Tahadhari kwa Watoaji wa Sadaka

Thanks Madam for this elaboration.
 
Ni kweli Biblia inatufundisha kuwa kutoa ni baraka, na Mungu huwalipa wale wanaotoa kwa moyo wa ukarimu.
Kuna Bibi alinikamata somewhere akaniambia Mwanangu sijala toka Jana naomba unisaidie kiasi chochote nikapata kula, nikataka kugoma Bibi akaniambia nisaidie hela kidogo nikapate kula na Mungu anakuona atakubariki, hili neno likaniingia sana lakini bado nikataka kugoma, Bibi akanihimiza akaning'ang'ania mikono yangu huku machozi yakimlenga akasema tafadhari Mwanangu usinipite km unaona nataka hela kubwa basi nipe walau 200 tu Mungu anakuona atakuongezea, nikaona eeh isiwe tabu mboni sauti ya Mungu inasikika sana mahali hapa nikatoa hela nikampa nikaondoka, Mungu ananiona kweli hapa nilipo
 
Wekeni na acc number ya Mungu tuweke pesa
Kasaidie wenye huitaji mfano Walemavu, Vilema, Viwete, Wenye kupooza, Wenye mapooza, Yatima, Wagonjwa Mahututi hospitalini, Wajane, Wagane, Wazee, Waliokata tamaa ya kuishi, Wenye msongo wa Mawazo, Wenye njaa, Wenye kiu, nk

Hizo ndio Acc za Mungu huko kwa hao wengine wavaa Suti wanafanya Biashara ya Dini tu hakuna kingine, na kuna mmoja aliwahi kulisema Wazi hilo Serikali ikamfungia kanisa lake na TV yake ila baadae wakamfungulia TV aendelee kuhubiri ila mahubiri yake ni yaleyale anapiga vita hayo mambo ya Sadaka Sadaka
 
Wavivu wa kulima
 
Umeandika mambo mengi kuhusu sadaka, lakini katika zama hizi za agano jipya, namba saba pekee ndio sadaka sahihi (Toa sadaka kwa hiari), zingine zote ulizozitaja piga chini kwa sababu hazikuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…