Tahadhari kubwa sana kwa Wana CCM, usikubali

Tahadhari kubwa sana kwa Wana CCM, usikubali

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Wapemba wanasema kaa chonjo saa mbaya. Ewe Mwana CCM upepo unaovuma ni kivumbi cha wananchi walio wengi tena wenye hasira ambao wameamua kupiga kura kwa kishindo kuondoa utawala na kusimika uongozi.

Usikubali kutumika kuingilia au kutumwa kuvuruga mwendo kasi huo, watawala watakuja kukukana na kutokutambua utokako. Kaa mbali na kivumbi maana pataruka kivumbi, sasa mtawala atakaekutuma ukatulize kivumbi hicho hakutakii mema na akikwambia vuta bangi, kunywa pombe ili kuongeza ujasiri, huyo anakualika kifo sio mazishi.

Wapiga kura wakija kukutia mkononi na mawe yako ujue hutawahi kufika kituoni umeshaaga dunia, si unaelewa majambazi wanapokamatwa na polisi hawafiki kituoni wameshatoka roho inaonyesha kuwa polisi walipambana kufa na kupona kuhakikisha majambazi wanaiwa mkononi na kufikishwa kituoni wakiwa hai au wamefariki kwa sababu za mapambano.

Mabadiliko haya ni makubwa ni wazi kabisa kiuhalisia haki ikitumika CCM itashindwa maeneo mengi sana ikiwemo Uraisi, hivyo ,wanaccm msikubali kutumika kufanya uhuni, mwambie anaekutuma aende yeye.
 
Back
Top Bottom