Hivi karibuni vimeongezeka visa vingi vya uzembe, utovu wa nidhamu kazini, kunakofanywa na baadhi ya watendaji wa kata zilizopo Arusha.
KERO kuu ya kwanza kabisa, ni kuchelewa kufika ofisini bila sababu za msingi, jambo linalosababisha wananchi kushindwa kupata huduma kwa haraka na inavyopaswa.
KERO ya pili inahusu watendaji wa kata ambazo zipo pembezoni mwa miji, mfano kata ya Muriet na kata ya Terati, ambapo watendaji hawa wamegeuka kuwa madalali wa kuuza ardhi na viwanja. Hali hii imesababisha kutokuwepo kazini kwa muda sahihi na pia inachangia migogoro mikubwa ya ardhi.
Mara nyingi, watendaji wa mitaa haswa wa kata ya Terati muda wa kazi mara nyingi utawakuta mjini katika vijiwe vya madalali wakitafuta wateja wa kununua viwanja na mara kadhaa wamesababisha migogoro mikubwa sana ya ardhi.
Je serikali hufanya ufuatiliaji na kuhakiki ufanisi katika ofisi za watendaji zilizopo pembezoni mwa miji?? Mfano: yule anaevaa suti kila siku, hivi mtendaji wa kata na Mkurigenzi hua mnafatilia kwa karibu KERO za wananchi wenu na hii migogoro haswa ya ardhi inayosababishwa na ukanjanja wa watendaji dhaifu?
Rai yangu kwako mkurugenzi wa jiji PAMOJA na mkuu wa wilaya, hebu piteni mfanye ukaguzi na msikilize wananchi kwa sababu mpo hapo kuwatumikia wananchi.
Swala lingine ni uchafu uliokithiri kwenye baadhi ya maeneo mjini katikati. Kuna sehemu wamachinga wamerudi na ni sehemu hatarishi, kinachosikitisha ni wimbi la garage bubu pembezoni mwa barabara kuu, tena mjini katikati (kwa hili naomba Lobikoki ajitizame na ajitafakari kama anastahili hiyo nafasi).
Pia huko Muriet na Terati kuna madampo ya watu binafsi kwenye makazi ya watu, kwa kisingizio cha kurecycle chupa za plastics pamoja na vyuma chakavu. Haya maeneo ni machafu hatari, afya za wananchi zinahatarishwa na watendaji wapo wanaona (tetesi wanapewa mpunga) na bibi afya nao wapo.
Nakushauri mkurugenzi, haya madampo funga yote na yahamishiwe dampo kuu la jiji, mule ndani muwakodishie sehemu za kuchakata hayo mauchafu. Kwa kufanya hivyo mtaokoa afya za wananchi, mtaliongezea jiji mapato na pia mtadhibiti uchafu.
Haya ni kwa uchache sana.
Kataa watendaji dhaifu kwa ustawi wa jiji.
Kwa upendo mkubwa sana, habari hii iwafikie wizara ya Tamisemi, mkuu wa wilaya ( former tarafa) mh. Felician najua unafahamu Arusha vizuri, na ikufikie Mkurugenzi Chitukuro (wanangu wanakuitaga mzalendo)