Mkuu Halisi
Heshima mbele.
Hii habari yako ukiisoma kwa makini utagundua vitu viwili muhimu.
Kwanza kuna watu ndani ya jamiiforums.com wamepewa kazi ya kudukuza vyanzo vya maoni nikimaanisha wapi maoni yanayoingia ndani ya tovuti ya jamiiforums yanatoka.
Na pili, vyanzo hivyo ni nani wanaishi wapi na wanafanya nini.
Sasa mimi niliwahi kutoa maoni yangu kuhusu ni kwanini nilijiunga na jamii forums na kama kuna anaependa kurudia kusoma maoni hayo yanapatikana katika unganisho lifuatalo hapo chini:
https://www.jamiiforums.com/habari-...2-why-i-like-jamiiforums-my-thought-week.html
Anyway yote ni maisha yale ya kupigania haki ya yale ya kudhulumu haki na ili upatikane usawa ni lazima vitu hivi vitwangane na apatikane mshindi na lazima mshindi huyo awe mpigania haki.
Nikiwa huku ughaibuni kuna siku nilikutana na moja ya vyanzo vyangu vya habari ambae yeye yupo pale kwenye uwanja wa vita (Tanzania).
Ni
very reliable na nnamwamini sana na akaniambia habari ambayo si tu ilinistua bali alinishangaza sana.
Jamaa akaniambia kwamba simu zote ziingiazo nchini Tanzania zinasikilizwa kupata habari ambazo pengine ni
"credible" kwa wasikilizaji au kwa
"fan" tu.
Mimi nikaelewa kwani mtindo huu ambao kwa kiingereza unaitwa
eavesdropping ni ule ambao simu zinasikilizwa na hizo task forces na zikiishachujwa basi wale elements za resistance, magaidi, na wasumbufu wote katika jamii huwa wanafuatiliwa.
Eavesdropping inaweza kufanyika kupitia nyaya za simu au
wiretapping, email, njia ya kutuma text kwenye simu au computer, na njia zingine za mawasiliano zinazochukuliwa kuwa ni
private. "Eavesdropping" iikinoga inaweza kupelekea kufanya kitu kiitwacho kwa kiingereza
snitching njia ambayo mkuu mwenzetu ameeleza ya task force ambapo watu wanatumika kutafuta watu wengine fulanifulani na kuwa-report kwa vyombo vya dola-hususan
Police.
Sasa mambo haya hayakatazwi ila yanakiuka haki za msingi ambazo zimo hata kwenye katiba yetu ya pamoja na mengine haki ya kutoa maoni na haki ya kupata habari. Sasa je yamepitishwa na Bunge? au ndio kimefanyika kikao cha dharura na
emergence laws zimepitishwa?