Tahadhari - Vionjo vitamu vya uongo wanavyotoa wagombea wa CCM

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
WaTanzania kaeni chonjo na hotuba za viongozi na wagombea wa CCM,wasikilizeni tu,mkiondoka unakibusu kichinjio huku unajisemea CCM mtanitambua mwaka huu.Chakubanga anakusanya vyombo vya habari na kurusha tumbaku,uongo mtupu,ila jamaa anajua kupangilia kama una akili ya kizezeta unaona kasema kweli,ila kama mfuatiliaji wa mambo kwa kina unauona uongo wake nje nje,unabaki kucheka na kukumbuka stori za chakubanga.

Chakubanga anawaona waTanzania ni walewale waliopigania uhuru,sijui tumejenga reli,tumenunua ndege,reli ya kati itabeba kilo tatu haijulikani anasema nini yupo yupo tu anajipitisha aonekane anakitetea chama kumbe ndio mkubwa wa kukizamisha maana hoja zake zinajibiwa na hata mtoto mdogo,hivi mtoto mdogo akimuuliza hivi hapo zamani hamkuwa na ndege na treni sijui atamjibu nini zaidi ya kumwambia tumeboresha.

Tanzania ya Magufuli hakuna hata mtu mmoja asie lalamika kuwa hela imekimbia mfukoni,awaeleze wananchi watafanya nini ili hela kurejea,kuleta ndege mpya ? akili za wanaccm zote zimeganda,zipo palepale zinapiga maktaimu ,haziendi kulia wala kushoto kusonga mbele ndio kabisa haziwezi hapo hapo reli ndege meli,yaani mnatafuta ndege na meli wakati watu wapo kwenye tunnel tube au kitaalamu wanaziita hyperloop.
Nilitegemea mseme miaka mitano ijayo mtajenga hyperloop.
 
CCM mmechoka sana sana akili zenu zimeganda.
 
Mwaka huu tuwachinjie ccm baharini basi.
 
Chadema mnapapatika sana.endeleeni kutapatapa ila mjini mipango na kila mji unawenyeji.
Hamna limoti wala tv.kama ni chekechea mshaibiwa penseli,kichongeo na kifutio.
tema mate kulia fukia kushoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…