DOKEZO Tahadhari: Pesa bandia za Tsh. 5,000 na 1,000 zimezagaa mtaani, tuwe makini

DOKEZO Tahadhari: Pesa bandia za Tsh. 5,000 na 1,000 zimezagaa mtaani, tuwe makini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Maskani tumekaa akapita muuza machungwa tukamuunganisha kimtindo, akaondoka kufika mbele akasimamishwa na jamaa wapo ndani ya IST wakachukua machungwa ya buku wakatoa teni, wakasepa chaap, kama utani jamaa akamwambia aisee jioni hii kaka kuwa makini na pesa unayopokea!...ashachelewa ashapigwa kitamboooo....
 
Hapa ndio umuhimu wa cashless economy unavyoonekana..

Au niko wrong wajuvi...
Kenya wamefanikiwa hili...sisi sijui tunafeli wap
Unaweza kaa kenya mwaka hujawahi shika hela... daladala unalipa kwa mpesa...mama ntilie, bodaboda, maduka yote nk.

Mungu jamani chukua Viongozi wote wazembe. Wanatufelisha sana. Kuanzia starlink, PayPal, mpesa, free wifi kwenye public spaces, BRT, SGR nk...ni uzembe tu na roho mbaya...

Halafu hawawazi shilling yetu inavyoporomoka hovyo...kutoka 2300 hadi 2800 na wako kimya na ukihoji unatekwa na kuuwawa
 
Back
Top Bottom