Tahadhari Wanunuaji wa Hisa, Hati fungani na Uwekezaji DSE!

Tahadhari Wanunuaji wa Hisa, Hati fungani na Uwekezaji DSE!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
hivi karibuni matapeli wa kimaraifa wameingia sokol la hisa la dar es salaam , wanakuja na kama ka advert kwenye insta, huwezi ona hiyo account, inakuwa ni advert tu , ukiingia huko umetapeliwa na kudukuliwa.
Wanajifanya wanakufundusha lakini ni utapeli mtupu.

Kama wewe unataka kujifunza na kuwekeza, nenda kwenye page za kina Mwalimu Emilian busara, Victor Busara, WArda, Edmund Muyagi, CFO Madam Kessy na wengine wana namba zao, sura unaziona , ukipiga na ukitaka appoinment wanakuja ofisini kwako ama unaenda kwao.

Kabla ya kuwekeza katika hisa zinazouzwa kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), epuka kujiunga na makundi ya WhatsApp yanayotangazwa kupitia Instagram, Facebook au mitandao mingine ya kijamii yakiahidi faida kubwa kwa muda mfupi.

Mara nyingi matangazo hayo hayatoi utambulisho wa wahusika, hayana namba za simu zinazoweza kuthibitishwa, wala hayaonyeshi walipo au taasisi wanazowakilisha. Baadhi yao hutumia majina na picha za wataalamu au taasisi bila idhini ili kuwashawishi watu kutuma fedha.

Kumbuka:

  • Hakuna uwekezaji halali unaohakikisha faida kubwa kwa haraka bila hatari.
  • Thibitisha kila taarifa kupitia taasisi zilizoidhinishwa kabla ya kuwekeza.
  • Usitume fedha kwa watu au makundi usiyoyafahamu kwa ahadi za "returns" za haraka.
Linda mtaji wako. Fanya uwekezaji kwa taarifa sahihi, si kwa ahadi zisizoweza kuthibitishwa.
 
Back
Top Bottom