Tahadhari za kuchukua uingiapo nyumba za wageni

Hivi huo.muda.natoa wapi, labda kwa dar mana dar nzima haina lodge nzuri wala guest ukitaka kufurahi dar tafuta hotel
 
Kuna zile gesti unaingia jumba kubwa vyumba vyote viko ndani. Nililala gesti moja yakanikuta makubwa. Asubuhi mtu aliyelala chumba kinachotazamana mlango na mlango wa chumba nilicholala aliamka mapema akaenda bafuni. Aliporudi akaanza kulalamika nimemuibia simu chumbani kwake kwani aliacha mlango wazi akaenda bafuni kuoga. Akaripoti kwa mwenye nyumba. Mwenye nyumba naye akaita polisi wakaja huku wakiwa na silaha za kivita. Polisi wakapekua begi langu kutafuta simu. Niliwaambia polisi sikuingia chumbani kwa mtu huyo na wala sikuchukua simu yake. Basi polisi walinipeleka kituoni kwao kwa uchunguzi zaidi wakataka kunifungulia kesi nikawaambia huyu mtu ajaje simu yake ilikuwa ya thamani gani akataja. Basi nikawaambia polisi hapa sina hiyo hela ila ipo benki twendeni benki nikadroo niwape mmpe huyu mtu na mimi mniachie huru kwani mimi ni mgeni mji huu kuhudhuria kesi sitaweza naishi mbali. Nikadro hela nikawapa na wao wakampa huyo mtu akapotelea migombani sikutaka kujua sana kama nimetapeliwa au vipi. Tujihadhari
 
Tuchukue tahadhari kubwa kwenye nyumba za kulala wageni huwa kuna visa na mikasa mingi sana. Ukaguzi ni muhimu, vitanda huwa na mambo ya kishirikina, unakukua kuna hirizi kwenye chaga, au mavi ya mnyama fulani chini ya godoro. Haya yaliyoelezwa kwenye uzi ni likely kuwepo kwenye nyumba za kulala wageni
 
Saf kwa feedback mana apa natoa code wadau wanabwabwaja ufila tu apa
 
Uwezekano ni ulitapeliwa mkuu ila bora ulilipa kuliko maigizo ya wizi. Ni kama ulinunua muda wanaojaribu kuupoteza.
 
Ni vizuri pia ukajua wa chumba cha pili ni mtu wa aina gani, anaweza kuja kukuletea sokomoko kuwa aliacha mlango wazi ukaingia kwake na kumuibia akitanabaisha mlikuwa wawili tu eneo hilo na anakushuku ni wewe tu ndiye uliyeingia chumbani kwake na kumuibia, atakuganda balaa mpaka polisi waje ulipishwe
 
Sasa kama ww mkuu hapa hata tahazari isingekusaidia. Vingine misala tu unakutana nayo ata uwe na tahazari
 
Kama mlikua wawili tu eneo husika, alipoacha mlango wazi alikutaarifu?

Na kwa nini aache mlango wazi wakati hapo ni guest House?

Kama ulienda kwa uzinzi ni bora ulimaliza kesi hivyo, ila kama upo pale kihalali, mpaka mkeo anajua, IGP ndio angekuja kuamua hilo varangati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…