Tahadhari kwa madereva hasa mnaoendesha usiku

Tahadhari kwa madereva hasa mnaoendesha usiku

TAHADHARI!!

Kama unaendesha Gari mida ya Usiku, na ghafla ukaona Mayai (Eggs) yamerushwa na kupiga kwenye KiOO cha Gari yako cha mbele, tafadhali sana USISIMAME, Usiwashe WIPER na wala usimwage MAJI kwenye KIOO chako cha mbele, sababu Mayai na Maji hubadilika kuwa maziwa na kufanya kitendo hicho utazuia kabisa uwezo wako kuona MBELE kiasi cha kukulazimu kusimama na kusababisha KUVAMIWA na MAJAMBAZI. Na Majambazi wakishakuvamia sihitaji kukueleza nini kinatokeaga…. Mshtue mwanzako ni moja ya Mbinu zitumikazo na WEZI
Hahaahha POLISI wetu nawapenda bure...
 
Asante kwa taarifa hii maana kila siku wezi na mbinu mpya,mungu akubaliki sana
 
Wamiliki wa magari wanapitia kipindi kigumu sana katika nyakati hizi.....watu wengi bado wanajua kuwa mtu anayemiliki gari ni mtu hela nyingi sana....wakati kumbe ni mambo ya kawaida tu....hata wakivamia huwa hakuna cha maana wanachokikuta simu na sigara....
 
Back
Top Bottom