Tahadhari kwa wanaotaka kuingia kwenye biashara ya kilimo

Tahadhari kwa wanaotaka kuingia kwenye biashara ya kilimo

Wewe umetumia kilimo gani? Inaonyesha ulilima kienyeji pole lakini usikate tamaa
 
Naona watu wanamshambulia mtoa mada badala ya kuchanganua hoja aliyoitoa.Mimi naona hakuna alichokatisha tamaa...Ameongea vitu sahihi vinavyotokea kwenye sekta ya kilimo ili wale wanaotaka kuingia wajipange zaidi.

Nani asiyejua soko linavyosumbua,madalali,Serekali kukopa wakulima,bei mbovu ya mazao n.k...

Pia changamoto ya usimamizi...kudanganywa kuhusu mavuno na waliolima mwanzo...Utapeli n.k

Kwenye kuhifadhi mazao kuna kuoza,mazao kupungua ubora,wadudu n.k
Kifupi watu wengi wanapata hasara sana kwenye kilimo kuliko ukweli unavyosemwa...
 
aliyeandika huu uzi si mjasiriamali. Alikurupuka tu kwa kuiga akaangukia pua. Sasa anawashauri wenziwe ambao si wajasiriamlai wasikurupuke kama yeye. Ila wajasiriamli msisikilize ushauri wake. Nu ushauri kautoa kwa losers wenziwe wenye mitizamo hasi kama yeye. Hiyo ndo observation yangu
 
aliyeandika huu uzi si mjasiriamali. Alikurupuka tu kwa kuiga akaangukia pua. Sasa anawashauri wenziwe ambao si wajasiriamlai wasikurupuke kama yeye. Ila wajasiriamli msisikilize ushauri wake. Nu ushauri kautoa kwa losers wenziwe wenye mitizamo hasi kama yeye. Hiyo ndo observation yangu

Basi ana nia nzuri,au ulipendelea asishauri kabisa ili wengine wapite alikopita na 'kuangukia pua'?
 
Mtoa maada yupo sahihi, na ni mmoja wa watu ambao nafikiri wanapaswa kuigwa!

Nimesoma maelezi yake vizuri, na ametamka kuwa ni tahadhari kwa wageni wa kilimo, wasiingie kwa mkumbo ktk kilimo.

Kataja changamoto zilizopo ktk biashara ya kilimo, na hz changamoto sii za kisiasa, ni uhalisia, na katoa the way foward, kwamba vijana tusikurupuke tu, ukisikia eti ooh, heka moja ukilima mahindi unapata gunia 20, kuna mambo mengi yanatakiwa yazingatiwe kufanikiwa ktk kilimo(amesema mtoa maada).

Hakatishi tamaa, kasema ukweli, na ww kama mjasiriamali ni lazima uzijue kero hizo.
Ni rahisi kuikabili risk kama una taarifa nayo.
 
aliyeandika huu uzi si mjasiriamali. Alikurupuka tu kwa kuiga akaangukia pua. Sasa anawashauri wenziwe ambao si wajasiriamlai wasikurupuke kama yeye. Ila wajasiriamli msisikilize ushauri wake. Nu ushauri kautoa kwa losers wenziwe wenye mitizamo hasi kama yeye. Hiyo ndo observation yangu

Kwa mtu anaefahamu kutafuta pesa ni lazima katika wakati fulani awe loser, kupitia hasara na failure unakuwa stable, hata aliegundua Bulb alifail zaidi ya mara 1000
 
Wadau nimeamua kuweka habari hii kuwapa taadhari vijana wapya wanaotaka kujiingiza kwenye kilimo. Kuna usemi unaosema kwamba kupitia failure ndio kujifunza, huo usemi uko sahihi, lakini kupitia kwa aliefail kujifunza inasaidia sana. Mimi ni moja ya watu waliopata hasara kupitia kilimo.

Watu wengi wamekuwa wakidanganywa kwamba kwenye kilimo pesa iko nje nje, ni kweli kuna pesa nyingi lakini si rahisi kama watu wanavyodhani. Kwa bahati mbaya wakulima huwa hawasemi ukweli, unaweza kukutana na mkulima akakwambia kila mwaka analima ekali 10 za mahindi na anavuna gunia 150 hadi 200. Hivyo ukipiga bei kwa haraka haraka unaweza ukwamwambia nitafutie ekari 20 na mimi nilime ili nipate gunia 400.

Utakapo hamua kulima utakuta hali ni tofauti kabisa maana kuna changamoto zifuatazo ambazo ni lazima uzikabili:

1. Kwa sasa kuna tatizo kubwa la ukame, yaani unapanda mazao yako lakini mwisho wa siku yanakauka au yanakuwa hayana afya nzuri, hii usababisha mavuno kidogo. Kulima kwa kutegemea mvua ni mchezo wa kubahatisha

2. Wengi tumezoea kulima kienyeji, yaani hatupimi PH ya udongo, pia hatuweki mbolea.

3.Kuna changamoto kubwa kwa upande wa upandaji, wengi tunapanda lakini hatupandi kwa population inayotakiwa. Unaweka vibarua wapande, lakini space kati ya mmea na mmea inakuwa siyo sahihi. Hivyo unaweza kusema kuwa mwaka huu umelima ekari 40 lakini kwa uhalisia ni ekari 25 kwa sababu ya space kuwa kubwa.

