Tahadhari kwa Watoaji wa Sadaka

Tahadhari kwa Watoaji wa Sadaka

Mifuko miwili ya cement iliyochanganywa na kokoto kidogo ikapigwa rangi we unaita ni mtakatifu?
Huyo jamaa anaonekana msomi. Mpaka apige magoti hapo, unafikiri hajui kwamba huyo ni mtakatifu. Halafu amekubali apigwe picha ya ukumbusho na magari yake mawili yamepaki pembeni.
 
Huyo jamaa anaonekana msomi. Mpaka apige magoti hapo, unafikiri hajui kwamba huyo ni mtakatifu. Halafu amekubali apigwe picha ya ukumbusho na magari yake mawili yamepaki pembeni.
Kipimo kinachoonyesha ni msomi mpumbavu ndo hicho kuomba toba mbele ya mifuko miwili ya cement
 
Pesa imesha kuwa ngumu bora nikabeti kuliko kumpa mwamposa
Uamuzi mzuri, lakini kubeti si ni sawa na kuruka majivu ukakanyaga makaa ya moto. Ungesema ukawekeze shambani ningekuunga mkono
 
Kipimo kinachoonyesha ni msomi mpumbavu ndo hicho kuomba toba mbele ya mifuko miwili ya cement
Ah, kanyaga pole pole, mkuu. Huyo amejifunza kutoka kwa wakuu wake wa dini. Wakuu wake wa dini kabla ya kuanza "utume" huwa wanasoma miaka mpaka tisa kwenye vyuo vikuu. Ukisema ni msomi mpumbavu unawatukana na wasomi waliomfundisha. Tafadhali bwana, acha maneno yako
 
Hujajiuliza kwanini Yesu hakutaja Acc number aliposema:
"...Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wezi hawavunji na kuiba. Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa."
Umefunga pm mkuu
 
Jambo la kuzingatia unapotoa zaka
Unapotoa zaka. Toa zaka kamili. Zaka ni sehemu ya kumi ya mapato ya mtu. Hivyo ukitoa zaka, toa 10%, siyo 9% au 5%.
Malaki 3:10 – "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi, mjue kwamba sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha."
Hii nayo haipo kwa sasa, ila inalazimishwa tuu, walawi walikuwa wakohudumu siku zote kwenye hekalu la Mungu, wanafunzi wa yesu walikuwa wanafanya kazi na wanahudumu na yesu, wachungaji wa sasa wanakomaa na zaka kwasababu ya uvivu wa kufanya kazi. Kwenye makanisa Kuna watenda kazi wengi, wazee wa kanisa, wanakwaya, viongozi wa vikindi, mashemasi n.k kama vipi wote wapewe zaka.
 
Ah, kanyaga pole pole, mkuu. Huyo amejifunza kutoka kwa wakuu wake wa dini. Wakuu wake wa dini kabla ya kuanza "utume" huwa wanasoma miaka mpaka tisa kwenye vyuo vikuu. Ukisema ni msomi mpumbavu unawatukana na wasomi waliomfundisha. Tafadhali bwana, acha maneno yako
Sawa Ntakuletea mifuko miwili ya cement na kokoto uwe unaiomba toba
 
Sawa Ntakuletea mifuko miwili ya cement na kokoto uwe unaiomba toba
Hiyo ni imani yake. Anao uhuru wa kuabudu. Kama una uhakika anakosea, badala ya kumcheka, msaidie kwa kumwandikia barua ya wazi(uzi maalum unaoelezea kwa kina hasara/madhara ya kuiomba ulinzi mifuko ya cement).

Mimi nimekuonyesha mfano. Badala ya kuweka picha za wanaotoa sadaka ya kujimaliza, nimewapa elimu wajue kuna matapeli wa kiroho. Tuko pamoja?
 
Ni muhimu kutambua kuwa sio kila mtu anayewashawishi watu kutoa sadaka ana nia njema. Biblia inasema nyakati za mwisho zitatokea roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani(1 Timotheo 4:1). Katika nyakati hizi, kuna watu wanaotumia jina la Yesu ili kuwashawishi watu kutoa sadaka kwa manufaa yao binafsi badala ya utukufu wa Mungu. Wanawaelekeza watu kutoa sadaka kwa ahadi ya kupata miujiza ya haraka au mafanikio ya kimaisha bila kuwafundisha kweli ya Neno la Mungu.

Ukweli ni kwamba watu hao wanakuwa wanaomba mchango ili wafanikishe mambo yao. Lakini kwakuwa wanajua wakisema wanaomba mchango hawatapewa, wanatumia neno "sadaka" ili mtoaji aone kana kwamba anamtolea Mungu.

Labda sasa unajiuliza: Mbona Maandiko yanasema tukiwapa watu vitu, na sisi tutapewa?
Ni kweli Biblia inatufundisha kuwa kutoa ni baraka, na Mungu huwalipa wale wanaotoa kwa moyo wa ukarimu. Lakini tukiwapa sadaka watu wanaotumia Jina la Mungu vibaya au kwa manufaa yao binafsi, ni sawa na kushiriki matendo yao ya udanganyifu(2 Yohana 1:10-11) Ni sawa na kuwasaidia kueneza zaidi uongo. Kwahiyo tukiwapa sadaka wadanganyifu(wanaovaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu) sadaka zetu zinaweza zisiwe na thamani mbele ya Mungu.

Hebu jiulize: Mbona watu wanatoa sana sadaka na kuahidiwa kwamba watapata magari, watapata nyumba, watapata mapesa; kwanini hawapati hayo wanayoahidiwa?

