Tahadhari kwa wanaotaka kuingia kwenye biashara ya kilimo

Wewe umetumia kilimo gani? Inaonyesha ulilima kienyeji pole lakini usikate tamaa
 
Naona watu wanamshambulia mtoa mada badala ya kuchanganua hoja aliyoitoa.Mimi naona hakuna alichokatisha tamaa...Ameongea vitu sahihi vinavyotokea kwenye sekta ya kilimo ili wale wanaotaka kuingia wajipange zaidi.

Nani asiyejua soko linavyosumbua,madalali,Serekali kukopa wakulima,bei mbovu ya mazao n.k...

Pia changamoto ya usimamizi...kudanganywa kuhusu mavuno na waliolima mwanzo...Utapeli n.k

Kwenye kuhifadhi mazao kuna kuoza,mazao kupungua ubora,wadudu n.k
Kifupi watu wengi wanapata hasara sana kwenye kilimo kuliko ukweli unavyosemwa...
 
aliyeandika huu uzi si mjasiriamali. Alikurupuka tu kwa kuiga akaangukia pua. Sasa anawashauri wenziwe ambao si wajasiriamlai wasikurupuke kama yeye. Ila wajasiriamli msisikilize ushauri wake. Nu ushauri kautoa kwa losers wenziwe wenye mitizamo hasi kama yeye. Hiyo ndo observation yangu
 

Basi ana nia nzuri,au ulipendelea asishauri kabisa ili wengine wapite alikopita na 'kuangukia pua'?
 
Mtoa maada yupo sahihi, na ni mmoja wa watu ambao nafikiri wanapaswa kuigwa!

Nimesoma maelezi yake vizuri, na ametamka kuwa ni tahadhari kwa wageni wa kilimo, wasiingie kwa mkumbo ktk kilimo.

Kataja changamoto zilizopo ktk biashara ya kilimo, na hz changamoto sii za kisiasa, ni uhalisia, na katoa the way foward, kwamba vijana tusikurupuke tu, ukisikia eti ooh, heka moja ukilima mahindi unapata gunia 20, kuna mambo mengi yanatakiwa yazingatiwe kufanikiwa ktk kilimo(amesema mtoa maada).

Hakatishi tamaa, kasema ukweli, na ww kama mjasiriamali ni lazima uzijue kero hizo.
Ni rahisi kuikabili risk kama una taarifa nayo.
 

Kwa mtu anaefahamu kutafuta pesa ni lazima katika wakati fulani awe loser, kupitia hasara na failure unakuwa stable, hata aliegundua Bulb alifail zaidi ya mara 1000
 


Mkuu uko SAHIHI Kabisa...mimi pia nilishalima nikapata hasara so ni vema kushare tulikosea wap na wengine wajifunze. Wanaokupinga nahisi ni roho mbaya walipata hasara sasa wanataka na wenzao wapate hasara.
 

Mbona ulichoakiandika sasa hivi ndicho nilichosema? Mimi nimetoa tahadhari tu ili watu wawe makini, si wote wanajua hayo uliyoandika. Pia nimefail mara kadhaa kwenye kilimo, lakini pia nimefaidika kwa kujirekebisha, kupitia kilimo nimeweza kununua Trekta na kununua mashamba. Mimi nimewaambia vijana wasiojua ABC'S za kilimo wajifunze
 
Mkuu uko SAHIHI Kabisa...mimi pia nilishalima nikapata hasara so ni vema kushare tulikosea wap na wengine wajifunze. Wanaokupinga nahisi ni roho mbaya walipata hasara sasa wanataka na wenzao wapate hasara.

Tatizo kuna wanadamu wasiopenda kusikia negative sides, wanataka umdanganye kuwa kilimo ni rahisi kufanya ndio afurahi. Hapa sikatishi watu tamaa, ninachofanya ni kuwataka wadau watumie sayansi ya kisasa kwenye kilimo
 
Kwenye ujasiliamali wowote kupata haaara ni jambo la kawaida,

Uko sahihi 100% kuna watu huwa wanajuta na kusema labda ningefanya biashara fulani ningepata faida, lakini kila biashara kuna watu waliopata hasara
 
Mleta mada umetoa ushauri mzuri; achana na huyo mpuuzi analeta matusi kwenye mada muhimu kama hii. Ushauri wako nimeukubali sana. In fact, hata tafiti nyingi zilizofanywa kuhusu changamoto za kilimo Africa zipo consistent na ushauri wako. Nashukuru kupata hii taarifa moja kwa moja kutoka kwa mkulima.
 
hizo za juu ni uzembe na kutokuwa na plan kwa unachofanya..
unapolima angalia njia kama irrigation..
pia kama unaona hauna muda ajiri mtu mtaalamu na apate motisha tatizo unamlipa kibarua 50000 atakufanyia Kazi nzuri kweli..?
kitu ambacho ni tatizo sugu katika kilimo ni soko na bei madalali wanakula bila jasho...
kwa mfano nimelima tikiti zimeshakomaa nilishapata soko ila kuna kamchezo wamecheza wanasema kuna pesa ya dalali 300 kila tunda!
 
Jamani alichokosea mtoa mada ki2 gani? Mnafikiri ushauri wake haujamsaidia hata mmoja wa waliosoma? Hata kama mtasema umewasaidia maloser wenzake poa 2. Ila alikua na nia njema 2
 

Seems like unasumbuliwa na stress!!! Punguza jazba. Life is too short
 

Huyo mpuuzi tumsamehe bure. Pengine anasumbuliwa na stress.. Si unajua tena maisha sa hivi ni vurugu tupu😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…