Samatime Magari
Senior Member
- Feb 10, 2017
- 119
- 457
NI gari flani zamani ukinunua Scania wanakupa kama nyongeza 😎..
.
Wadau wengi wamevinunua ili kufanyia biashara ya mizigo sasa basi ni vyema tukapata ABCD zake, maana usipovielewa vitakupasua kichwa..
.
Suzuki Carry imezaliwa toka Tanganyika inapata uhuru 1961 mpaka leo bado kinazalishwa and as we speak kina generation 11, NI vigari flani old school sana though Bongo tulianza kuvileta miaka ya 2000, Inasemekana kuna mchaga mmoja aliagiza Scania wakampa na haka kagari kama nyongeza..
.
Basi alivyokuja nako akaanza kubebea mizigo yake binafsi kutokana na consumption nzuri akakisifia. Raia wengi wakaanza kuvipenda demand ikaja Jamaa nao wakaanza kuviuza wakati walikua wanatoa kama nyongeza..
.
As i said Carry iko na generation 11, Generation ya 1 [1961-1964], G2 [1965-1969], G3 [1966-1969], G4 [1969-1972], Generation 5 [1972-1976], G6 [1976-1979], G7 [1979-1985], G8[1985-1990] G9[1991-1998] G10 [1999-2012] na G11 [2013-Todate], Inshort Kina uzao kweri kweri This is to say hii gari kwenye uzazi wa mpango haikua serious Kabisa..
.
Ndo maana kuna time hata mwenzake hajafikisha miezi 9 kengine tayari kameshazaliwa. Vimekuja na body shape aina 2 tu, Suzuki carry Pick up truck na Suzuki Carry Van maarufu kama Suzuki Every..
Carry ni gari ya biashara[commercial vehicle] so usitegemee comfortability hapa, Ndani pale kwa dereva Kioo chake ni kama umevaa miwani kiko karibu sana. Dashborad utafikiri saa mkononi ukiwa bonge au mrefu sana haukai vizuri mle, Radio ipo ya kawaida tu haina mbwembwe..
.
A/C kuna baadhi za kisasa zipo zingine hazina ila kuna option ya fan kama sijakosea, Ila ukitaka radio nzuri unaweza funga sema ukisema uweke speaker hapafai pale ndani ni padogo sana. Unaweza washa redio ukawa unasikiliza mziki kama uko ndani ya speaker vile..
.
Kwa nje kina kuonekano simple tu usiokua na mambo mengi ila unawavutia traffic, Nyuma kawaida kuko flat kwa ajili ya mizigo na mbele kuna seat 2 tu ya dereva na abiria wake mmoja. Na hapa kuna kichwa kikubwa [extended cabin] na kichwa kidogo [standard cabin]..
Kwa bonge au mtu mrefu hii kichwa kikubwa ndio option nzuri zaidi maana yenyewe pale mbele iko na space zaidi kuliko huyo mwenzake. Tanzania tunatumia generation ya 8[1985-1990], 9 [1991-1998], 10 [1999- 2012] na 11 [2013++] Kwa uchache sana..
.
Sasa huko kwao wanakiita Suzuki light carry ila Bongo tumakageuza Suzuki heavy Carry, Maana hii gari inatakiwa ibebe kilo 350 za mzigo [Kama mifuko 7 tu ya cement ] Ila wananchi wa Chief Hangaya wanajua wenyewe wanachokifanya hapa..
.
Ukiangalia ni kigari flani ambacho hakipendi shida ila sasa kwa mazingira ya Bongo lazima kipambane nazo tu, Vimekuja na engine ndogo zikiwepo za cylinder 3 [cc 539-657] na 4 [cc 797-970]. Zikiwa na 4/5 Manual transmission na 3 speed AT vikiwa na option ya 2WD na 4WD..
.
Hivi vya cylinder 4 walitengeza kwa ajili ya soko la ulaya. Kwa Japanese Domestic market wakabaki na cylinder 3 kama Passo Pasua ambavyo ndo hivi tunatumia na sisi huku wadau wa royal tour. Hizi engine za Piston 3 cc650 mafuta zinatumia vizuri sana kikiwa poa kabisa With no issues kanaweza kukupa mpaka 18-20Km/L..
.
