DOKEZO TAHADHARI: Kuna watu wamepata madhara baada ya kula mboga za majani zilizonunuliwa stendi ya daladala Mbezi Luis

DOKEZO TAHADHARI: Kuna watu wamepata madhara baada ya kula mboga za majani zilizonunuliwa stendi ya daladala Mbezi Luis

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Pale Luis tunatambuaje mboga zanazotoka Kibaha kwa Mathias na za kwingineko? Anyways Mamlaka zipo wakachukue sample wakapime.Ni vipi umehitimisha kama vile umeshapata majibu rasmi kuwa tatizo linasababishwa na mboga na tena zinazolimwa Kibaha?.
 
Habari ya mchana

Nimeamua niwaandikie wenzangu kwa kifupi kuhusu madhara rafiki zangu waliyoyapata baada ya kununua mboga za majani pale stendi ya daladala Mbezi Luis.

Siku chache zilizopita rafiki zangu Hawa walinunua mchicha pale stendi ya mbezi Luis na kwenda kuupika na kula. Madhara waliyoyapata ni pamoja na kuchubuka ngozi, kushindwa kupumua vizuri, kuharisha damu, kutapika damu, vidonda vya Tumbo na kichwa kuuma sana muda wote. Hawa rafiki zangu walikwenda hospitali na kupima vipimo na kugundulika wamekula mboga zenye vimelea sumu. Pia Kuna taarifa mgonjwa mkaka amefariki kwa kula mboga hizi alizonunua mbezi yeye alikuwa akiishi kinyerezi.

Uchunguzi wa haraka niliofanya baada ya kuuliza ni wapi wamezipata zile mboga za majani wakasema wamezichukua zinapolimwa kibaha kwa Matias na chache picha ya ndege huko huko kibaha.

Naombeni kuwataadharisha kuhusu Kununua mboga za majani mbezi Luis zilizoagizwa kutoka zinapolimwa kibaha kwa Matias. Naomba uusambaze ujumbe huu kwa wapendwa wako utakuwa umeokoa maisha yao. Pia taarifa hizi nimezipeleka mamlaka husika

Asanteni
Magonjwa yote hayo? Mpaka vidonda vya tumbo siku hiyo hiyo? We una lako jambo
 
Back
Top Bottom