TAHADHARI: Majambazi waunda Task force


kama haoni kuwa inafaa kuwataja sasa hivi ni sawa, ila kama ulivyo sema tuwape watoto wetu watu lele. Hapa halisi ametumia high level language kutuma ujumbe. Kwamba miongoni mwetu kunawatu wamevaa ngozi ya kondo ndio maana kuna upotoshaji mkubwa na wa maksudi taarifa mbali mbali.
 
hapa ngoma ndo inanoga sasa JF OYEEEEEEE!!!
 

Thanks for noting
 
Mkuu kwenye chako hamna kuogopa cha jambazi wala nini piga kelele tu....
 

Mkuu Halisi

Heshima mbele.

Hii habari yako ukiisoma kwa makini utagundua vitu viwili muhimu.

Kwanza kuna watu ndani ya jamiiforums.com wamepewa kazi ya kudukuza vyanzo vya maoni nikimaanisha wapi maoni yanayoingia ndani ya tovuti ya jamiiforums yanatoka.

Na pili, vyanzo hivyo ni nani wanaishi wapi na wanafanya nini.

Sasa mimi niliwahi kutoa maoni yangu kuhusu ni kwanini nilijiunga na jamii forums na kama kuna anaependa kurudia kusoma maoni hayo yanapatikana katika unganisho lifuatalo hapo chini:

https://www.jamiiforums.com/habari-...2-why-i-like-jamiiforums-my-thought-week.html

Anyway yote ni maisha yale ya kupigania haki ya yale ya kudhulumu haki na ili upatikane usawa ni lazima vitu hivi vitwangane na apatikane mshindi na lazima mshindi huyo awe mpigania haki.

Nikiwa huku ughaibuni kuna siku nilikutana na moja ya vyanzo vyangu vya habari ambae yeye yupo pale kwenye uwanja wa vita (Tanzania).

Ni very reliable na nnamwamini sana na akaniambia habari ambayo si tu ilinistua bali alinishangaza sana.

Jamaa akaniambia kwamba simu zote ziingiazo nchini Tanzania zinasikilizwa kupata habari ambazo pengine ni "credible" kwa wasikilizaji au kwa "fan" tu.

Mimi nikaelewa kwani mtindo huu ambao kwa kiingereza unaitwa eavesdropping ni ule ambao simu zinasikilizwa na hizo task forces na zikiishachujwa basi wale elements za resistance, magaidi, na wasumbufu wote katika jamii huwa wanafuatiliwa.

Eavesdropping inaweza kufanyika kupitia nyaya za simu au wiretapping, email, njia ya kutuma text kwenye simu au computer, na njia zingine za mawasiliano zinazochukuliwa kuwa ni private. "Eavesdropping" iikinoga inaweza kupelekea kufanya kitu kiitwacho kwa kiingereza snitching njia ambayo mkuu mwenzetu ameeleza ya task force ambapo watu wanatumika kutafuta watu wengine fulanifulani na kuwa-report kwa vyombo vya dola-hususan Police.

Sasa mambo haya hayakatazwi ila yanakiuka haki za msingi ambazo zimo hata kwenye katiba yetu ya pamoja na mengine haki ya kutoa maoni na haki ya kupata habari. Sasa je yamepitishwa na Bunge? au ndio kimefanyika kikao cha dharura na emergence laws zimepitishwa?
 
Last edited:
Wakuu mbona mna wasiwasi..hela za kampeni 2010 ndio zinakusanywa taratibu...kwa makisio zitahitajika kama Dola Milioni 100 na ushee...sio nyingi sana. Ndio zinakusanywa taratibu hivyo...msiwe na wasi utaratibu huu ni wa kawaida kama mtakumbukwa uchaguzi wa 2005 zilitoka moja kwa moja pale BoT ila kwa sasa pameshaonekana kuwa hapafai.
 
Hafi mtu. Ni lazima kieleweke. Ila tahadhari ni lazima tuchukue!!!!
 

Utasikiliza simu ngapi bongo. Wana set target na kufuatilia simu hizo tu.
 

Kwa hiyo wamekutuma wewe uje useme huku siyo? Basi waambie ujumbe umefika...
 
Ndio maana yule mrembo aliyejiunga siku za karibuni ananiuliza namba za simu na nani wamilikiwa JF
 
hao mafisadi tunasema sisi na hizo kesi wakishinda itakuwaje ?? yule anayemwita mtu fisadi wakati suala liko mahakani ni sawa na yule anayeita mwizi njiani anapoona watu wanaita mwizi
 
Wana JF kuna jambo lisilo la kawaida.Tumevamiwa.Jinsi mijadala inavyokwenda inaelekea kuna tatizo. Wasafisha mafisadi wamo humu na mashushu wamo humu.

Wamejizatiti kabisa kutuhujumu,kwa hiyo hatuna budi na sisi kuwa more articulate and smart katika kutoa hoja zetu.

Tukumbuke kwamba JF ipo kwa ajili ya kuinua maisha ya watu wetu.
 

Kama majungu vile??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…