Top speed ni 120Km/h though mara nyingi kinaishiaga 80Km/Hr Full Tank ni Litre 30 Na engine zake kuna zinazotumia Carburetor na za Direct injection. Hizi za carburetor kama wewe ni mdau wa hivi vigari au unategemea Kununua siku za mbeleni kwa ajili ya biashara sikushauri ununue go for Direct injection, kabla hatujaendelea tujue carburator ni nini kwanza.. .
.
Carburetor ni kifaa kinachochanganya hewa na mafuta kwenye engine kwa ajili ya internal combustion kwenye engine katika uwiano sawia, Sasa sababu ya mazingira yetu na mafuta carburetor zinachafuka na kuziba mara kwa mara na kuzuia mzunguko sahihi/rahisi wa mafuta. Na hapa ndo unakuta gari ina miss au haitulii silence au inakosa nguvu na hali hii inasababisha fuel pump kufa mara kwa mara..
Engine zake zina nguvu ndogo ukikapa mzigo mkubwa then ukawa unaforce kakimbie sana unasababisha mlundikano wa mafuta mengi kwenye clinder [Rich mixture].. . Hii husababisha liquid hammering kwenye cylinders na hizi gari zina cylinder zake ni delicate utafikiri mapafu ya mtoto..
.
Cylinder zikitanuka au kupata michubuko huwa hazitulii tena. So ni muhimu ku accelerate gently hasa pale gari inapokua na mzigo maana hakachelewi kuanza ku-smoke then kufa engine. Hapa ndo utaambiwa gari imezungusha mkono unaanza kujiuliza mkono upi mbona sijawahi kuona..
.
Vina tabia ya kuchemsha na kukosa nguvu kutokana na kupiga kazi sana. Hebu imagine unatakiwa ubebe mifuko 7 ya cement ila waja wanakubebesha mpaka mifuko 20++, Kutoka Kg 350 mpaka Kg1000 yani unafanyishwa kazi mara 4 ya uwezo wako hapa lazima utachemsha tu..
.
Unakuta gari muda wote engine inakua overworked temperature iko juu na inaleta overheating. Ikishaleta hivi mafundi wao ni kufunga fan direct tu [inazunguka muda wote]. Hapa napo ni swala la muda tu hiyo engine ita RIP na ukishaona hivi achana na mswaki kanunue engine full..
.
Gari parts zake za chini kama tie rod end, bushes, shocks etc hazijawa designed kama za gari kubwa [off roaders], So acha kufukia nacho mashimo, Yani kwenye njia mbovu pita nacho taratibu ukipata mkeka mzuri ndo kikimbize. Bila hivi vitu kufa huko chini itakua daily..
.
Fanya service kwa wakati na weka oil nzuri na fanya vitu nilivyokwambia hapo juu na gari itakaa kwa kuda mrefu tu bila usumbufu na utapata matunda ya pesa yako. Kikubwa Hii gari ina engine ndogo sasa inakua rahisi kupata overheating pale unapoifanyisha kazi sana au unaipa Mzigo mkubwa tofauti na uwezo wake, so unakua advised kubeba recommended load tu ili kiwe safi na kipate maisha marefu..
.
Sema nikiwaza tajiri anataka hesabu na dereva anatakiwa kuishi hapo hapo sometime dereva hata akipata kazi za kubeba tofali anakipigisha mzigo bila huruma.. Suzuki Carry kuitoa Japan Million 10-12 unapata, inaweza panda zaidi kutokana na Mwaka wa matengenezo na condition ya gari, Hapa nchini showroom unaipata kwa 14M mkononi 5M++.. .
.
Kama unahitaji kuagiza gari, kununua hapa nchini showroom au mkononi karibu tutakuassit. Tunafanya kazi na dealers wa Japan, UK, Singapore na hapa nchini, dealers wanaotupa gari nzuri kwa ajili yako..
.
Simply njoo WhatsApp [0714547598] au ofisini Kigamboni tutaku assist, Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu pia, Utatupa hitaji lako Tutakupa ushauri bure then tutakutumia options 2 3 za gari ili uchague ukipendacho..
.
Ukishachagua utapewa invoice na utafanya malipo at cost [no extra cost], Malipo utafanyia huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo..
.
Asante
Samatime car dealers
Get a smart car like you