LOooh! Joannah.
Ni hivi: kabla hata ya kwenda huko kwenye ubora n.k., ni udanganyifu, kudai kwamba mtu anauza uji wa ulezi, wakati ni mchanganyiko wa ulezi na unga wa mchele. Aseme tu wazi kwamba anauza uji uliochanganywa ulezi na mchele, na watu wanaotaka uji wa namna hiyo watanunua kwa hiari yao wenyewe, kwa bei iliyopangwa na muuzaji.
Kuna watu unapowaambia ni uji wa ulezi, wanajuwa ni ulezi ambao haukuchanganywa na mchele, na wao watanunua kwa bei husika. Hapo hakuna udanganyifu wowote.
Kuhusu utofauti uliopo kati ya ulezi na mchele, kuna vitu vingi; inaweza hata kuwa ni muonjo wake tu; kiasi cha wanga, 'fiber', na kadhalika. Bado hatujazungumzia madini, na hata kiasi cha protein, hata kama ni kidogo sana kwa kila moja wapo.
Lakini ninachokusisitizia ni hilo la kutokuwa mdanganyifu unapofanya biashara ya aina hiyo. Bila shaka unajua kwamba bei ya ulezi ipo juu kulko bei ya unga wa mchele. Sasa nikuulize hapa, wewe unadhani ni kwa sababu gani?