Tahadhari ya ndoto inavyoshindwa kuniepusha na majanga yanayonikabili

Tahadhari ya ndoto inavyoshindwa kuniepusha na majanga yanayonikabili

Igombe fisherman

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Posts
2,178
Reaction score
3,865
Katika maisha yangu nimekuwa nikiota ndoto kadhaa. Zingine zinakuwa hazieleweki ila zingine zinakuwa na ukweli baada ya muda flani. Yaani kinatokea kama nilivyoota. Nimekuwa nikiishi hivyo kwa kwa siku zote za maisha yangu. Wakati mwingine nikawa najilaumu kwa kutochukua tahadhari kwa majanga yanayonipata kwani kuna ndoto nakuwa nimeoteshwa kabla hilo janga linipate. Mnamo kama miaka mitano zilizopita nikaanza kuzichukulia ndoto u serious kuzihusu ili kujinasibu na majanga hapo ndipo nilianza kushangaa inavyoshindikana.

Tuanze na ndoto hii mwaka 2019

Nilikuwa kisiwani flani hali ilikuwa tu ninzuri ya kihewa. (Kazi yangu ni kama jina langu hapa) na pesa tulikuwa tunapata ila kwenye hicho kisiwa hapakuwa makao makuu ya kambi yetu kwakifupi tulienda pale kwa ajiri ya kuna samaki wengi kwa kipindi kile na hujirudia kila mwaka hali kama ile kwa majira kama yale. Nilikuwa na wife pande za bukoba na alikuwa na mimba kipindi hicho. Sasa siku moja nikaota hivi.

Niko kwenye jengo flani kama kanisa hivi na linakabustani ka nyasi nzuri kama za uwanja wa mpira nikiwa na simu yangu tunaongea na wife na wife ananilaumu kwa kutokumpa mahitaji yake na simjari. Huku mimi katika ndoto hiyo nikijitetea kuwa hali ndo mbaya ndo chanzo cha kutomtimizia mahitaji yake.

Kitu hicho kilileta ugomvi wa kimaneno mpaka kila mtu akabwaga manyanga katika simu baada ya yeye kukata simu ndo nashituka usingizini. Nikagundua hiyo ni ndoto tu na maisha yakawa yameendelea lakini nikaamua kuifanyia kazi hiyo ndoto maana nilihisi ni tahadhari flani Mungu kanionyesha.

Tulimaliza mkataba wetu kazini kisha nikaenda kwa wife bukoba na maisha yakaendelea ila baada ya siku kadhaa mimba ya wife ikaharibika niko nae hapo. Mambo yalikuwa mengi kidogo ila tufupishe stori.

Basi kale kahela nilikotoka nako kule majuu kakawa kamekata. Maana alitakiwa akafanyiwe usafi flani tumboni kwa gharama kidogo. Sasa nikaanza kuitafakari ile ndoto nifanyeje ili maisha yasinishinde kama ndoto iliyonijia hapo nyuma maana naziona dalili za kutimia.

Nikapiga simu kule kisiwani nikasikia hali si nzuri. Nikapiga simu kisiwa kingine nikaambiwa hali ni nzuri tu tena nikaribu na hapo bukoba kisiwa kinaitwa misira.

Nikaamua kuingia pale na kazi nikapata maana sisi tunajuana wazungukaji wa ziwani huwa tunakutana walewale tunafahamiana.

Kweli maisha yakawa bomba tu hela napata na maisha yakaendelea. Ukipata nafasi unamzukia wife na mambo mengine. Kila nilkipiga simu kule nilikotoka nasikia hali ni mbaya hivyo mimi nikaona ile ndoto imenisaidia maana waliobaki kule wanakiona cha mtema kuni.

Sasa baada kama ya miezi miwili hali ikachange hapa ikawa mbaya sana harafu kule ikawa nzuri. Ikadumu kama wiki mbili hivi hali ikiwa ni ileile na wife alikuwa na uhitaji wa pesa kwa inshu flani sasa akawa anahitaji hiyo pesa na mimi napata hela ya vocha na kula tu kule.

Marafiki zangu wa kule wakawa wananihitaji ila nikawa sipokei simu zao maana sikutaka kwenda kule kwa hicho kipindi. Sasa wamenitafuta kwa namba ya wife na wakamwambia kuwa mwambie jama aje tupige kazi mambo yameshakaa sawa.

