SoC01 Tahadhari: Wamasai hatarini kutolewa kwenye ardhi yao

SoC01 Tahadhari: Wamasai hatarini kutolewa kwenye ardhi yao

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 29, 2021
Posts
0
Reaction score
10
Na
Kasale Maleton Mwaana (Mwenyeji wa Ngorongoro)

NINI KIFANYIKE KUBORESHA UHIFADHI NA MAISHA YA WENYEJI!?

Mamlaka ya hifadhi kwa kusaidiana na wizara ya maliasili na utalii pamoja na serikali kwa ujumla, waruhusu kilimo cha kujikimu kwa wenyeji katika maeneo husika ili kupunguza janga la njaa na umaskini kwa wenyeji.

Serikali wahakikishe wanawapa watu Uhuru wa kumiliki ardhi na kijenga makazi ya kudumu katika ardhi yao. Hivyo watu waruhusiwe kuingiza vifaa vya ujenzi ili kubadilisha makazi kwa kujenga nyumba Bora zisizotumia miti kwa asilimia kubwa Kama nyumba za kienyeji, kwani zinaathari kwa mazingira ( haya ni miongoni mwa makosa yaliyofanywa na wahifadhi kuwanyima watu kujenga nyumba za kudumu Kama za tofali n.k.)

Serikali iboreshe huduma za kijamii Kama elimu na afya na maji kwa kujenga shule nyingi za msingi, sekondari na vyuo, kujenga vituo vingi vya Afya na hospitali, kutafuta vyanzo vingi vya maji , kuwaelimisha watu juu ya namna ya kuepukana na magonjwa , na kuwaelimisha juu ya ujasiriamali na shughuli nyingine za kiuchumi mbali na ufugaji .

Serikali, wizara ya maliasili na utalii na Mamlaka ya hifadhi kupitia idara yake ya maendeleo ya jamii, wahakikishe kuwa wenyeji wanafaidika na kile kitokanacho na utalii, kwa kutoa upendeleo wa pekee wa ajira kwa wenyeji, angalau asilimia 30 ili kupunguza umaskini na kuongeza uhusiano mwema Kati ya wenyeji na uhifadhi.

Pia watoe elimu juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, kutumia nishati mbadala na ambayo ni rafiki kwa mazingira ( Environmental friendly and renewable sources of energy), na namna ya kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira .

Serikali waboreshe miundombinu ya Barabara, masoko na kutengeneza mazingira rafiki ili wenyeji waweze kushiriki ipasavyo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Zoezi hili liende sambamba na kuwaelimisha vijana na akina mama juu ya ujasiriamali, na kutengeneza fursa na mazingira wezeshi ili waweze kuwekeza katika maeneo yao na kuepuka kwenda kuzurura mijini na nchi jirani hivyo kuhatarisha maisha yao.Hii pia huwasaidia kuondokana na umaskini na kushiriki katika shughuli nyingine za kiuchumi mbali na ufugaji.

Wafugaji waruhusiwe kuingiza mifugo katika maeneo yenye vyanzo vya maji na majani ya kutosha kwa mifugo wakati wa kiangazi Kama Oldupai na misitu ya Ngorongoro ( Entim oolturot), kwani maeneo hayo ni kimbilio la wenyeji hasa wakati wa kiangazi ambapo Kuna shida ya maji na kukosekana kwa malisho ya Ng'ombe, na Hakuna ushahidi kwamba mifugo wanaharibu maeneo hayo.

Pia tunaomba serikali waruhusu watu kupeleka mifugo katika kreta ya Ngorongoro ili kupata maji yenye madini muhimu kwa afya ya mifugo. Jambo hili linaweza kufanywa periodically ( atleast twice a month) kwa miezi ya desember Hadi june.

Mamlaka ya hifadhi, wizara ya maliasili na utalii na serikali kwa ujumla waturudishie baraza letu la wafugaji Ngorongoro ( NPC), kwani chombo hicho ilikuwa ni daraja muhimu kati ya Mamlaka na wenyeji na uhifadhi kwa ujumla. Ni chombo ambacho wananchi hutumia katika kupasa sauti yao kwamba mambo yanayohusu uhifadhi na maisha ya wenyeji.

Mabadiliko ya tabia ya nchi, hali ya hewa, maendeleo ya teknolojia na sayansi, mabadiliko ya kiutamaduni na utandawazi, maendeleo ya kiuchumi kijamii na kisiasa n.k. hayazuiliki kutokea kwa wakati tuliopo na huweza kuwa na athari chanya au hasi katika uhifadhi na jamii kwa ujumla. Athari hasi zinapotokea, serikali, Mamlaka ya hifadhi na wenyeji washirikiane kwa pamoja kukabiliana na athari hizo, na sio Mamlaka au serikali kufanya maamuzi yasiyoshirikishi kwa jamii, na hivyo kuja na matokeo ambayo Mara nyingi huelekezwa kuwaumiza wenyeji

Serikali wahakikishe wanawapa watu Uhuru wa kumiliki ardhi na kijenga makazi ya kudumu katika ardhi yao. Hivyo watu waruhusiwe kuingiza vifaa vya ujenzi ili kubadilisha makazi kwa kujenga nyumba Bora zisizotumia miti kwa asilimia kubwa Kama nyumba za kienyeji, kwani zinaathari kwa mazingira ( haya ni miongoni mwa makosa yaliyofanywa na wahifadhi kuwanyima watu kujenga nyumba za kudumu Kama za tofali n.k.)

