Tahadhari: Kwa hali ilivyo tusishangae kushuhudia kifo au vifo kwa wanagombania kupanda Mwendokasi

Tahadhari: Kwa hali ilivyo tusishangae kushuhudia kifo au vifo kwa wanagombania kupanda Mwendokasi

Last week ndugu yangu aliumia mgongo kwa kusukumwa akipanda Mwendokasi Kariakoo. Nilitoka Mwanza kwenda kumsalimia kisha nikaenda kujionea mazingira yaliyopelekea yeye kuumia.

Naomba niseme tu kwamba kwa hali ilivyo kituo cha Msimbazi na Gerezani sitashangaa kukatokea kifo.

Kwa namna watoto wanavyosukumwa na jinsi abiria wanavyogombania magari tutapata maafa.

Niwaombe viongozi wa Mwendokasi na viongozi wa serikali, itasikitisha sana kujitokeza kuomboleza vifo vya wanafunzi katika kituo cha Msimbazi, Kivukoni,Gerezani, DIT,Fire, Korogwe na Kimara. Naandika just kutoa taadhari nikitambua sikio la kufa alisikii dawa
Kiukweli kwenye mwendokasi huwezi kuona tofauti ya binadamu na mbuzi maana Kuna kitu fulani ambacho hutegemei kufanywa na binadamu mwenye akili timamu.Prukshani zote zile eti mtu apate siti wakati safari yenyewe haichukui hata dkk 30.Tubadilike.Jambo la pili mwendokasi zinadharirisha utu wetu.Watu wanabanana kama magunia ya viazi sio sawa.
 
KUNA PROF MMOJA ANASEMA MKIPANDA MAGARI YA UMMA,HAMSOMI VITABU

Ova
 
Kiukweli kwenye mwendokasi huwezi kuona tofauti ya binadamu na mbuzi maana Kuna kitu fulani ambacho hutegemei kufanywa na binadamu mwenye akili timamu.Prukshani zote zile eti mtu apate siti wakati safari yenyewe haichukui hata dkk 30.Tubadilike.Jambo la pili mwendokasi zinadharirisha utu wetu.Watu wanabanana kama magunia ya viazi sio sawa.
Nimeuliza kwanini hawapangi foleni wanasema ukipanga foleni utakuwa wa 1000. Sasa umefika kituoni wewe ni mtu wa 1000 unataka uwe wa kwanza kweli mtakosa kuvunjana viuno?
 
Waondoe ukiritimba, warugusu ushindani kwenye routes za mwendokasi na daladal ziwepo.
Nakazia hoja na pia kama hawataki ushindani basi wajenge guard rails za mabomba mazito zitakazo lazimisha watu wakae kwenye mstari aka .foleni (Ni pendekezo langu ila wanaweza pia kutumia njia nyingine) tusisubiri maafa. :KEKBye:
 
Serikali muda mwingine inawaletea matatizo wananchi kwa makusudi.

Warutishe route za kwenda Mbezi na Kimara. Mwananchi ndiye ataamua kupanda Mwendokasi au daladala.

Hizi ndio akili za viongozi wetu zilipoishia waliua mashirika ya ndege binafsi na kutuletea Air Tanzania ambayo ni gharama sana na huduma za kusuasua.

Waache ukiritimba. Waruhusu ushindani kwenye ugawaji wa huduma.
 
Nimeuliza kwanini hawapangi foleni wanasema ukipanga foleni utakuwa wa 1000. Sasa umefika kituoni wewe ni mtu wa 1000 unataka uwe wa kwanza kweli mtakosa kuvunjana viuno?

Havunjwi mtu yani ni mapambano tu na siti unapata 😁😁😁
 
Back
Top Bottom