Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 705
Wanajamvi, tunaambiwa kuwa chanzo cha ugonjwa wa Ebola ni muingiliano wa binadamu na wanyama wanaobeba virusi vya ugonjwa huo, hasa kwa kula nyama ya nyani na aina fulani ya popo. Mimi binafsi haya maelezo nayatilia shaka kwa sababu ndiyo hayo hayo yaliyotolewa kuhusu virusi vya UKIMWI. Lakini inawezekana yakawa na kiasi fulani cha ukweli. Swali langu ni je, kuna jamii hapa Tanzania zinazokula nyama ya nyani na popo ambazo zinaweza kuwa chanzo cha virusi hivyo kuhamia kwa binadamu? Kama zipo kuna tahadhari yoyote ambayo imeishachukuliwa kujiridhisha kuwa wanyama hao hawana hivyo virusi? Je, wanasayansi wetu (madaktari na watfiti) wa hapa Tanzania wameishafanya kazi zozote kuhusiana na virusi hivi au ndiyo wanangoja wazungu wafanye na wao waje ku-copy na ku-paste? :embarrassed::embarrassed: