Tahadhari ya Ebola: Kuna Jamii Zinazokula Nyani au Jamii ya Nyani na Popo Tanzania

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2006
Posts
1,838
Reaction score
705
Wanajamvi, tunaambiwa kuwa chanzo cha ugonjwa wa Ebola ni muingiliano wa binadamu na wanyama wanaobeba virusi vya ugonjwa huo, hasa kwa kula nyama ya nyani na aina fulani ya popo. Mimi binafsi haya maelezo nayatilia shaka kwa sababu ndiyo hayo hayo yaliyotolewa kuhusu virusi vya UKIMWI. Lakini inawezekana yakawa na kiasi fulani cha ukweli. Swali langu ni je, kuna jamii hapa Tanzania zinazokula nyama ya nyani na popo ambazo zinaweza kuwa chanzo cha virusi hivyo kuhamia kwa binadamu? Kama zipo kuna tahadhari yoyote ambayo imeishachukuliwa kujiridhisha kuwa wanyama hao hawana hivyo virusi? Je, wanasayansi wetu (madaktari na watfiti) wa hapa Tanzania wameishafanya kazi zozote kuhusiana na virusi hivi au ndiyo wanangoja wazungu wafanye na wao waje ku-copy na ku-paste? :embarrassed::embarrassed:
 

Well said! Tanzania researchers need doing something as part of scientific community, at least do what is within our reach. We should not be spectators! Costech need to invite concept notes on ebola virus research or call workshop for lead Tanzanian researchers to deliberate the way forward on Ebola virus research on all fronts from basic and social researchers
 
Madaktari na wanasayansi wa Bongo mko wapi? Mimi hapa naona fursa ya mtu kupata Ph.D au u-profesa kwa kuongeza maarifa kuhusu hivi virusi na ugonjwa wa Ebola. Au na nyinyi bado mnaamini katika uchawi au kumtupia mzigo mwenyezi Mungu (mapenzi ya Mungu)?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…