Kwani hujaelewa nini Samcezar, kwa sababu nilichokitia ni tahadhari kwamba biashara za mtandao nyingi tena kwa asilimia kubwa ni chanzo cha umaskini na kwenye maelezo yangu nimetoa mifano ya fx, forever, betting na kadhalika kuwa na duka na kuuza bidhaa zako hapo mitandao inatumika kama njia ya kuitangaza biashara yako na kutafuta wateja wapya ni tofauti kabisa na biashara ninazozizungumzia ni tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom