Tahadhari ya Kuvunjika Muungano wa Tanzania - USSR

Tahadhari ya Kuvunjika Muungano wa Tanzania - USSR

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Tanganyika nayo itatawanyika vipande vipande.

Mbali ya huyu Mtanganyika huyu Mzanzibari, Tanganyika haitakuwa salama na ndio hata Waasisi wa Tanganyika waliusia sana kuhusu kuizulumu Zanzibar.

Zanzibar ni ya kulelewa na kufanikishwa kila wanachokitaka, wanahitaji kudekezwa kwa hali na mali, ila mkiendelea kuona ni chawa basi mjue hampo salama.

Natumai mmenielewa kwa kina kwani inabidi uzamie ndio utaona uhalisia wa umuhimu wa umoja uliopo, Zanzibar ni kanchi kadogo sana, ikiwa kuna mikoa mikubwa kuliko Zanzibar, tunashindwaje kuilea Zanzibar na kuondoa kionekanacho kama kero?
 
Zanzibar wapo tofauti na nyie, tatizo la bara na zanzibar kila mtu anajiona yupo sawa. Shutuma za kipumbavu kila mtu anampa mwenzie kiufupi wote wana matatizo.
 
Hiyo Tanganyika ni kitu gani kwanza.

Wako wangapi kwanza hao watanganyika wanaoipigania Tanganyika yenyewe 🐒
 
Muungaño hauwezi kuwa imara iwapo wànanchi wa pande mbili hawaafikiani.

Haiwezekani Muungano uwe imara kama Muungano huo unang'ang'aniwa na baadhi ya viongozi wachache tu kwa maslai ambayo hata hayajulikani.

Ili Muungano huu uwe imara inabidi wananchi waridhie.

Kuna umuhimu mkubwa iitishwe Kura ya maoni kwa wananchi wa pande zote mbili waamue kuhusu mustakabali wa huu Muungano.

Haiwezekani kuwe na Muungano imara wenye makandokando kibao Mara kero za Muungano, Mara viongozi tena mbunge anaibuka ndani ya bunge na kulalamika kuna upande unaiba ajira za upande mwingine. Mara kuingia huku lazima kuwe Kwa passport Ila kuingia kwingine kusiwe Kwa pasport.

Viongozi mwingine wa kiroho analalamika mbele ya Rais kwamba wananyimwa ardhi ya kujenga makanisa.
Raia wa kawaida nao wanalalamika mbona upande mwingine wanaruhusiwa kumiliki ardhi upande mwingine wakati upande mwingine hawamilikishwi.

Huu Muungano abadani si imara viongozi wasijifanye vipofu ki ukweli Muungano hakuna.

Kama ni ndoa basi ni ndoa mfu ndani baba analala chumba chake ,mama chumba chake Ila nje eti mnajiita wana ndoa abadani hiyo siyo ndoa.
 
Back
Top Bottom