Tahadhari na hospitali za private.....

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Nimekuwa natibiwa hospitali za private zinazosifika hapa nchini na kuaminika, nilichogundua juzi kimenishangaza mno.

wakati nasuburi kumuona daktari wakaja watu wawili wamependeza na wameshika mikoba as if ni watu wako na haraka hivi na wamekuja labda kufanya vipimo au kuwaona watu wanaowafahamu kwa dharura.....

Baada ya ku chat na mmojawapo ambaye ni mdada mrembo hivi, it turn out kumbe ni watu wa promosheni
za madawa,na hapo hospitali wamekuja fanya promosheni ya madawa yao.

kwa ufupi wenye makampuni yanayoingiza madawa na pharmacy kubwa kubwa wanafanya promosheni ya madawa mahosipitailini..hasa ya private... wanachokifanya ni kudeal na madokta tu,mwenye hospitali anaweza hata asijue.

wanawapa madokta kuanzia diary,t shirts,vikombe mpaka pesa nimeambiwa ili dokta awaandikie wagonjwa dawa fulani ambazo wenye maduka hayo wanazo.

yaani unaweza andikiwa dawa hata kama hiyo dawa si dawa kweli wataalamu wanaita placebos......unaingia gharama huku hujui unalipia placebos na sio dawa, na pia madawa ya kweli ambayo pengine mgonjwa hana ulazima wa kuyatumia....

Tahadharini jamani.
 
Hapo yapaswa mtu ukacheki sehemu tofauti tofauti!Ila hilo la kuandikiwa dawa hata kama sio mgonjwa halijaanza leo...na wala sio kwa private hosp tu!
 
bora za serikali mi naona...
 
bora za serikali mi naona...

Hao ndo maarufu wa kukwambia una malari tano kumbe huna!Tafuta daktari ambae utakua rafiki nae au hata rafiki wa rafiki ndo hawezi kukuliza!Bongo kila kitu kinahitaji ujanja!
 
Hao ndo maarufu wa kukwambia una malari tano kumbe huna!Tafuta daktari ambae utakua rafiki nae au hata rafiki wa rafiki ndo hawezi kukuliza!Bongo kila kitu kinahitaji ujanja!
that is what is needed here mamaaa!!
 
da!!, sijui tutaponea wapi kila mahali kuna uchakachuaji,,,watu hawathamini kabisa utu na afya ya mtu kilichobora kwa ni pesa tu..umakini unahitajika sana wakati wa matibabu iwe katika hosp za private au govmnts , manake hosp nyingi wanachojali na kupata pesa hata kwa matibabu ambayo siyo kabisa........muhimu wananchi tujitahidi kuzilinda afya zetu ili tusipatwe na maradhi mara kwa mara.....kwa wale wanaotoa matibabu kwa haki mungu azidi kuwabariki.......
 
ni kawaida kampuni za dawa kufanya promotion ma hospitalini .. usiogope mkuu
 
dactari hawezi kukuandikia dawa feki kisa kapewa tshit au pesa na watu wanaotangaza madawa yao, halafu hao watu huwa ni reliable kwani wanawakilisha makampuni ya dawa yanayoaminika
 
Hili swala la dawa niliwahi kugombana na dr fulani kisa nimekataa sawa yake aliyoniandikia hizi zipo sana
 
Kwa asilimia kubwa, mgonjwa hana control, au nguvu ya kukataa dawa anayopewa na daktari, unless awe na idea ya matibabu!

Lakini napenda kusema kuwa ni jambo la dhambi kubwa kama madaktari waliokula viapo vya uaminifu, uadilifu na usiri watatumika kuwalaghai wagonjwa, kwa ujira wa tshirt, au hata mamilioni ya fedha!
I personally term it as a Manslaughter!
 
dactari hawezi kukuandikia dawa feki kisa kapewa tshit au pesa na watu wanaotangaza madawa yao, halafu hao watu huwa ni reliable kwani wanawakilisha makampuni ya dawa yanayoaminika

wengi ni wakweli lakini wapo wanaopromote dawa feki, kuna hospitali za binafsi zinazuia kuandika dawa kwa majina ya biashara (trade names) na hata bima ya afya pia ukiandika dawa kwa trade name hawalipi, lengo lao ni hilo hilo kuzuia prescription ya dawa zisizo na ubora. Kwa hiyo kama unaenda hospitali mwambie daktrari tafadhali dawa unayonipa niandikie kwa generic name, kama ni paracetamol, akuandikie paracetamol sio sheladol, sijui panadol, huku ni kuwatangazia biashara wauza dawa. Akikuandikia kwa generic name utaondoa utata wa kupewa dawa ya biashara isiyo na ubora. Ukifika dukani muulize muuzaji kama hilo jina ni generic au trade ili uwe na uhakika. So msiache kwende hospitali lakini insist on generic prescription.
 
ASANTE SANA DR KAPOTOLO ,nimejifunza kuhusu GENERIC NAMES nilikuwa sifahamu hili.....ntakapoenda hosp ntasisitiza kuandikiwa dawa kwa generic prescription,,,,,asante sana.
 
Sio hilo tu kwa private hospital,kuna watu hufanyiwa operation za kutoa watoto(C/S) ili hospitali iingize fedha,kuweni macho na private hospital hasa za mijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…