Tuchunguze sasa kwa ufupi, aina mbalimbali za sadaka zinazotajwa katika Biblia na madhumuni yake ili tunapotoa tutoe tukiwa na ufahamu sahihi. Vinginevyo kama tulivyoona, tunaweza kujikuta tumeingia katika kundi la “wajinga ndio waliwao.”

Katika Biblia, kuna aina mbalimbali za sadaka ambazo watu walimtolea Mungu. Hizi hapa ni baadhi ya aina za sadaka:
1. Sadaka ya Kuteketezwa
Hii ilikuwa sadaka iliyotolewa wakati wa Agano la Kale. Ilikuwa sadaka ya wanyama walioteketezwa kabisa kama ishara ya toba, kujisalimisha na kupata kibali kwake.
(Mambo ya Walawi 1:3-4)

2. Sadaka ya Mavuno
Hii ni sadaka ya mazao ya shambani kama unga, nafaka, au mkate, inayotolewa kama shukrani kwa Mungu (Mambo ya Walawi 2:1-2)

3. Sadaka ya Amani
Hii ni sadaka iliyotolewa kwa hiari ili kumshukuru Mungu kwa baraka zake.
(Mambo ya Walawi 3:1)

4. Sadaka ya Dhambi
Sadaka hii ilitolewa kwa ajili ya kufunika dhambi zilizotendwa bila kukusudia.
Mambo ya Walawi 4:2-3
"Semeni na wana wa Israeli, mkisema, mtu awaye yote atakapokosa, akafanya neno lo lote lisilopasa kufanywa, kwa amri za Bwana, ajapokuwa hakulifahamu... atamsongeza ng’ombe mume asiye na waa kwa ajili ya dhambi yake."

5. Sadaka ya Hatia
Ilitolewa kwa ajili ya dhambi zilizotendwa kwa makosa, hasa dhidi ya vitu vitakatifu au wanadamu. Mambo ya Walawi 5:15
"Mtu akifanya kosa, akatenda kwa kutokujua katika mambo matakatifu ya Bwana, ndipo ataleta kwa Bwana sadaka ya hatia."

6. Zaka au Kikumi
Hii ni sehemu ya kumi ya mapato ya mtu. Wakati wa Agano la Kale
Ilitolewa ili chakula kiwemo nyumbani mwa Mungu; ili Makuhani na Walawi waweze kufanya huduma. Wakati wa Agano Jipya zaka inatolewa kwa makusudi hayo pia lakini hasa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Yesu alisema chakula chake ni kazi ya Mungu.

7. Sadaka ya Hiari
Sadaka hii hutolewa Kanisani, kwa hiari, bila masharti, kama sehemu ya ibada au shukrani kwa Mungu au kwa lengo la kufanya kazi ya Mungu.
2 Wakorintho 9:7
"Kila mtu na atoe kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu." Mungu hupendezwa na sadaka zinazotolewa sawasawa na mapenzi yake.

Naamini mpaka hapo umetambua aina za sadaka, kama zilivyoandikwa katika Biblia, kitabu kinachotuongoza kufanya yatupasayo kufanya.

Kwahiyo mtu akikuambia utoe sadaka ambayo jina la sadaka hiyo halijaandikwa kwenye Biblia na madhumuni ya sadaka hiyo hayaendani na Maandiko, ni vizuri ujiulize kwanza mara mbilimbili. "Unamtolea Mungu au unatapeliwa?"

Kwa mfano, mtu akikuambia utoe sadaka ya ukombozi, shtuka! Katika Agano Jipya, Yesu alijitoa kuwa sadaka au dhabihu mara moja tu ili kutukomboa. Kwahiyo hakuna haja tena mtu kutoa sadaka ili akombolewe.

Ni aina gani nyingine ya sadaka, ulizowahi kusikia watu wakiambiwa watoe? Tutajie hapa majina ya sadaka hizo, na pia kama ulisikia mistari ya Biblia inayounga mkono sadaka hizo tutajie, tujiridhishe kama ndivyo ilivyo, tusije "tukaingizwa mjini."

Thank you!
Ni sahihi ulivyosema. Jambo lingine ni kwamba kuna wahubiri wenye maagano na shetani ukitoa sadaka kwenye huduma zao unakuwa umeungamanishwa na mafhabahu za giza na maisha yako yanakuwa kifungoni.
 
Ni sahihi ulivyosema. Jambo lingine ni kwamba kuna wahubiri wenye maagano na shetani ukitoa sadaka kwenye huduma zao unakuwa umeungamanishwa na mafhabahu za giza na maisha yako yanakuwa kifungoni.
Duh! Kweli watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Tuombe Mungu awafungue macho ya rohoni wasijiungamanishe na madhabahu za giza. Na tuzidi pia kuwafunulia Maandiko
 
Hii nayo haipo kwa sasa, ila inalazimishwa tuu,
Tukizingatia Andiko la Mathayo 23:23(NEN) bado ni sahihi kutoa zaka hata wakati huu wa Agano Jipya. Mstari huo unasema:

"Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnatoa zaka ya mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu zaidi ya sheria, yaani haki, huruma na uaminifu. Iliwapasa kufanya haya makuu ya sheria bila kupuuza hayo matoleo(zaka).

Wakati wa Agano la Kale watu walitoa zaka ili chakula kiwemo nyumbani mwa BWANA. Makuhani na Walawi wapate chakula ili waweze kufanya huduma.

Yesu alipokuja aliweka mkazo kwenye chakula cha kiroho(kazi ya Mungu)
Yohana 4:34 SRUV
"Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenituma, nikaimalize kazi yake."

Hivyo zaka inapaswa kutolewa hata wakati huu ili chakula alichosema Yesu kiwepo. Chakula hicho ni kuikamilisha kazi yake.
 
Back
Top Bottom