Tahadhari kwa maafisa elimu wanao zunguka na fomu za vitisho

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
208
Reaction score
72
Natoa ushauri kwa maafisa wanaozunguka na fomu kuwa waache mara moja, nadhani wamefanya taathimini na kuona hali halisi nawashauri kwa kesho wasifanye hivyo tena vinginevyo wasije kutuona wabaya kwani uoga wa walimu haupo tena. Unawaambiaje walimu wajaze fomu wanaogoma wakati wamepita na kuona hawapo kazini wajaze wenyewe kuwa wlimu hawapo kazini. wanawapa wakati mgumu walimu wakuu walioamua kujitolea kukaa shuleni.

Halafu wakumbuke kuwa na wao ni walimu wasijione kuwepo ofisi za elimu wao nao ni miungu. Kama vipi wagawane waende kufundisha. Wakiendelea na vitisho hivyo na sisi tuunde jeshi la kuwasaka maana sisi tunajua kona zipi za kuwavizia ili kuwaonyesha kuwa tumechoka na unyanyasaji. Leo wamejionea kuwa wao si tishio tena kwa walimu.

Kama ni hivyo waache mara moja kututisha tumegooooooooooooooooooooooooooma!!!!!!!
 
Sehemu kubwa ya maafisaelim ni mafisadi. Wanatafuna sana hela za halmashauri,
 
Maafisa elimu wengi,
wamepata vyeo hivyo,
kwa aibu kubwa.

Kuwavulia kaptula viongozi wa CCM,
au kuwa makuwadi wa waheshimiwa,
kufanikisha kuwabaka,
walimu wapya wa kike,
kwa matishio ya kuwahamishia bushi zaidi.
 
Hayo maovu yao ndo yanawafanya wakurupuke. Ni wakati wetu kuwaonyesha kuwa sisi ni walimu wala si mazuzu. Vitisho havitasaidia watulipe madai yetu. Na huyu mzee wa wazee wa dare ssalaam atahutubia nini au anasubiri ashauriwe na Pinda na Rwemamu ndo ahutubie.

Wanamdanganya sana hivi yeye akili ya kuambiwa hachanganyi na yake maana huwa anakurupuka tu. Akikurupuka hili la walimu litamweka pabaya maana walimu wameamua aache kuahirisha matatizo kwa kwenda mahakamani. Na hata tukirudishwa kazini kwa nguvu tutaenda kupiga stori mwanzo mwisho. Viongozi wa kisiasa si tishio tena kwa walimu TUMEAMUA HATUTAKI KUONEWA. KUONEWA SASA BASI. TUNASUBIRI VIRUNGU SI ALISEMA ATATUPIGA VIRUNGU DIKITETA WETU.
 
Me sikanyagi shule hadi nisikie kauli ya Gratian Mkoba....bila kauli yake, hakuna ambacho kitafanyika. Leo hapa Mpanda mjini, askari polisi waliwakamata Katibu na Mwenyekiti wa CWT kwa sababu walipita mji mzima na gari lenye mic ambalo lilikuwa likitangaza kuwa kesho (leo tarehe 30) hakuna mwalimu kwenda shule, na kwamba atakaye kwenda atakuwa amejidhalilisha...! Wamewashika na kuwasweka Lumande...walimu walikusanyika kituo cha kati cha Wilaya na kuhakikisha kuwa viongozi wetu wameachiwa huru na hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi yao...tukaandamana hadi ofisi za CWT wilaya tukaacha na kurudi makwetu....RAHA KWELI, HADI WAKOME WASHENZI HAWA WAMEZOEA KUTUFANYA SISI VIJAKAZI VYAO....Kesho kama kawa...mimi asubuhi naingia kwenye bustani zangu...sikanyagi shule. SOLIDARITY FOREVER!!!!
 
wakazieni msuli 2muone kawambwa atafanya nn, nilikimbia hii kaz kwa upuuz wa wa2 wa elimu pale temeke manispaa.
 
Hii ngoma safi sana,nimefurahi sana kupata taarifa mbalimbali za mgomo na mafanikio ni makubwa sana.Hakuna kuchoka wala kurudi nyuma,liwalo na liwe.....Arrrrrrrrrrrrrrrrrgh!
 
Maafisa elimu wengi,
wamepata vyeo hivyo,
kwa aibu kubwa.

Kuwavulia kaptula viongozi wa CCM,
au kuwa makuwadi wa waheshimiwa,
kufanikisha kuwabaka,
walimu wapya wa kike,
kwa matishio ya kuwahamishia bushi zaidi.

haah haah mkuu hapa naunga mkono hoja mia.mia
 
Waheshimiwa walimu poleni,
kwa masahibu yote yalo wakuta,
nawaunga mkono kwa dhati,
endelezeni msimamo wenu,
hata ikibidi gomeni mpaka Novemba 2015,
acheni fanywa bwegge na CCM,
kwa faida yao binafsi na wake zao.

