TAHADHARI: wimbi la wizi wa Mtandaoni kutumia simu

TAHADHARI: wimbi la wizi wa Mtandaoni kutumia simu

MAMESHO

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
1,432
Reaction score
1,738
habari za leo. Nawataarifu kuwa kuna wezi wanazunguka kwenye vituo mbalimbali wakidanganya watu kuwa wanawarekebishia vifurushi vilivyotajwa na Mh Raisi. Wana swap simcars kuchykua taarifa za akaunti za benki na za mitandao ya simu na kuiba fedha.
na kama huna fedha wanakopa kutumia salary advance na kuhamisha fedha. Kuweni makini kutowapa watu simu zenu wala kutaka kurekebishiwa kupewa vifurushi vya bei rahisi. Pia wanakwambia fanya transaction yoyote au nunua kifurushi au salio. Hapo ndio wanadaka namba zako za siri.Watu hawa wanafaa nguo za timu za mauzo za mitandao ya simu. Ukiona watu hawa kuweni makini sana. Wanatembea mashule, mahospitali, na maeneo Mengi sana. Pia kama akaunti yako ya simu ina password inayofanana na huduma za kipesa za akaunti yako badilisha zitofautiane. Pia usihifadhi taarifa za kutoa au kupokea fedha kwenye simu yako.
 
Back
Top Bottom