Usifanye biashara kwa hela ya kustaafu kama hujawahi fanya biashara, ili usipate magonjwa ya moyo, pressure, kupooza nk. Ni mara kumi upambane na wapangaji akishindwa lipa utasamehe ataingia mwingine, utaishi.
Mzee wangu tangu astaafu ana miaka 27 kwa afya tele, shida tu pressure ya macho hatujui tiba yake. Angalau vibanda vyake ndivyo umuweka mjini. Bila hivyo kitambo sana angeshawahi kwa Yesu.
Kufanya Kazi hakuzuii kujiajiri.Hata serikali inawashauri watumishi wafanye ujasiliamali Ili wapate uzoefu, maana wengi ufa baada ya kustaafu kwa kuingizwa mkenge wakizipata zile pesa, motivation speaker uwatembelea sana.
Jifunze kupitia visa hivi;
1. Pana mama anaugua pressure na kisukari alidanganywa dili fulani feki la utajiri wa haraka, akazichukulia mkopo shs milioni 200, nyumba zake nne alizojenga kwa kujinyima akiwa mtumishi kapoteza zote zimepigwa mnada.
2. Pana mstaafu aliambiwa treka zinalipa akachukua milioni 100 akanunua trekta mbili mpya leo zipo juu ya mawe na pressure juu hana hata mia ya kununulia spea.
3. Pana mstaafu Shemeji yake alimwambia pikipiki zinalipa ukizinunua china na kuleta bongo kuuza akampa Shemeji yake milioni 200 akafunge contena la pikipiki. Shem akapotelea nazo china.
4. Mwingine akazinunulia bajaj aliambiwa zinalipa kwa siku moja inalaza elf 30 akazinunua 10 leo zimepaki juu ya mawe.
5. Mmoja akastaafu akaambiwa dagaa zinalipa ukileta dar toka Mwanza,akaenda kufunga tela na mtoto wake yaani pulling yote imejaa dagaa kwa milioni 50. Kufika nzega gari imekata spea,spea inabidi itoke Dar siku tatu wamekaa njiani ,mvua ikanyesha mzigo wote umelowa maji kufika Dar mzigo aufai ikabidi ukauzwe chakula cha kuku.
6. Mwingine akastaafu akanunua daladala akiambiwa daily hakosi laki moja, akachukua za kustaafu. Vijana kila siku hadithi mara traffic, mara majembe, mara sijui garage, mzee akawa anashinda barabarani anahesabu tripu za daladala. Haya si mateso jamani.
7. Umestaafu umejenga guest kuogopa kupigwa eti unakaa reception, anaingizwa binti wa shule sawa na mjukuu wako na libaba nawe unapokea pesa za kwenda kuchafua shuka si laana hii! Huu ni umri wa kutengeneza na Muumba wako na siyo kusimamia uzinzi hata kama ni biashara.
Pana guest Mbeya zinaitwa ten commandments, huna cheti cha ndoa siyo ruksa kulala jinsi mbili chumbani. Sawa analinda maadili kwa biashara isiyo na maadili. Visa ni vingi Sana.
Ni laana sana kula hela ya mstaafu aliyetumikia taifa kwa miaka 40. Tuwaonee huruma tusiwe chanzo cha vifo vyao.