Tahadhari:Corona imekuwa fursa kwa matapeli ,wanajifanya wametoka Wizara ya afya wanataka kupuliza dawa ya Corona na kuiba majumbani, kuweni makini

Tahadhari:Corona imekuwa fursa kwa matapeli ,wanajifanya wametoka Wizara ya afya wanataka kupuliza dawa ya Corona na kuiba majumbani, kuweni makini

Course Coordinator

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2019
Posts
1,742
Reaction score
3,224
Habari wana Jamvi,

Wakati dunia inahangaika kutafuta dawa(tiba) ya kutibu ugonjwa wa Corona Virus Covd19.

Ikumbukwe hadi sasa watu wapatao 111,000 tayari wameambukizwa katika mabara 3 na zaidi ya watu 3,890 tayari wamepoteza maisha .

Hivyo hili ni Janga kwa Dunia nzima.

Lakini kwa wenzetu matapeli(conman) hapa nchini kwetu wanaona kama ndo fursa ya upigaji na kujitafutia kipato
..
Kuna baadhi ya matapeli wanatembea majumbani na kujitambulisha kuwa wametoka wizara ya afya kwa ajili ya kupiga spray kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa Corona Virus ...hivyo ukiwaruhusu tu kuingia ndani wanakuliza pesa,vito vya thamani, simu, na vitu vingine vya kubebeka kwa urahisi.

Hivyo kwa wale mnaowaacha ma-ma-house girl majumbani ni bora mkawapa tahadhari kwa kipindi hiki ili wasije wakawarubuniwa kwa kuwaruhusu matapeli hao kuingia ndani mwisho wa siku wakaiba au kutapeli.

Tahadhari ni mhimu .
Aidha nawakumbusha kuchukua tahadhari ya kutosalimiana kwa kushikana mikono ,na kuepuka kusogelea maeneo yenye msongamo wa umati wa watu wengi..kunawa mikono mara kwa mara ,hata ikiwezekana kuacha mara moja kununua nguo za mitumba au nguo zozote zilizotoka China au Italia kwa kipindi hiki kwan katika nchi hizo maambukizi ni makubwa zaidi kuliko nchi zingine .
Protect yourself and your community from coronavirus with common sense precsution,listen the local health centre authority and listen to the experts and follow the science.

Mungu Ibariki Tanzania,Tuepushe na Corona virus.
 
😂 😂 😂 😂 aisee nacheka kama mazuri vile,
 
Back
Top Bottom