Tahadhari: Ugonjwa wa Mlipuko Huu unasumbua Madagascar

Tahadhari: Ugonjwa wa Mlipuko Huu unasumbua Madagascar

bowlibo

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2011
Posts
3,205
Reaction score
2,905
Ndugu wanajukwaa

Nimesoma kwenye gazeti la Mailonline kwamba kuna ugonjwa wa mlipuko umetokea Madagaskar na unaambukizwa kwa njia ya hewa, mate au kamasi na unaua ndani ya masaa 24.

Naomba kama kuna hatua zozote zimechukuliwa na serikali kutengeneza awareness kwetu mnifahamishe maana inasemekana kuna uwezekano wa ugonjwa kusambaa na kufika Tanzania pamoja na mataifa yanayopakana na nchi ya Madagaskar

SOURCE: World Bank releases $5m to tackle Madagascar plague | Daily Mail Online
 
ujue nipo kwenye mwendo kasi, yaani hapa na hizi habari zako ndo zimnivuruga sababu mbele yangu kuna lijamaa lina mafua hadi hali ya hewa imebadilika,
 
Ikiwa itabidi kuja basi ufikie magogoni, usimuache bali umpitie, na waliosimama na mibunduki wajue kuwa bunduki ni urembo tu wala sio ya kutumainiwa.
 
ujue nipo kwenye mwendo kasi, yaani hapa na hizi habari zako ndo zimnivuruga sababu mbele yangu kuna lijamaa lina mafua hadi hali ya hewa imebadilika,
Yeah, ni kweli maana wizara ya afya sijapata kusikia imetoa tahadhari gani kukabiliana na ugonjwa huu unaoathiri watu masikini.
 
Ikiwa itabidi kuja basi ufikie magogoni, usimuache bali umpitie, na waliosimama na mibunduki wajue kuwa bunduki ni urembo tu wala sio ya kutumainiwa.
hee, yaani afe kabisakabisa?
 
ndui si ile inachomwa begani na kuacha kovu la maisha au?
Moja ya chanjo za begani ndiyo hiyo, kama ulipata hiyo chanjo ugonjwa huu si rahisi kukupata, kwa sababu mwili wako unakuwa ushatengeneza kinga ya asili kukabiliana na ugonjwa huu.

Huko Madagascar inaonekana watu hawakupata hizi chanjo.

Ubaya ni kwamba ugonjwa huu ulionekana kama umetokomezwa kabisa kiasi watu wengine waliacha kupata hii chanjo na wanaweza kuupata.

Noma kichizi,halafu katikaehemu ambazonilikuwa natakakwenda kutalii Madagascar ni mojawapo. Ina wanyama na mimea ya pekee duniani.

Itabidi nisubiri upepo huu upite kwanza.
 
Daaaah! Kumbe black death au bubonic plague ndo ndui.

Nilikua sijui asee big up kwa kunifungua macho mkuu.
Ndiyo hiyo.

Baba Nyerere muhifadhi wetu tutamsema kwa mengi mabaya aliyoyafanya, ni haki yetu.

Lakini vitu vya msingi kama hivi aliviweka sawa enzi zile mara nyngine kuliko hata serikali zetu za sasa hizi.

Nachelea kunaweza kuwepo watu wengi wanaozaliwa miaka hii ya karibuni hawapati hizi chanjo ambazo zamani karibu kila mtu alipata.
 
Al-Watan nimepitia hiyo article ya The Economist, at least nimeshusha pressure baada ya kukuta kwamba inaweza kutibika
 
Ndiyo hiyo.

Baba Nyerere muhifadhi wetu tutamsema kwa mengi mabaya aliyoyafanya, ni haki yetu.

Lakini vitu vya msingi kamahivi aliviweka sawa enzi zile mara nyngine kuliko hata serikali zetu za sasa hizi.

Nachelea kunaweza kuwepo watu wengi wanaozaliwa miaka hii ya karibuni hawapati hizi chanjo ambazo zamani karibu kila mtu alipata.
umesema ukweli kabisa, Nyerere alifanya kitu katika mambo ya afya na elimu umenikumbusha usafiri bure, madaftari bure n.k.
 
Back
Top Bottom