Sasa baada ya hayo maongezi na huyo jamaa yangu akaniirukia hewani na kuanza kunituhumu kama mimi ni mzembe wa kutafuta na sina uchungu na maisha.

Sasa katika hayo maongezi yakawa marefu huku nikipangua hoja kadha na mimi nikawa natafuta sehemu yenye utulivu huku tuukiongea nilijikuta nimelala kwenye vinyasi flani huku badala ya maongezi umeshakuwa ugomvi.

Kila mumoja wetu akiwa hataki kushuka mwisho wa siku akasema ye anaona kwa hali ile hatutofika mbali na mimi nikamwambia kama vipi tuishie hapo hata tulichuwa tunaunganishwa nacho kilishaondoka(mimba) ndo akakata simu.

Baada ya kukata simu ndo nikakumbuka ile ndoto na mazingira yake ni yaleyale nikiwa kwenye kania la Othodox pale misira na nilikuqa sihawahi fika pale kule kabla ila nilishapaota.

Hivyo tahadhari niliyochukua haikunisaidia. Nitaendelea kuleta zingine ndoto katka comment kutetea hoja yangu
 
Ndoto ya pili niliyoshindwa kujiokoa japo nilichukua tahadhari 2022. Ikiwa mwezi wa kumi nilipanga nikale sikukuu za mwisho wa mwaka sehemu flani. Nilichabaki nawaza ni kutafita hela kwa ajili ya kutimiza hilo sasa mwezi wa 11 nikapata ndoto moja kati ya mashemeji zangu ambaye anaishi hapo tunaongea nae katika simu na maongezi yetu ni hivi. Siku ya christmass yenyewe ananiambia. Ila shemu ulivyokuwa umepanga imeenda tofauti. Na mimi namjibu shemu huwezi amini hapa nilipo nina tsh 70k tu mpaka nimechananyikiwa. Naile ndoto inanionyesha niko kwenye kabaa frani na nakajua na kako kisiwani kerebe na ndipo nilipokuwa kile kipindi. Ile ndoto nikaanza kuitengenezea mazingira ili isitimie hivyo nikaona hapa inawezekana hali haitokuwa nzuri kwa mwezi 12 hivyo natakiwa nitunze pesa nyingi ili mwisho wa mwaka niweze kutimiza nia yangu ili niipinge hii ndoto. Nilipoangalia hali pale kerebe nikaona siyo nzuri nikaamua nihamishie chombo kisiwani goziba maan kule hali ilikuwa nzuri. Kufika goziba nikaanza kupata samaki sana. Yaani ndani ya siku saba tu nilikuwa kama na 500k bosi akaanzaa kunisifia kuwa nilijiongenza na mimi chombo changu kinalipia gharama vyombo vingine. Sasa si zikaanza fainali za kombe la dunia. Chombo tulailaza hapo ili tukalilaksi tu ufunguzi sijui qotar na nani wanacheza. Kuamkia kesho upepo umepiga na chombo kimepasuka. Sasa bosi kumwambia akasema wewe ulitorola bandali salama kwa maegesho umepeleka huko chombo kimekufa usubiri sana. Sasa nikaanza kutumia zile pesa. Si unajua tena mabo ya kombe la dunia nikuangalia mochezo tu na kula kulala. Kuja kwamba chombo imekaa sawa ilikuwa ni tarehe 19 /12/2022 ndiyo nikapakia kuanza kazi. Kumbuka kule nilikotoka wanatengeneza tu pesa na kilichokuwa kinaniuma ni kwanini nimejaribu kuibadiri future na imeshindikana. Basi bwana tarehe 22 ndo nikatoka kule kuja huku kufanya kazi hivyo nikafanya kazi siku mbili tu nikakaa kula christmass. Sasa ile siku ya xmass sasa niko ndani ya bar flani ndo yule shemu ananipogia simu baada ya mimi kum wish ua la merry christmass kule fb ndo ananipigia tukaongea ndo nakuja kukumbuka kuwa kilekile nilichokiota ndicho kimebaki. Tukio la tatu haina haja ya kulisimulia labda baadae kidogo lakini nataka wenzangu mniambie. Huwa mnaepuka vipi majanga ambayo munaonyeshwa katika ndoto. Mbona mimi nikipanga kuyaepuka najikuta nimeyashiriki? Kabla ya hapo walikuwa wananiambia niwe nachukua tahadhari lakini sasa hivi nimeshaacha kuchukua tahadhari. Hayo ni mawili tu katika matano niliyoyachukulia tahadhari
 
Back
Top Bottom