Tahadhari ili kuepuka gharama uji wa ulezi huchanganywa na unga wa mchele

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Nimeona niwape tahadhari kabla ya kuwatakia usiku mwema

Ni kwa wale Ndugu zangu wanaopenda kunywa uji wa ulezi kama mimi hapa.

Huu ni utafiti usio na chembe ya uongo kuhusu uji wa ulezi unaouzwa kwa kutembezwa barabarani na Wamama hususani hapa Dar es salaam

Inadaiwa kuwa uji huo huwa unachanganywa kwa ufundi mkubwa na mchele uliosagwa.

Sababu ni gharama kubwa za unga wa Ulezi hivyo wauzaji huchanganya na mchele ili kuufanya uji huo uwe mzito na hivyo kumpatia muuzaji faida huku mnywaji akikosa virutubisho muhimu

Unashauriwa kuwa makini na matumizi ya uji huo unaotembezwa barabarani vinginevyo nenda sokoni nunua unga kisha mpatie mkeo akuandalie

Njia rahisi kugundua mchanganyo huo haramu kwa wazoefu ni ladha tu ya uji kuwa siyo ya kawaida

Ucku mwema

 
doh acha kuharibu biashara za watu..uji mzuri kabisa au unataka tuanze kushusha nondo za mchelw vs ulezi?
 
Unakumbuka ile taasisi ya Lishe serikali iliifuta?
Inawezekana serikali ilifanya hivyo kwa ujinga ilionao, kutojua umuhimu wa taasisi kama hiyo.
Hata hivyo nachelea kusema serikali itakuwa imechukuwa uamzi kama huo kwa vile taasisi ilikuwa ikifanya kazi zake kwa ueledi.

Mambo kama haya uliyo yaelezea hapa hutokea kwenye nchi hovyo hovyo kama hii yetu sasa hivi. Serikali hakuna inalosimamia kwa ufanisi, kila jambo ni hovyo hovyo tu.
 
Mkuu kwani TFNC -
"Tanzania Food and Nutrition Centre" ina kazi gani?

TFDA unayosema haikufutwa bali ilitengenishwa Vyakula kivyake na Madawa kivyake ili kuleta ufanisi kwa hiyo vyakula vinasimamiwa haswaa.
 
Sijaelewa kitu hapo, nikwamba huo unga unachanganywa baada ya uji kuiva au unachanganywa na unga wa ulezi alafu vinapikwa kwa pamoja?
 
Maziwa kuwa ghali Tanzania ni jambo la kujitakia. Nadhani nchi yetu ilitakiwa maziwa mengi kiasi cha watu kuogea kama wanataka bila kuhofia bei.
 
Wanaweka hivi kwa watoto. Wa watu wazima mara nyingi huwa ni ulezi bila kuchanganya unga mwingine. BTW uji wa ulezi na mtori origin yake ni uchagani na hivi ni vyakula vya mama waliojifungua.
 
Wanaweka hivi kwa watoto. Wa watu wazima mara nyingi huwa ni ulezi bila kuchanganya unga mwingine. BTW uji wa ulezi na mtori origin yake ni uchagani na hivi ni vyakula vya mama waliojifungua.
Ulezi pekeyake?
 
Ulezi pekeyake?
Yeh, unga wa ulezi wanaweka maziwa mgando baada ya uji kuiva. Huu ni upikaji wa asili unavyokuwa huko uchagani. Pia huwa wanaongeza siagi kama uchumi unaruhusu. Huu upikaji wa uji wa ulezi kwa watoto ambao huchanganya vitu kama karanga, ngano nk. ni version ya ambayo imeanzia mjini.
 
Kuna desa jipya kwani?
 
Yaani unavotoa hiyo tahadhari utafikiri watu wanalishwa sumu. Unga wa mchele si ndio vitumbua hivyo? Mchele si ndio wali huo? Au umeeambiwa hii combination ya mchele na ulezi ni sumu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…