Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Ni muhimu kutambua kuwa sio kila mtu anayewashawishi watu kutoa sadaka ana nia njema. Biblia inasema nyakati za mwisho zitatokea roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani(1 Timotheo 4:1). Katika nyakati hizi, kuna watu wanaotumia jina la Yesu ili kuwashawishi watu kutoa sadaka kwa manufaa yao binafsi badala ya utukufu wa Mungu. Wanawaelekeza watu kutoa sadaka kwa ahadi ya kupata miujiza ya haraka au mafanikio ya kimaisha bila kuwafundisha kweli ya Neno la Mungu.
Ukweli ni kwamba watu hao wanakuwa wanaomba mchango ili wafanikishe mambo yao. Lakini kwakuwa wanajua wakisema wanaomba mchango hawatapewa, wanatumia neno "sadaka" ili mtoaji aone kana kwamba anamtolea Mungu.
Labda sasa unajiuliza: Mbona Maandiko yanasema tukiwapa watu vitu, na sisi tutapewa?
Ni kweli Biblia inatufundisha kuwa kutoa ni baraka, na Mungu huwalipa wale wanaotoa kwa moyo wa ukarimu. Lakini tukiwapa sadaka watu wanaotumia Jina la Mungu vibaya au kwa manufaa yao binafsi, ni sawa na kushiriki matendo yao ya udanganyifu(2 Yohana 1:10-11) Ni sawa na kuwasaidia kueneza zaidi uongo. Kwahiyo tukiwapa sadaka wadanganyifu(wanaovaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu) sadaka zetu zinaweza zisiwe na thamani mbele ya Mungu.
Hebu jiulize: Mbona watu wanatoa sana sadaka na kuahidiwa kwamba watapata magari, watapata nyumba, watapata mapesa; kwanini hawapati hayo wanayoahidiwa?
Tuchunguze sasa kwa ufupi, aina mbalimbali za sadaka zinazotajwa katika Biblia na madhumuni yake ili tunapotoa tutoe tukiwa na ufahamu sahihi. Vinginevyo kama tulivyoona, tunaweza kujikuta tumeingia katika kundi la “wajinga ndio waliwao.”
Katika Biblia, kuna aina mbalimbali za sadaka ambazo watu walimtolea Mungu. Hizi hapa ni baadhi ya aina za sadaka:
1. Sadaka ya Kuteketezwa
Hii ilikuwa sadaka iliyotolewa wakati wa Agano la Kale. Ilikuwa sadaka ya wanyama walioteketezwa kabisa kama ishara ya toba, kujisalimisha na kupata kibali kwake.
(Mambo ya Walawi 1:3-4)
2. Sadaka ya Mavuno
Hii ni sadaka ya mazao ya shambani kama unga, nafaka, au mkate, inayotolewa kama shukrani kwa Mungu (Mambo ya Walawi 2:1-2)
3. Sadaka ya Amani
Hii ni sadaka iliyotolewa kwa hiari ili kumshukuru Mungu kwa baraka zake.
(Mambo ya Walawi 3:1)
4. Sadaka ya Dhambi
Sadaka hii ilitolewa kwa ajili ya kufunika dhambi zilizotendwa bila kukusudia.
Mambo ya Walawi 4:2-3
"Semeni na wana wa Israeli, mkisema, mtu awaye yote atakapokosa, akafanya neno lo lote lisilopasa kufanywa, kwa amri za Bwana, ajapokuwa hakulifahamu... atamsongeza ng’ombe mume asiye na waa kwa ajili ya dhambi yake."
5. Sadaka ya Hatia
Ilitolewa kwa ajili ya dhambi zilizotendwa kwa makosa, hasa dhidi ya vitu vitakatifu au wanadamu. Mambo ya Walawi 5:15
"Mtu akifanya kosa, akatenda kwa kutokujua katika mambo matakatifu ya Bwana, ndipo ataleta kwa Bwana sadaka ya hatia."
6. Zaka au Kikumi
Hii ni sehemu ya kumi ya mapato ya mtu. Wakati wa Agano la Kale
Ilitolewa ili chakula kiwemo nyumbani mwa Mungu; ili Makuhani na Walawi waweze kufanya huduma. Wakati wa Agano Jipya zaka inatolewa kwa makusudi hayo pia lakini hasa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Yesu alisema chakula chake ni kazi ya Mungu.
7. Sadaka ya Hiari
Sadaka hii hutolewa Kanisani, kwa hiari, bila masharti, kama sehemu ya ibada au shukrani kwa Mungu au kwa lengo la kufanya kazi ya Mungu.
2 Wakorintho 9:7
"Kila mtu na atoe kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu." Mungu hupendezwa na sadaka zinazotolewa sawasawa na mapenzi yake.
Naamini mpaka hapo umetambua aina za sadaka, kama zilivyoandikwa katika Biblia, kitabu kinachotuongoza kufanya yatupasayo kufanya.
Kwahiyo mtu akikuambia utoe sadaka ambayo jina la sadaka hiyo halijaandikwa kwenye Biblia na madhumuni ya sadaka hiyo hayaendani na Maandiko, ni vizuri ujiulize kwanza mara mbilimbili. "Unamtolea Mungu au unatapeliwa?"
Kwa mfano, mtu akikuambia utoe sadaka ya ukombozi, shtuka! Katika Agano Jipya, Yesu alijitoa kuwa sadaka au dhabihu mara moja tu ili kutukomboa. Kwahiyo hakuna haja tena mtu kutoa sadaka ili akombolewe.
Ni aina gani nyingine ya sadaka, ulizowahi kusikia watu wakiambiwa watoe? Tutajie hapa majina ya sadaka hizo, na pia kama ulisikia mistari ya Biblia inayounga mkono sadaka hizo tutajie, tujiridhishe kama ndivyo ilivyo, tusije "tukaingizwa mjini."
Thank you!