Serikali iboreshe huduma za kijamii Kama elimu na afya na maji kwa kujenga shule nyingi za msingi, sekondari na vyuo, kujenga vituo vingi vya Afya na hospitali, kutafuta vyanzo vingi vya maji , kuwaelimisha watu juu ya namna ya kuepukana na magonjwa , na kuwaelimisha juu ya ujasiriamali na shughuli nyingine za kiuchumi mbali na ufugaji.

Serikali, wizara ya maliasili na utalii na Mamlaka ya hifadhi kupitia idara yake ya maendeleo ya jamii, wahakikishe kuwa wenyeji wanafaidika na kile kitokanacho na utalii, kwa kutoa upendeleo wa pekee wa ajira kwa wenyeji, angalau asilimia 30 ili kupunguza umaskini na kuongeza uhusiano mwema Kati ya wenyeji na uhifadhi.

Pia watoe elimu juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, kutumia nishati mbadala na ambayo ni rafiki kwa mazingira ( Environmental friendly and renewable sources of energy), na namna ya kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira .

Serikali waboreshe miundombinu ya Barabara, masoko na kutengeneza mazingira rafiki ili wenyeji waweze kushiriki ipasavyo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Zoezi hili liende sambamba na kuwaelimisha vijana na akina mama juu ya ujasiriamali, na kutengeneza fursa na mazingira wezeshi ili waweze kuwekeza katika maeneo yao na kuepuka kwenda kuzurura mijini na nchi jirani hivyo kuhatarisha maisha yao.Hii pia huwasaidia kuondokana na umaskini na kushiriki katika shughuli nyingine za kiuchumi mbali na ufugaji.

Wafugaji waruhusiwe kuingiza mifugo katika maeneo yenye vyanzo vya maji na majani ya kutosha kwa mifugo wakati wa kiangazi Kama Oldupai na misitu ya Ngorongoro ( Entim oolturot), kwani maeneo hayo ni kimbilio la wenyeji hasa wakati wa kiangazi ambapo Kuna shida ya maji na kukosekana kwa malisho ya Ng'ombe, na Hakuna ushahidi kwamba mifugo wanaharibu maeneo hayo.

Pia tunaomba serikali waruhusu watu kupeleka mifugo katika kreta ya Ngorongoro ili kupata maji yenye madini muhimu kwa afya ya mifugo. Jambo hili linaweza kufanywa periodically ( atleast twice a month) kwa miezi ya desember Hadi june.

Mamlaka ya hifadhi, wizara ya maliasili na utalii na serikali kwa ujumla waturudishie baraza letu la wafugaji Ngorongoro ( NPC), kwani chombo hicho ilikuwa ni daraja muhimu kati ya Mamlaka na wenyeji na uhifadhi kwa ujumla. Ni chombo ambacho wananchi hutumia katika kupasa sauti yao kwamba mambo yanayohusu uhifadhi na maisha ya wenyeji.

Mabadiliko ya tabia ya nchi, hali ya hewa, maendeleo ya teknolojia na sayansi, mabadiliko ya kiutamaduni na utandawazi, maendeleo ya kiuchumi kijamii na kisiasa n.k. hayazuiliki kutokea kwa wakati tuliopo na huweza kuwa na athari chanya au hasi katika uhifadhi na jamii kwa ujumla. Athari hasi zinapotokea, serikali, Mamlaka ya hifadhi na wenyeji washirikiane kwa pamoja kukabiliana na athari hizo, na sio Mamlaka au serikali kufanya maamuzi yasiyoshirikishi kwa jamii, na hivyo kuja na matokeo ambayo Mara nyingi huelekezwa kuwaumiza wenyeji.

Kasale Maleton Mwaana
The Son of the Land.
 
Upvote 2
Uliyoandika ni sahihi kabisa kwa upande wa jamii ya wamaasai lakini kwa upande hifadhi linaondoa maana ya uhifadhi. Tujiulize je tunataka tuwe na hifadhi endelevu(ngorongoro)?

Nadhani tunahitaji ngorongoro endelevu kwa umuhimu wake kimazingira na kiuchumi ukizingatia wamaamasi wanaweza kuhama lakini ila jamii ya viumbe(biodiversity)tutaipeleka wapi au ikipotea tutaipata wapi?, Wenzetu wanatamani wangepata maeneo ya asili Kama haya wanayatamani sisi tunayachezea.

Lazima tukubali kuongeza nguvu kwenye kupunguza na kudhibiti idadi ya watu kwenye hifadhi ili kuboresha jamii ya viumbe
 
Okay, ahsante kwa maoni yako, lakini kumbuka imeandikwa, enendeni mkaongezeke mkaijaze dunia, na kutawala vyote vilivyomo! Je, wewe waona wanadamu wateseke ili wanyama waishi!?

