Tahadhari kwa single parents wote

Mtoto yeyote anatakiwa kufundishwa juu ya hatari ai madhara anaweza kutana nayo toka kwa strangers...na stranger anaweza kua ndugu wa karibu kabisa si lazima jirani rafiki au anybody else mtoto now mafunzo mapema awe na heshima kwa watu lakini awe vigilant na tabia zisizo sahihi zinapojitokeza..wengi ktk jamii kiafrika tunawafundisha Watoto kuwaogopa wakubwa na si kuwaheshimu kiasihata wakifanyiwa mabaya wanaogopa pia kusema Why? Kwa sababu wameshika neno kwamba mkubwa hasemwi ubaya...mtoa Mada you sawa ila nahisi ulilenga zaidi Maisha ya mamtoni so yes topic inafungua akili Sana, mfano ni Yule dogo alibaka mtoto wa dadake halafu akamnyonga mweh[emoji15]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inasikitisha sana,sasa huyo mtoto wamemkagua vizuri na vipimo vya hospital wamecheki lisije kuwa limempa na magonjwa ya hatari mtoto?

-Ndumilakuwili-
 
Sijawahi muamini mtu kwa kiasi hicho aisee. Mana dunia imegeuka sasa. Na hiyo ni moja ya tabia mbaya iliyokithiri.

Ahsante dada ake kwa uzi wenye kufundisha mana katika maisha yetu ya kawaida tulio wengi huwa hatuoni mbali mpaka yatukute.
 
kabla sijaandika mengi huyo jamaa bado anaishi?
 
Hii Inaashiria ujirani mwema kuisha maana siku vijitabia hivi vinafanywa na watu wa Karina sana tena ambao hudhanii kabisa yani

Hapa ninapoishi nina jirani yangu ni afisa jeshi la polisi,sasa nilitembelewa na mdogo wangu hivi majuzi tu kutoka kijijini kwetu

Walizoeana kama marafiki ukizingatia wote tulikuwa mabachala

Lakini mazoea yalipowakolea dogo akaanza kuona tofauti kutoka kwa yule afande dogo akaja akanitonya na hii ni kutokana na malezi tunayopewa huko vijijini ya ubabe mwingi na kutojishusha heshima (ukuryani)

Nikamtahadharisha dogo nae akaelewa sasa huku na huku jamaa akakomaa apakuliwe na dogo,dogo fasta akanitumia text nikavamia ndani kwake nilimkuta jamaa yupo uchi ameshika pesa kama elfu hamsini hivi ampe dogo ili asaidiwe shida yake asee nilichomfanya hatosahau kabisa na nilitaka kumpeleka kituoni kwake ila akabembelza sana maana huko angetimuliwa kazi

Ikabidi tuite mwenye nyumba akampa nots jamaa akahama pale now dogo karudi shule ila kashangaa sana tabia za mjini vijijini nadra sana ujinga huu

Htari sana miaka hii na sijui kwanini yani
 
Nakumbuka wakati nipo mdogo mshua aliwahi nipeleka pahali ni baada ya kumtembelea ila ilikuwa miaka ya nyuma kidogo

Ilikuwa ni Manzese hivi bila Shaka akanitembeza sehemu flani palikuwa na hao watu akawa ananionesha tu bila Kusem kitu
Kisha tukarudi Home akaniuliza nimejifunza nini
Nilipochelea kujibu akanijibu yeye sasa alinipa sifa mbaya za mashoga,tabia zao na athari zake,heshima yao mtaani,wanavyochukuliwa and so so.....

Lakini hadi likizo inaisha narudi kijijini kuendelea na shule nilikuwa sipendi sana kusikia habari hizo za hao watu hadi leo hii huwa nikkutana na shoga natamani kumpa makofi matatu mawili hivi

Juzi tu kuamkia jana hapa komakoma wapo wengi sana wanakibaa chao mkabala na bank ya nini sijui nimesahau ila ni jirani tu na masai klabu nilipita yakawa yanagombea mwanaume,sasa nikamkuta qchila yule msanii anayagombelezea sasa sina habari nashangaa nakoswa chupa asee afu nipo barabarani sina habari mi natembea

Dadeki walifunga mbona hicho kigrosari chao sijui hata yule msanii alipotelea wapi yaani nikaongeza chuki niliopandikizwa kwao na mshua miaka ile....

Kifupi malezi,msiogope kuongea na watoto wenu,wafanyeni marafiki lakini kikubwa hivi vizawadi kutoka kwa ma anco au maanti vipigeni marufuku kwa watoto wenu.

Nakumbuka mimi nilifundishwa kutokula kwa mtu au cha mtu,kutopokea cha mtu na hata nikipokea kama namheshimu sharti nikipeleke kwa mzazi Mama au baba na tulikuwa tukienda kinyume na maagizo tunachezea mbata sana so hadi Leo hii hata nikute wala nini Siwezi kukaa tule labda rafiki yangu kabisa tena yule wa moyoni namjua nje ndani.

Si mimi tu hata wadogo zangu wapo hivyo lakini huku utakuta mtoto anatembea na mama yake kila mtu anamnunulia anachokkitaka nawe unasema tu chukua mjomba kakunulia hiyo ni hatari sana

Au utakuta mtoto analilia chokoleti jirani anamchukua anaenda kumnunulia we unachekelea tu,chapa anyamaze na asillie vitu hovyo,hakuna kununuliwa na nani sijui

Malezi malezi ni muhimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…