Tahadhari kwa wanaoenda kumuaga Rais Magufuli

Tahadhari kwa wanaoenda kumuaga Rais Magufuli

Unategemea kuwa hai kwa miaka mingapi? Kuna maradhi zaidi ya 1000 duniani na yote yanaua.

Unajua ni kwa jinsi gani Malaria inateketeza ulimwengu au kwa vile vifo vya Malaria havirekodiwi?
Watu wangekuwa na mawazo kama yako kusinge kuwa na hospital watu wasinge hangaika kutafuta chanjo na dawa

Lakini hata Yesu asinge ponya wagonjwa
 
Wasalaam!

Wakati zoezi la kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg John Pombe Magufuli likiendelea mkoani Dar es Salaam ni vema kila anayepanga kwenda kutoa heshima za mwisho achukue tahadhari zifuatazo.

a) Jitahidi uvae barakoa. Inakupasa kufahamu ya kuwa unaenda kwenye msongamano mkubwa wa watu na ukweli ni kuwa gonjwa hatari la COVID-19 lipo. Hivyo, chukua tahadhari kwa kuvaa barakoa yako ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa ama kuwaambukiza wengine..

b) Kama una shinikizo la juu la damu na matatizo mengine ya upumuaji kama Athma, pumu, kifafa, basi nakushauri ubaki nyumbani. Kumuona marehemu amelala inaweza kukusababisha mshtuko na kuzirai. Na huenda ikakusabisha matatizo mengine zaidi. Vema ubakie tu nyumbani kufatilia kwenye luninga.

c) Hakuna sababu yeyote ya kumpeleka mtoto mdogo kwenye shughuli kama hiyo. Kwanza ni kwa ajili ya usalama wake. Hewa ni nzito, jua ni kali na hakuna mantiki yeyote ya kumuonesha marehemu. Taswira ya marehemu hubaki sana kwenye kumbukumbu zao na siyo afya kwa ukuaji wake. Mtoto anaweza pia kukupotea. Ikakusababishia usumbufu zaidi. Watoto wabaki nyumbani.

d) Vaa viatu vya kufunika uendapo huko. Usipendelee kuvaa Sandals. Kuvaa viatu inakupa nafasi ya kutembea kwa uangalifu. Sandals zinaweza kukatika na kusababisha utembee peku. Kwa kuwa watu ni wengi, mnapotembea ni rahisi sana sandals kukanyagwa na kusababisha usumbufu.

e) Tunza vitu vyako kwa umakini. Kuibiwa na kupoteza mali ni jambo la kawaida katika makutano ya watu wengi kiasi hicho. Inaweza kukuletea hasara inayoepukika. Usibebe vitu vyenye ncha kali au vifaa vya moto. Huenda usiwe na nia mbaya lakini ikakugharimu.

f) Fuata maelekezo yote utakayopewa na wana usalama na waongozaji. Njia gani ya kupita, tumia muda mchache kutoa heshima. Ikibidi isizidi sekunde 10. Kama ni ishara ya msalaba, ifanye ukiwa unatembea. Kuchukua muda inasabisha usumbufu na ucheleweshaji.

g) Umalizapo kuaga, rudi nyumbani haraka na kaendelee na majukumu mengine ili kuwapa wengine fursa ya kuaga.. Haina haja ya kuendelea kubaki uwanjani na maeneo jirani.

Mungu atusimamie.
JamiiForums1839644475.jpg
 
Watu wangekuwa na mawazo kama yako kusinge kuwa na hospital watu wasinge hangaika kutafuta chanjo na dawa

Lakini hata Yesu asinge ponya wagonjwa
Wanatafuta chanjo kwa sababu ya hospitali au kwa sababu ya watu?
 
Nashukuru umeandika andiko refu kidogo kuonesha msisitizo ila sitoungana nawe kamwe na hili la Corona wala si ujanja wa barakoa. Mataifa makubwa dunia yamekuwa wahanga wa huu ugonjwa zaidi ya mataifa masikini ambayo raia wake lazima watoke ili kupata riziki.

