mkumbwa junior
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 835
- 1,608
Mwaka 2014 bro alinunua gari kwa msanii mmoja mkubwa wa Bongo flevaa,,Siku walokubaliana biashara ifanyike kulikuwa na tamasha la Fiesta(kilele) DSM akamwambia baada ya shoo tu wakutane eidha usiku au asubhi sana maana saa nne anasafiri kwenda SA...basi bwana sisi asbuhi na mapema tukaenda home kwake(mimi kama shahidi)na yeye tulimkuta anaishi na msanii mwenzake(mkubwa)akawa shahidi tukafanya mauziano tukampa hela CASH kulingana na makubaliano,kadi akatupa Copy kwa madai Og ipo kwenye nyumba yake ingine ni mbali hivyo akitoka SA atatupatia..tukakubali ukizingatia ni mtu maarufu,,ebwanaa eeh ile kadi ilizingua balaa baada ya miezi minne tunagundua kumbe ile gari alikopa Bank na kuiweka kama dhamana,,baada ya kusumbuana sana bro alifanikiwa kuizua ile gari kwa mtu wa mkoani huko na kadi ile ile copy,,sijui walimalizanaje huko badae