rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Upo sahihi watanzania usitaarabu ni zero si wanaume si wanawake si vijana Wala watu wazima wanaona kupanga foleni ni tatizo.1. Utaratibu ule ulifanikiwa hapo awali wakati ulinzi ulikuwa ukisimamiwa na SUMA JKT, baada ya kubadilisha na kuweka kampuni binafsi ya ulinzi wanashindwa kudhibiti abiria kupanga foleni.
2. Utaratibu wa kupanga foleni unakuwa mgumu sababu unahitaji sana kuratibiwa na madereva wa mwendokasi ambaya anapaswa kudhibiti abiria kwa kuhakikisha mlango mmoja tu wa gari ndio unaofunguliwa, badala yake wakifika vituoni kama kivukoni wanafungua milango yote na kusababisha watu kugombania. Kwa kweli ni kero sana hakuna ustaarabu tena.
Pia watu wa ulinxi waondolewe itafutwe kampuni nyingine.