Hatuna barakoa wala hatuna tahadhari ya Corona zaidi ya US, China, UK, France wala Italy ila kikubwa cha kujivunia ni kuwa Afrika ina idadi ndogo ya wazee na miili ya Waafrika wengi inaweza kupambana na magonjwa.
Kwahiyo kwa sababu Africa in number ndogo ya wazee ndiyo waachwe wafe kwani kuna ugumu gani kuwapa wazee tahadhari
 
Wasalaam!

Wakati zoezi la kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg John Pombe Magufuli likiendelea mkoani Dar es Salaam ni vema kila anayepanga kwenda kutoa heshima za mwisho achukue tahadhari zifuatazo....
NARUDIJE GOBA HARAKA NIKITOKEA CHATO NA MFUKONI NINA LAKI MOJA. USHAURI WA KUTOKWENDA NA WATOTO WAKATI TAYARI MADHARA?
 
Mleta mada Barakoa uvae wewe uliye nyumbani sisi tulioko Chato hatutaki
 
Zidumu fikra za Magufuli
Tanzania hatutarudi nyuma mtumishi wake Mungu ametuacha na neno la wokovu
 
Natazama umati uliofurika hapa uwanja wa Chato msibani naona ni 5% tu ndio wamevaa barakoa hata....
Uzuri wa kauli za kuogofya Kama hizi hazijaanzia kwako wewe ni muendelezaji tuu, Bill Gate, WHO, Africa CDC, mbowe genge lake hadi bungeni walitoka lakini bado Tanzania tunaishi. Nakusihi chapa kazi Corona tunaishi nayo, nayo inatuheshimu
 
Kwahiyo unapenda uone kila eneo limetapakaa maiti za wafu wa Corona? Tusilazimishe kufa kwa Corona tuache mkono na Mungu uonekane juu yetu pia.
Umeniuliza ndugu zangu wangapi wamekufa nimekujibu zaidi 6,sasa unaniuliza napenda kuona maiti za wafu wa corona zimetapakaa?kwa misingi ipi?.
Yaani kuwaonya watu wachukue tahadhali ugonjwa upo na umeua hadi watu wangu wa karibu ni kupenda kuona watu wanakufa sio?.

Hivi nikimkuta rafiki yangu kalewa sana,hajitambui na ni usiku,ana gari anataka kurudi kwake,nikamshauri kuwa si busara kuendesha gari akiwa katika hali hiyo high-way,ni bora apaki atafute usafiri wa kumfikisha kwake,akanisikiliza.

Nitakuwa nimemsaidia au nataka kuona maiti yake akiwa amekufa?
 
Uzuri wa kauli za kuogofya Kama hizi hazijaanzia kwako wewe ni muendelezaji tuu, Bill Gate, WHO, Africa CDC, mbowe genge lake hadi bungeni walitoka lakini bado Tanzania tunaishi. Nakusihi chapa kazi Corona tunaishi nayo, nayo inatuheshimu
Kweli imewaheshimu sana,siku saba hizi imewaheshimisha mno,marais 10 wamefika nchini,watu 45 wameondoka uwanjani,ziara mikoa minne mikubwa,na kesho tukio kubwa sana la heshima linakuja.
 
Invigilator ungepata kufahamu walau kwa uchache kuhusu korona sidhani kama ungekuwa unashabikia barakoa.
Korona ni kitisho cha kiuchumu zaidi kuliko kiafya nitakupa mfano kidogo Kenya wanaanza curfew saa 3 usiku hadi asubui na hii ni kwa mujibu wa mikataba waliongia kwenye mikopo waliopewa jee hii kwenye akili yako inakupa picha gani. Magufuli angekuwa fisadi korona ingemnufaisha sana.
Jana Xi Jinping alikua na mkutano Shaoxing kwenye jimbo la zhejiang hapakuwa na barakoa wala social distance sababu wanaelewa mchezo nyuma corona hivyo ndugu yangu tusitishane zaidi chapa kazi na lipa Kodi yako kwa wakati mwezi unaisha huu
 
b) Kama una shinikizo la juu la damu na matatizo mengine ya upumuaji kama Athma, pumu, kifafa, basi nakushauri ubaki nyumbani. Kumuona marehemu amelala inaweza kukusababisha mshtuko na kuzirai
Childish
 
Back
Top Bottom