Kazeni buti walimu,
manunda wapigeni makwanja,
ukombozi jikomboa kata kamba,
wakoloni weusi tii wa CCM ya mafisadi,
si jambo la kuchelea asilani
ni la lazima na muhimu tekelezeni,
wasiwachezee manunda habithi CCM,
hekima yao siku zote ni ujinga na kiburi.

Weusi wenzetu hawa mamruki,
kwa kutamani shangingi waiuzaa nchi,
siku zote waabudu fedha na wageni,
matapishi yao ya kale wayafanya Tunu,
wajitunisha mifuko kwa ngawira haramu,
kwa gharama ya taabu na ufukara wetu,
wauza ardhi na watu pia,
Uhuru wetu bei sokoni wamefikia.

Walimu nawaomba msiwalegezee,
manunda kenge hawa wa CCM,
wao hujilipa posho za mabilioni,
kwenye warsha za ovyo gubikwa utusi,
zajaa umalaya ubasha sagana,
tembezan wake waume changanya,
hayawani mbwa twawasingizia,
wazee mvi sharubu magugu makavu,
kuzini na vijana wadogo uturi maziwa ya mama,
Warsha za kupeana na kuvuliana,
vyeo vya chupi na heshima uchini.

Walimu sasa inatosha,
mmnenyanyasika kwa miongo mingi mno,
hata lini mtadumu fanywa wajinga,
kugeuzwa vijiko vya chipsi,
visoogopa mafuta makaa ya moto pia???

Hata lini sauti zenu zitaendelea kubanwa,
na kupwelea kwa kikohozi cha chaki?

Walimu ndiyo mshikao dira,
kuonyesha kule tuendako,
mabango imara yaelekezayo daima,
bila ushuru kutoza.
walimu ndiyo viongozi mahususi,
wa ujanja wote dunia nzima,
kiduchu kiduchi mwatusindilia,
wa elimu na teknolojia mlo nayo,
bila wivu hiana wala majivuno.

iweje walovilaza Werema pia Mwigulu,
kuwatusi ya nguoni?
Iweje Kikwete alo uzaowa DESSA,
kuwatishia nyau kucha paruza?

Mgomo wenu walimu,
nyonga ya CCM vipand vipande,
mmewatia ngeu kifo ki njiani,
na kuondoa kilanga chao,
Walimu pekee mwatosha,
kuifungisha vilago na machulupwete,
Dola mufslisi ya CCM.

CCM yawatumia kama Chupi,
Siri mwahifadhi heshima kwenu sifuri,
CCM yawatumia kama chambio,
mwaisafisha pee nyie mwanuka shonde,
CCM yawageuza shimo maji taka,
mahali pa kutolea uoza wake.
CCM yawaona nyie mbumbumbu hamnazo,
Ionyesheni Nyie ndo Walimu.

Zamu yenu hii sasa jamani,
itumieni vema kamwe msiipote,
waonyesheni CCM na vibaraka wao,
Nyie ni walimu na siku zote mwalimu hapuuzwi,
Nafasi yenu katika jamii,
yashinda ile ya dhahabu safi,
walimu muhimili katika jamii
Jiwe la pembeni kwa maendeleo ya taifa.
 
Ila wazee tuseme ukweli, hawa maafisa elimu wanawagonga sana walimu wa kike wageni, hata walio olewa tayari.
 
hawa wanataka kuf.ilwa...njoon kwangu na iyo fomu,mi nina kondom
 
Wazunguke tu cwanatfuta posho(night) ni kaufisadi kalikoendelea kuota mizizi kutoka juu. Hawawezi kutuambiakitu mi mwl wa mpwapwa vijijini kituoni kwangu hakuna umeme wala network nimekuja mjini nipate na updates za mgomo. This tym no retreating kabsaa we r sick n tired of these bloodsuckers.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
kikubw kuliko vyote waalimu wasing'ae kabisa kazini.ili tuone hizo fomu watampa nani azijaze kama watawapa wanfunzi hapo sawa waalimu endeleeni kukomaa maafisa elimu ni watu kama nyie wala sio miungu,ni kama wamesahau kwamba na wao walishawahi kuwa waalimu,
 
waheshimiwa walimu poleni,
kwa masahibu yote yalo wakuta,
nawaunga mkono kwa dhati,
endelezeni msimamo wenu,
hata ikibidi gomeni mpaka novemba 2015,
acheni fanywa bwegge na ccm,
kwa faida yao binafsi na wake zao.

...

masalia ya shabai robert na seifu khatibu wa miaka ya 1960s
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…