Kwamba wanyama wawe na ubora kuliko binadamu!? Kwamba hifadhi itakuwa endelevu endapo binadamu watateseka!?

Lakini zaidi, Kama ukisoma vizuri, tulipoteza ardhi Mara mbili, we lost Serengeti, we lost Ngorongoro creater, then unataka tupoteze Tena Ngorongoro higher lands!? Tuende wapi Sasa!?

Karibu, waweza kuwa na maoni mazuri zaidi
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Okay, ahsante kwa maoni yako, lakini kumbuka imeandikwa, enendeni mkaongezeke mkaijaze dunia, na kutawala vyote vilivyomo! Je, wewe waona wanadamu wateseke ili wanyama waishi!? Kwamba wanyama wawe na ubora kuliko binadamu!? Kwamba hifadhi itakuwa endelevu endapo binadamu watateseka!?
Lakini zaidi, Kama ukisoma vizuri, tulipoteza ardhi Mara mbili, we lost Serengeti, we lost Ngorongoro creater, then unataka tupoteze Tena Ngorongoro higher lands!? Tuende wapi Sasa!?
Karibu, waweza kuwa na maoni mazuri zaidi
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Kutokana na Imani yako hiyo ndio maana Mungu alimuumba mwanadamu kwa kumuongeza utashi na uelewa kitu ambacho viumbe wengine hawana. Kwenye biblia kitabu Cha MWANZO 2:15 mwanadamu alikabidhiwa dunia ailinde na aitunze kwamba alikua anajua kabisa katika kuzaliana huko kutaleta uharibifu.
Kuhusu suala la kunyang'anywa ardhi sio sahihi Tanzania bado tuna eneo kubwa ambalo halijatumika na ukizingatia asili ya mmasai ni kuhama na mifugo yake mi nadhani ni suala jema tu kuhifadhi maeneo kama ngorongo creater na Serengeti kutokana na umuhimu wake kihistoria,kiuchumi, kimazingira na hata kijamii
 
Ndugu mwandishi kabla hata sijaanza kusoma andiko lako, naomba nitoe maoni kuhusu haya maneno yako kwamba Wamasai hatarini kutolewa kwenye ardhi yao. Naomba nikusahihishe kuwa wamasai hawana ardhi katika nchi hii. Ardhi yote ni mali ya serikali na ndio wanaopanga matumizi sahihi ya ardhi hii kwa uendelevu pasipo kujali kabila la mtu. Sasa unaposema wamasai wananyanganywa ardhi yao unamaanisha nini? Ardhi hiyo walizaliwa nayo au walishuka nayo kutoka mbinguni?
 
Kwani serikali ilishuka nayo kutoka mbinguni?? Serikali Ni Nani kwanza na iko kwa ajili ya Nani!? Nikiondoa neno Masai land nikaweka sukuma land, hakuna ardhi ya usukumani? Na wasukuma sio wananchi! Specifications Ni kukudokeza aina ya watu wanaoishi eneo husika la nchi na Sio kwamba eneo sio la serikali!!

Be serious! Be kind and maintain a sense of humanity!!
Key points to note!
~wamasai wa Ngorongoro hawaruhusiwi kulima, hivyo janga la njaa linawakumba kwa miongo kadhaa Sasa
~wamasai wa Ngorongoro hawaruhusiwi kujenga makazi ya kudumu ( mf. nyumba za block n.k.) hivyo poor life standard ! Sio kwamba hawana uwezo kama watanzania wengine? Lahaula Ni wanakatazwa!

~kupeleka huduma za kijamii Ngorongoro Kama vile shule, zahanati, hospital n.k., inahitaji kibali Cha NCAA na wizara ya maliasili na utalii, Mara nyingi wamekuwa wakinyimwa hivyo, kiuhalisia, huduma za kijamii kule ni ndogo Sana!

Sasa, hayo Ni maisha ya watu hao kwa miaka 60+ Sasa tokea watolewe Serengeti 1959!!
Sasa nikuulize ndugu, unaposema ardhi Ni ya serikali nakubali, je, wewe ulipo huna makazi Bora au huna uhakika wa chakula kwa sababu ardhi Ni ya serikali!!?
Wewe umewahi kuhamishwa na serikali Mara kadhaa Kama wanangorongoro walivyotolewa kutoka moru( Serengeti) wakahamishiwa Ngorongoro wakaahidiwa kwamba Ngorongoro itakuwa ardhi Yao milele ( mkataba upo), lakini mwaka 1974 wakatolewa katika bonde la hifadhi ya Ngorongoro Tena kwa ajili ya uhifadhi)!! Wakitolewa Sasa Tena maana yake Ni hamisho la tatu!! Is that humanity!? Uhifadhi unaotegemea kutesa watu hivyo!?

Maumivu ya kundi la watu yanaweza yasikuguse mpaka uwe umepata matatizo sawa na wao ndio utajua kweli watu wanateseka!!
 
Mkuu nimekupigia kura maana naona ulikiwa na 0 yaani hata ids zako zimeshindwa kukupigia
 
Back
Top Bottom