4.Usimamizi. Kwa wale walioajiriwa hii ni changamoto kubwa sana, kilimo cha kupiga simu ni hatari. Mara nyingi msimamizi wako atakwambia mazao yako vizuri, lakini ukienda shambani unakuta ni tofauti kabisa, unaweza kupata presha. Pia unaweza kutuma pesa lakini isifike shambani, matokeo yake msimamizi anatumia kwa matumizi yake mwenyewe na kuwalipa vibarua akiwa amechelewa

5. Mavuno. Moja ya changamoto ya mkulima ni bei ya mazao, wakati wa mavuno mazao ushuka bei, hapa lazima utafute mahali pa kuhifadhi mazao yako hadi soko liwe imara.

NB: Uzi huu ni kwa ajili ya kukusaidia wewe usie na uzoefu ili usije ukakurupuka. Ili upate gunia 20 za mahindi kwa ekari moja ni lazima uwe umefanya intensive care ikiwemo kumwagilia, bahati mbaya mabwana shamba na wauza mbegu huwa wanadanganya wakulima kuhusu uzalishaji kwa ekari moja.


Mkuu uko SAHIHI Kabisa...mimi pia nilishalima nikapata hasara so ni vema kushare tulikosea wap na wengine wajifunze. Wanaokupinga nahisi ni roho mbaya walipata hasara sasa wanataka na wenzao wapate hasara.
 
Nilichokwambia, umetumia kushindwa kwako kutisha watu kuwa haiwezekani, swali ni je kweli haiwezekani au wewe ndo umeshindwa? Je walio weza wameweza vipi?, kwanini tutumie reference yako amabo ni dhaifu sana kuonyesha kuwa haiwezekani?

Ungeandika kuhusu kushindwa kwako kisha ukaomba ushauri, ukaonyeshwa ni wapi ulipokosea na nini ungefanya.
Biashara ya kilimo si ya kuingia kichwa kichwa, ni biashara inayotaka research, unalima nini ( Ubora wa mbegu, soko, unalima wapi (hali ya hewa), aina ya udogo, upatikanaji wa maji ya uhakika kwa ajili ya umwagiliaji na pia ubora wa maji. pia kuna uhifadhi wa mazao wakati unasubiri soko zuri ( high demand).

Mwisho, Kilimo ni Sayansi.

Mbona ulichoakiandika sasa hivi ndicho nilichosema? Mimi nimetoa tahadhari tu ili watu wawe makini, si wote wanajua hayo uliyoandika. Pia nimefail mara kadhaa kwenye kilimo, lakini pia nimefaidika kwa kujirekebisha, kupitia kilimo nimeweza kununua Trekta na kununua mashamba. Mimi nimewaambia vijana wasiojua ABC'S za kilimo wajifunze
 
Mkuu uko SAHIHI Kabisa...mimi pia nilishalima nikapata hasara so ni vema kushare tulikosea wap na wengine wajifunze. Wanaokupinga nahisi ni roho mbaya walipata hasara sasa wanataka na wenzao wapate hasara.

Tatizo kuna wanadamu wasiopenda kusikia negative sides, wanataka umdanganye kuwa kilimo ni rahisi kufanya ndio afurahi. Hapa sikatishi watu tamaa, ninachofanya ni kuwataka wadau watumie sayansi ya kisasa kwenye kilimo
 
Mleta mada umetoa ushauri mzuri; achana na huyo mpuuzi analeta matusi kwenye mada muhimu kama hii. Ushauri wako nimeukubali sana. In fact, hata tafiti nyingi zilizofanywa kuhusu changamoto za kilimo Africa zipo consistent na ushauri wako. Nashukuru kupata hii taarifa moja kwa moja kutoka kwa mkulima.
 
hizo za juu ni uzembe na kutokuwa na plan kwa unachofanya..
unapolima angalia njia kama irrigation..
pia kama unaona hauna muda ajiri mtu mtaalamu na apate motisha tatizo unamlipa kibarua 50000 atakufanyia Kazi nzuri kweli..?
kitu ambacho ni tatizo sugu katika kilimo ni soko na bei madalali wanakula bila jasho...
kwa mfano nimelima tikiti zimeshakomaa nilishapata soko ila kuna kamchezo wamecheza wanasema kuna pesa ya dalali 300 kila tunda!
 
Jamani alichokosea mtoa mada ki2 gani? Mnafikiri ushauri wake haujamsaidia hata mmoja wa waliosoma? Hata kama mtasema umewasaidia maloser wenzake poa 2. Ila alikua na nia njema 2
 
Hebu ondoka huko, unatuonyesha kushindwa kwako na jinsi gani ulivyo mpumbavu. Kwa maelezo yako ulifanya kilimo cha kizamani sana( Kilimo kwanza) alafu kwenye N.B unajifanya wewe unauzoefu unataka kuwasaidia wasio na uzoefu.

Kama hujui afadhali ungeuliza kwa kuomba ushauri, kwenye pont yako namba mbili inatosha kuonyesha ulivyo .........

Seems like unasumbuliwa na stress!!! Punguza jazba. Life is too short
 
Mleta mada umetoa ushauri mzuri; achana na huyo mpuuzi analeta matusi kwenye mada muhimu kama hii. Ushauri wako nimeukubali sana. In fact, hata tafiti nyingi zilizofanywa kuhusu changamoto za kilimo Africa zipo consistent na ushauri wako. Nashukuru kupata hii taarifa moja kwa moja kutoka kwa mkulima.

Huyo mpuuzi tumsamehe bure. Pengine anasumbuliwa na stress.. Si unajua tena maisha sa hivi ni vurugu tupu😀
 
Back
Top Bottom